KATIKA kubororesha soko la filamu kuanzia mwakani mwezi wa kwanza bei ya filamu itapanda na kuletwa bei mpya ya filamu, lakini si kupanda tu bali vile vile kutakuwa na bei moja kwa wasambazaji wote tofauti na ilivyo sasa, ambapo kila msambazaji anakuwa na bei yake kiasi cha kuwachanganya wanunuzi wa filamu kwa hapa nchini.
Haya yanafanyika kwa kufuata utaratibu uliopangwa na TAFF kwa wanachama wake.
Bei ya sasa sokoni ni tata kwani wakati kauli ya pamoja ya wasambazaji baada ya kushusha bei ilipangwa wauze filamu kwa bei ya Tshs. 2,000/= hadi 2,500/=, kwa sasa kuna kampuni ambayo wanaamini kuwa ni kubwa wao wanauza Dvd moja kwa Tshs. 1,600/= hadi 1,000/= wadau wanaamini kuwa kukiwa na chombo cha kusimamia bei na wasambazaji kwa ujumla soko litaenda mbele.
Wasambazaji kwa sasa tayari kupitia Shirikisho la vyama vya filamu Tanzania (TAFF) wameunda chama chao kinachojulikana kama Tanzania Film Distributors Association (TFDA).
Bei mpya ambayo imependekezwa na TFDA ni Tshs. 3,000/= kwa Dvd moja hii ni bei ya jumla, hata hivyo tumegundua kuwa pamoja na misuguano kuhusu punguzo la bei za filamu inayoletwa na wasambazaji haina faida kwa mnunuzi wa mwisho kwani Mmachinga akinunu kwa bei yoyote yeye atauza kwa bei kubwa tu, na Wamachinga ndio wenye kupanga bei huku wakiangalia maslahi zaidi kwao.