BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Tuesday, December 6, 2011

Ramsey awaasa wasanii wa muvi bongo..


VIPAJI vina nafasi kubwa katika ulimwengu wa sanaa, lakini kuna wakati lazima mhusika atafute elimu kwa ajili ya kulinda na kuendeleza kipaji chake.

Hayo ni maneno ya mwigizaji mahiri wa filamu Bongo, Hashim Kambi Ramsey aliyoyatoa hivi karibuni katika mazungumzo yake na Mwanaspoti.

Wakati naanza kuigiza nilikuwa najua ni kitu cha kujifurahisha tu, nilifanya hivi huku nikiendelea na shughuli nyingine, anasema Ramsey.

Lakini nimebaini uigizaji ni kazi. Inakuhitaji mtu uwe na taaluma hiyo ili uweze kudumu nayo katika kiwango bora.

Kinachosikitisha tu ni kuwa kuna hili tatizo la gharama kuwa kubwa kwa masomo ya filamu.

Akielezea zaidi, anasema kwamba wasanii wanaweza kujiendeleza kwa njia ya mitandao ya filamu, kama anavyofanya yeye.

MAGIC MONEY SOKONI HIVI KARIBUNI.


'PESA SHETANI ASIYE EPUKIKA KATIKA DUNIA HII YA SASA NA USIOMBE ABISHE HODI NDANI YA FAMILIA KABISA'' ...KUMKANYWA NA KUPEWA TAHADHALI KWA MTU NDIYO KUMTIA HAMASA NA MUWASHAWASHA KUITIKIA KIU YA NAFSI YAKE YA TAMAA YA PESA NA HAPO MAISHA YA KUKIMBIA DAIMA HUANZA NA NDIYO MATOKEO YAKE KAMA SIO KUKOSANA NA NDUGU AU MPENZI/MUME/MKE WAKO...MTIZAME BINTI HUYU NAMNA NDOA YAKE INAVYO TIBULIWA NA SHETANI (PESA)


CAST
Daudi Michael (DAUDI)
Hemed Suleiman (ERICK)
Halima Yahaya (SANTANA)
Msafili Njechele (BUGO)
Ibrahim Lipili(NYANGO)
Ratifa Idabu (BADRA)


STORY
Daudi Michael
SCRIPT
Daudi Michael
EXCTIVE PRODUCER
D.Production
(A DAUDI MICHAEL FILM PROMO)

Sunday, December 4, 2011

SAJUKI AFUNGUKA KUGAWANYIKA KWA WASANII...

MWIGIZAJI na mwongozaji wa filamu Bongo, Juma Kilowoko Sajuki, amesema watayarishaji wa filamu wamegawanyika katika makundi, ingawa ni vugumu mwingine kulibaini hilo.

Akizungumza na jukwaa hili nyumbani kwake Tabata Bima, jijini Dar es Salaam, msanii huyo ambaye kwa sasa anasumbuliwa na tumbo, anasema kuwa mara nyingi wale ulio karibu nao ndiyo hukuzunguka.

Sisi wasanii tayari tuna makundi japo tunafanya kazi moja, kwa mfano mimi rafiki zangu labda Frank au Dino, basi watakuwa ni hao tu, hata linapotokea jambo kama la msaada wao ndiyo watawajibika, alisema.

Hata kama mtu akiongea na mwingine atasema kuwa huyu jamaa hajichanganyi na watu, lakini ukweli tunajuana kuwa kila mtu na mtu wake. Msanii huyo alisema japo jambo hilo lipo, lakini si rahisi kuyataja makundi hayo. Kutokana na hali hiyo, anawataka wasanii kujilazimisha kujenga umoja wa kweli kuliko ilivyo sasa.

MABINTI WANAOTETEMESHA VIDUME NOLLYWOOD..

MERCY Johnson ameshaolewa. Nani anafuata? Ndiyo swali wanalojiuliza mashabiki wa filamu za Nollywood, asilimia kubwa ya wasanii wa kike hawajaolewa na wengine hawana hata mpango na hayo mambo.
Wengine walishaolewa wakaachika kutokana na kuendekeza starehe na kushindwa kutulia kwenye ndoa zao. Hii ni orodha ya mabinti ambao hawajaolewa na wanaotetemesha wanaume Nollywood. 

Funke Akindele
Huyu binti ana mafanikio makubwa kikazi na ni miongoni mwa wasanii wanaolipwa sana. Ana umri wa miaka 35, hana skendo nyingi za mapenzi kama walivyo mastaa wengine wa Nollywood.
Yuko kwenye uhusiano wa kudumu na huenda muda wowote akatamka jambo kwa marafiki zake.
Amesomea sheria kwenye Chuo Kikuu cha Lagos. Baadhi ya filamu alizowahi kufanya ni kama Jenifa, Omo Ghetto na Return of Jenifa Part 2. 

