BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Tuesday, September 28, 2010

Mapinduzi ya filamu hapa bongo.

Na haya ndio mapinduzi ambayo huwa tunayawaza na tunayazungumzia kila siku , naona sasa yameanza



 
wasanii wa filamu hapa nchini
Nazungumzia uzinduzi wa filamu ya Black Sunday iliyosimamiwa na Pilipili Entertainment ulivyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa sinema wa Mlimani City ambapo iliigizwa kama Ulaya

Waigizaji waalingia katika gari la kifahari, huku kukiwa na wageni na wadau wa filamu kukiwepo na red carpet huku mahijoano kutoka vyombo mbalimbali yakifanyika


bila shaka huu ni mwanzo na itakuwa kila filamu kwani wakati filamu hii inazinduliwa Bongo huko Kenya nako ilikuwa inazinduliwa katika kumbi zipatazo saba.


Mungu saidia Tanzania saidia Tasnia hii ya filamu ikue

Tuesday, September 21, 2010

KANUMBA AMTEMBELEA MZEE KIPARA KUTAZAMA HALI YAKE!.



 Mzee Kipara.
Bila shaka umesikia habari kupitia vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vinavyomilikiwa na Global Publishers kuhusu hali ya muigizaji mkongwe nchini,Fundi Saidi maarufu kama Mzee Kipara.
Habari hizo zilikwenda sambamba na habari kwamba msanii huyo mkongwe,amesikitishwa na hali ya “kutelekezwa” na baadhi ya wasanii aliowasaidia katika kuinua kama sio kuanza safari yao katika kazi za sanaa kama vile Steven Kanumba na Ray Kigosi.
 Kanumba na Mzee Kipara wakizungumza.
Katika kuthibitisha kwamba kimsingi hakuna uhasama au “kutojaliana” baina ya Mzee Kipara na wasanii hao,hivi karibuni Kanumba alimtembelea Mzee huyo nyumbani kwake maeneo ya Kigamboni jijini Dar-es-salaam.

Mzee KIPARA anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu ambapo kwa mujibu wake ameeleza hospitali kadhaa alizoenda hawaoni tatizo japo miguu inamuuma

 Kanumba akimpatia Mzee kipara kiasi cha pesa cha kumsaidia.

Monday, September 20, 2010

SHIRIKISHO LA WASANII WA FILAM TANZANIA (TAFF) LAZINDULIWA RASMI LEADERS CLUB


 Wadau wa filamu na wasanii katika viwanja vya leaders dsm.
 
Shirikisho la Wasanii wa filam Tanzania (TAFF) limezinduliwa rasmi katika viwanja vya Leaders Club na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wasanii wa filamu.Akifungua tamasha hilo Rais wa shirikisho hili Saimon Mwakifamba amesema kwanza wameshukuru kwa serikali kuanza kulitambua shirikisho lao na kazi yao ya kwanza kuanza nayo ni kutetea maslahi ya wasanii wa filam kwani mapato wanayopata ni madogo sana,vile vile wamedhamiria kuanzisha tamasha la filamu litakalojulikana kama Nyerere film festival litakalofanyika December mwaka huu.

 Diamond musica ilisherehesha uzinduzi huo.

Sunday, September 12, 2010

“WADAU NA WASANII WA FILAMU HAPA NCHINI TUKUBALI KUKOSOLEWA”


 Kanumba (Msanii wa filamu Tanzania).
Hivi sasa sanaa ya filamu inazidi kukua nchini Tanzania. Inatia moyo sana kuona watu wa mataifa mengine wanaangalia filamu ambazo zinaitwa “za kibongo”. 
 Msanii wa filamu Irene Uwoya kutoka Bongo.
Pamoja na hayo kazi kubwa bado ipo mbeleni.kuna haja ya serikali kutoa support ya kutosha ili kuzidi kuinua sanaa hiyo. Marekani ipo hapo ilipo kwa sababu ilitangaza sanaa na sera zake za mambo ya nje kupitia kwenye filamu. Ikulu ya Marekani ina kitengo cha kushughulikia masuala ya filamu.Kama filamu itaonekana haijakaa “vizuri” kwa mujibu wa taratibu zao,basi haitoki.
Frank (Msanii wa filamu Tanzania).
Mmoja wa wasanii wa filamu hapa nchini Frank alifanya mazungumzo na waandishi na akasema lazima wasanii na washika dau wote katika nyanja za filamu wakubali kukosolewa. Unapokubali kukosolewa unajipa nafasi ya ushindi kwani maana yake ni kwamba kesho utafanya kizuri zaidi.Lakini pia ipo haja ya wakosoaji kutokuwa “wabezaji”. Unapokosoa basi useme pia sababu zako na utoe ushauri wa kujenga kwamba nini kifanyike.Kwa mwendo huo filamu za kibongo zitazidi kupata jina na sio ajabu kabisa siku moja nasi tukaona wakina Denzel Washington wa kikwetu kutokana na sanaa hii hapa bongo.
 Msanii wa filamu Ray kutoka Bongo.

