UNAPOTAJA majina ya wasanii wakongwe wa filamu nchini, huwezi kuacha jina la Jacob Stephen maarufu kama JB au Erick Ford. Huyu ni msanii aliyejizopatia umaarufu katika tasnia hiyo.
Unakumbuka kikundi cha Mambo hayo? Bila shaka utaafiki kuwa ni miongoni mwa vikundi vya maigizo vilivyowika na kuvuta hisia za wengi katika miaka ya 1990. JB ni mmoja wa waliounda kikundi hicho, ana umri wa mika 13 katika fani.
Kazi inayofanywa na JB si rahisi kwa maana inamlazimu kuishi kambini kwa siyo chini ya miezi sita katika mwaka na ni mume wa mtu pia ameokoka.
“Kwa sababu ninamiliki kampuni ya kutengeneza filamu, ninaongoza na kucheza filamu nakosa muda wa kulala nyumbani kwangu, katika mwaka mmoja nagawanya miezi sita kambini na miezi sita nalala kitandani kwangu,” nasema JB na kuongeza;
“Mimi ni mtumishi wa Mungu kazi yangu inanilazimisha kuingia sehemu mbalimbali ambazo hazistahili kwa mtu aliyeokoka wakati huo huo napaswa nielimishe jamii hii ni changamoto kubwa sana kwangu,”.
Anasema, wakati mwengine jamii inashindwa kumuelewa kwa sababu anaingia katika majumba ya starehe na kwamba muda wa kushiriki mambo mbalimbali na jamii yake au ndugu anakosa.
“Hata majirani ninaoishi nao siwafahamu, misiba au vikao vya ndugu nashindwa kuvimudu kutokana na kazi hii, namshukuru Mungu kwa sababu naamini kuwepo kwangu jukwaani ninapowakilisha ujumbe kwa jamii ni mchango wango mkubwa katika kushirikiana nao mambo mengi,” anasema.
JB anasema, anatarajia kuifanya kampuni ya Jerusalemu Filims kuwa ya kimataifa na kwamba atajikita katika kucheza filamu za burudani lengo likiwa ni kuwafurahisha watu baada ya kuchoka katika mizunguko ya simu nzima.
“Kama nilivyotangaza kuwa sitafanya filamu nje ya kampuni yangu nitaendelea kuboresha kampuni yangu na ninatarajia kuifanya kuwa ya kimataifa na kwa kuanza nitatengeneza nembo itakayoitambulisha hata sehemu yeyote ukiniona,”alisema.
Anasema, atabadilisha mfumo wa filamu katika kampuni hiyo na kuwa za kuburudisha ili aweze kuwaburudisha mashabiki wake na kwamba atalitaka soko la filamu kwa kiwango kikubwa.
“Ninacholenga nikuwarejezea watu mawazo mapya wanapokuwa wamechoka katika mizunguko ya kazi lakini pia kuinua vipaji vya wasanii wengi na tayari hilo nimelianza katika filamu ninazoziandaa zimetawaliwa na wasanii chipkizi,” alisema.
JB anasema, matarajio yake hayo ni kuwa msanii wa mfano wa kuigwa nchini kama ilivyo kwa msanii mashughuri wa Nigeria Amitabh Bachchan na Bollywood.
Akizungumzia kukua kwa tasinia ya filamu nchini JB anasema Tanzania inashika nafasi ya tatu kati ya nchi tano za Afrika Mashariki na kwamba kinachochelewesha tasinia hiyo kukua ni kuchelwa kuanza kwa sanaa nchini.
“Maendeleo ya filamu yapo tatizo kuwambwa linaliifanya iwe nyuma ni kuchelewa kuanza kwa sanaa hiyo lakini tukikaza buti na kushirikiana tunaweza kufika mbali zaidi,” anasema na kuongeza:
“Filamu ya Tanzania imeanza kukua mwaka 2009 wenzetu walianza zamani na wanaelimu wanapata ushirikiano kwa jamii yao hivyo lazima waonekane wamepanua wigo wa sanaa kwa kiwango kikubwa,”.
JB anasema, wasanii wachanga wanaharaka na uigizaji, hawajichunguzi kama wanauwezo na kwamba uigizaji ni zawadi kutoka kwa Mungu.
“Usanii sio rahisi kama unavyofikiria hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, sio kila mtu anaweza na kupenda sio sababu ya wewe kuweza kuigiza kinachotakiwa ni kujichunguza kama anaweza na baadaye aanza kwa kufuata utaratibu wa sanaa,” aliasema.
Anasema wasanii wengi wanaharaka ya kupata mafanikio na kuwa wanasahau kuwa kila kitu ambacho ni mpango wa Mungu kinapaswa uende taratibu.
JB (40) ambaye alifanya bishara ya mahindi katika kipindi cha miaka 10 kabla hajaanza kazi ya sanaa anasema, amefanikiwa kwa kiasi na kwamba anamiliki kampuni yake ya filamu na maduka mawili ya nguo.”
Anasema anachojivunia katika maisha yake ni wokovu na tuzo ya ymsanii bora wa kiume aliyoipata mwaka 2009 na kwamba ni msanii anayeheshimiwa na kupendwa na kila mtu.
“Katika maisha yangu ya usanii sijawahi kuwa na skendo chafu, napendwa na watu wa kila aina kutokana na ucheshi wangu nilionao, yote hii ni kwa sababu Mungu anasimamia maisha na kazi zangu pia.
JB alifanikiwa kuchukua mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mwaka 1992 ingawa hakuweza kuajiriwa, ni mzali, elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya St Joseph, kidato cha kwanza hadi cha sita aliipata katika shule ya Popatlal.