Rita Dominic
Sura na umbo lake vinadanganya watu wengi sana, ukimwangalia kwa haraka unaweza kudhani ana umri wa miaka 25, lakini kwa taarifa yako ana miaka 37 sasa na bado pia yumo kwenye kundi hilo la mabachela.
Mambo yake ya uhusiano wa zamani hayajafunuliwa sana lakini aliwahi kuwa na uhusiano na msanii mwenzie, Jim Iyke, hususani alipokuwa anaishi maeneo ya Wemabod Estates, Ikeja. 

Genevieve Nnaji
Miaka yake ni 32 na anatafsiriwa kama nembo ya filamu za Nollywood Afrika na Dunia nzima. Ni miongoni mwa mabinti matajiri Nigeria, lakini bado hajabahatika kufanya maamuzi magumu ya kuachana na ubachela.
Ana mtoto mmoja wa kike na awali alishavumishwa kuwa na uhusiano na Makamu wa Rais wa zamani wa Nigeria, Abubakar Atiku. 

Chika Ike
Ni mzuri na ana mvuto. Aliolewa lakini baada ya muda akaachika kwa sababu ambazo marafiki zake wa karibu waliziita za kitoto na ni binti wa kuendekeza sana starehe. Amenunua Range Rover ya kisasa na amefungua saluni za kisasa jijini Abuja, kama ni fedha anayo. 

Uche Jombo
Anawatoa udenda wengi. Lakini rafiki yake wa karibu amedokeza kwamba huyu binti hana mpango wa kuolewa sasa hivi, akili yake imekaa kibiashara zaidi. Anatengeneza fedha sana na anajua kuzitumia.
Anaishi maeneo ya Lekki jijini Lagos. Ametamba na filamu kama Secret Fantasy, Endless Lies, Kiss and Tell, Silent Scandal na Home in Exile. Miaka yake ni 32 na ni msomi wa Chuo Kikuu cha Calabar, Nigeria. Aliwahi kuwa na uhusiano na Ikechukwu Uche ambaye ni mchezaji. 

Monalisa Chinda
Ni bachela mzoefu. Aliolewa akazaa mtoto mmoja maisha yakamshinda akaamua kurudi kwao na sasa maisha yanaendelea kwa staili ya kujirusha kwa wingi.
Mwanaume waliyeachana naye ameshaoa lakini Monalisa bado yupo yupo ingawa inaelezwa wanaume wengi sana wanamnyemelea. Amesomea sanaa kwenye Chuo Kikuu cha Port Harcourt kwao Nigeria. 

Stephanie Okereke
Kila kukicha ana skendo na sura yake haikosekani kwenye kurasa za mbele za magazeti ya udaku. Kwenye masuala ya urefu na uzuri kote amesheheni.
Alishawahi kuolewa pia akaachika sasa hivi yuko kwenye penzi zito na jamaa mmoja anaitwa Linus Idahosa. Hakuna anayejua ni lini wana mpango wa kuoana.

MATANGAZO YA BIASHARA HAYA LIPI.... Ray

NYOTA katika tasnia ya filamu Bongo, Vincent Kigosi (Ray), amesema matangazo ya biashara hayalipi na ndiyo maana hashiriki katika kutengeneza matangazo hayo kwa sababu hayana faida kwake.

Si kama sipati matangazo ya biashara kwa ajili ya kutangaza bidhaa, fedha wanayotoa wahusika ni ndogo sana kiasi cha kukatisha tamaa, siwezi kutumika katika matangazo kwa pesa ndogo wakati nikitengeneza filamu naipata zaidi ya hiyo, alisema Ray.

Kwa wale wanaopenda sifa za kuonekana bila faida waache tu wafanye, lakini mimi msimamo wangu upo kimaslahi zaidi.

Msanii huyo alisema kuwa tatizo la matangazo hayo pamoja na kuwa malipo ni kidogo, lakini hayana ukomo wa muda wa kutumika. 

Mwenye bidhaa husika ana uwezo wa kulitumia hata milele bila kuendelea na malipo mengine, sasa hii si halali kabisa, aliongeza.

Mara nyingi makampuni hunifuata, lakini kila linapofika suala la malipo na ukomo wa tangazo wanakimbia, kuna tangazo ilitakiwa nilifanye, lakini baada kuambiwa kuwa nitalipwa dola 2,500 (Sh 223,864 za Kenya) na litatumika milele bila malipo ya ziada nilikataa.

Msanii huyo alisema kama kuna kampuni inataka kufanya kazi naye anaikaribisha, lakini ikubali kutimiza masharti yake kwa kuwa na mkataba unaoeleweka na si wa kuuza sura.