Wednesday, September 8, 2010



Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni muda ambao Waislamu duniani kote wanafunga, wanaswali na kufanya matendo mema. Aidha ,ni wakati wa kutafakari na kuimarisha imani zao,kutenda mema, kuwasaidia wenye shida na kuwa na huruma.
 Ibada ya Eid El Fitri.

Wadau wote wa blog hii ya www.filamutanzania.blogspot.com na www.thazealottz .blogspot.com pia. ninapenda kuwatakia Waislamu wote wa Tanzania Eid El Fitri njema. Muda huu wa kujitafakari unatukumbusha kuwa maadili ya uislamu wema, kujali wengine, kuhudumia jamii, ushirikiano na huruma ni amali ambazo sisi kama watanzania tunazithamini sana na ambazo kwa hakika zimechangia sana katika tamaduni nyingi duniani kote.

Wenzetu waislamu wakisherekea Eid El Fitri

Nawatakia Eid El Fitri njema wadau wangu.

 mmmh! Misosi mbalimbali ya Eid unaona tende!?



Frank Aman Mawenya(Tha Zealot).
 Eid El Fitri njema

Tuesday, September 7, 2010

New SIBUKA TV yaanza kurusha vipindi kupitia king'amuzi cha star time.


Kupitia TV SIBUKA nuru ya jamii fahamu vipindi vipya leo usiku tarehe 7/09/2010.hii kwa watazanaji wa king'amuzi cha startime na watumiaji wa satelite tuu kwa hivi sasa.

RATIBA YA TV SIBUKA.

1.   DOCUMENTARIES - CRI.
2. MOVIES - HARRY POTER (HALF PRINCE).
3. SERIES & SOAPS – FIRST SUNDAY.
4. TV SHOWS – GROLY CHURCH OF CHRIST.
5.  MOVIES (DRAMA) – GIFTED HANDS (THE BEN CARSON STORY).
6. MUSIC MIX – BONGO (ONE HOUR).
7.  RELIGIONS – CHRISTIAN SONGS.
8. DOCUMENTARIES – ENVIRONMENT LAKE VICTORIA.
9. MOVIES – UP.



Kila kukicha wasanii wamekuwa wakilalamika kuhusu kipato wanachovuna kutokana na kazi zao.Lakini mpaka leo kilio hiki hakijatafutiwa ufumbuzi wake, kila kukicha ni pirates wanaolalamikiwa na wasanii.Ebu fikiria kibanda kama hiki pichani kinaingiza watu wapatao 30-50 ambao lila mtu analipa 500 mpaka 300 kwa picha moja,kwa ujumla unapata kama 15,000 mpaka 20,000 kwa session moja na unakuta kwa siku kuna sesion mpaka 5,Je? msanii ni shs ngapi anapoteza kwa watu kama hawa.Je? watu wanaoingia humu wangeamua kununua kwa kila tape moja shs 5000 ni shs ngapi msanii angepata.Yote haya ni kwasababu hakuna sheria za kuwabana watu kama hawa hata ukiwakamta utamfungulia mshataka kwa sheria ipi? Hiki ndicho kilio chetu kila siku wasanii.Hawa ni wachache tu wako wengi sana huko mitaani wanaorudufu kazi zetu.Ni lini serikali itatilia mkazo kazi zetu ili tufaidike kutokana na kazi zetu?,
Baadhi ya bidanda vinavyoonesha filamu za kibongo.
Msanii Chopa akiangalia kwa masikitiko makubwa bango la matangazo.

KANUMBA THE GREAT FILM MZIGONI KUTOKA NA UNCLE JJ.

Kanumba the greatest na Jeniffer katika scene.

MSANII nyota wa filamu na maigizo hapa nchini Kanumba ama the Great ameanza kuandaa kazi yake mpya iitwayo UNCLE JJ akiwa na wasanii vijana wadogo wale waliokamua nae vizuri katika THIS IS IT. Safari atakuwa Bush na anasema itakuwa na full vituko.filamu hii ikiwa imeandaliwa chini ya kampuni yake ya KANUMBA THE GREAT FILM na akitumia vifaa vyake mwenyewe ambavyo kanumba anasema kwa sasa hatarudi tena katika suala la kukodi kutokana na kununua vifaa hivyo kuanzia kamera mpaka vifaa vya editing. 

Akizungumzia kuhusiana na ma-actors walioshiriki katika filamu hiyo ni watoto waliokuwepo katika filamu ya THIS IS ITambao ni Jenifa na Patriq na anasema kuwa toka awatambulishe katika ulimwengu wa filamu Jenifa na Patriq kupitia filamu hiyo wamekuwa gumzo mtaani hata kwa watoto wenzao kila wanapopita inawalazimu kupiga picha na wenzao jambo ambalo nao kwa sasa wanaanza kuzooea hawakatai maana ameshawafundisha nini maana ya kuwa Star,mbali na hayo anawasimamia shuleni kuhakikisha wanasoma vizuri na kupata elimu bora hii ni kutokana na uwezo wao katika sanaa.

 Patric na Jeniffer wakiwa na watoto.
Katika filamu hiyo amemtumia Farid Uwezo kama camera man ambae ndio mara ya kwanza kufanya nae kazi,na Farid alimweleza Kanumba kuwa kila mara kwa mda mrefu sana alitamani kufanya kazi na yeye na leo ndoto yake imetimia tena akitumia camera yake ya kiwango cha juu,
 Farid Uwezo akiwa na Kanumba na Camera yake mpya.
Jamani hiyo ndio camera yake Kanumba kutoka katika kampuni yake ninayomiliki kwa sasa ‘ni kifaa ninachojivunia kukinunua maana uwezo wake ni mkubwa mno katika picha pia ni producer wachache sana nchini wanaotumia na kumiliki camera kama hii,ni SONY DSR 390’ asema kanumba.

Hiz ni picha za baadhi ya scene zitakazo kuwepo katika filamu hiyo ya UNCLE JJ.
 Jeniffer akifanya mambo katika Scene.
Kanumba the greatest na Jeniffer katika scene.
 Patric na Jeniffer katika Scene.

Saturday, September 4, 2010

INI EDO, TONTO DIKE WAPATA SKENDO YA KUSAGANA.


Tonto Dike


Tangu Nollywood diva, Ini Edo aingie rasmi katika ndoa na, Philip Ehiagwina, mfanya biashara maarufu anaye fanyia shughuli zake marekani, amekuwa akipatwa  na uvumi kuwa ana mahusiano na wanawake wenzake, kutokana na taarifa tofauti tofauti zinazovuma chini chini nchini Nigeria.
Kwamba katika ndoa yake na Philip kuna migongano na inasemekana kuwa amekuwa na wakati mgumu katika ndoa yake hiyo. Kuna habari zinazo vuma chini chini hivi sasa kuwa ana mahusiano na mwanamke mwenzake tabia inayotambulika kama ‘lesbianism’.



Ini Edo

Skendo hiyo ambayo inamuhusu yeye na Mwigizaji mwingine kutoka Nollywood, Tonto Dike na Ini Edo ambao inasemekana kuwa wote walionekana wamelewa hivi karibuni kwenye location na walionekana wakifanya vitendo vilivyo washtua watu. Kwa mujibu wa mtoa habari amesema kuwa,Ini Edo and Tonto, wameonekana wakiwa usiku mmoja wakiwa pamoja na wameonekana wakifatana kama mapacha katika sehemu mbalimbali za starehe kama Alpha Beach, Lekki area huko  Lagos.

Tonto Dike anaishi maeneo Abraham Adesanya huko Ajah area Lagos.Na kwa mujibu wa habari kutoka katika mtandao wa  www.nigeriafilms.com ulifanya utafiti na kuona hali ya ulevi na utupu umeingilia maisha ya wanadada hao.