Meneja wa matangazo wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Bw Nicholas Machugu (Kushoto) akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya wa mpira wa miguu kutoka idara ya biashara kwa nahodha wa timu ya idara ya biashara katika tamasha la Vodacom Family day lililofanyika katika viwanja vya kunduchi Beach Hotel lililofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waimbaji wa Skylight Band wakitumbuiza katika tamasha la Vodacom Family Day, tamasha lililo fanyika katika viwanja wa Kunduchi Beach Hotel mwishoni mwa wiki.
wafanyakazi wa mtandao wa simu ya mkononi Vodacom Tanzania kitengo cha
Customer care wakitoa msaada wa vitu mbali mbali kama vyakula, vitanda,
magodoro vyenye thamani ya Sh6 million.
Marehemu John Maganga mwigizaji wa filamu enzi za uhai wake.
KATIKA Tasnia ya filamu Swahiliwood wiki hii imekubwa na simanzi
baada ya wasanii wake kuaga Dunia siku ya jana msanii mahiri wa maigizo
Halid Mohamed ‘Mlopelo’ alizikwa na leo hii tasnia hiyo imekubwa na
msiba mwingine mkubwa baada ya John Maganga kufariki katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Marehemu John Maganga akiwa na msanii mwenzake katika moja ya sene.
Marehemu John Maganga enzi za uhai wake.
Taarifa za awali zinasema kuwa marehemu John amefikwa na mauti baada
ya kusumbuliwa na ugonjwa wa tumbo, ni huzuni kwa wasanii na wadau wa
tasnia hiyo ya filamu kwani wengi wamedai kuwa msanii huyo ni jana tu
walikuwa naye katika matembezi na leo hatunaye tena.
Taarifa zaidi kuhusu mazishi mtazipata hapa hapa bado timu ya FC
inajaribu kufuatilia kwa karibu na kuwataarifu, Bwana Mungu alitoa na
ametwaha jina lake lihimidiwe.
""zimebaki sikuchache kuingia sokoni noma..."" ni kauli ya msanii wa filamu Daudi Michael katika wall yake ya facebook akiongelea ujio wa fila mu yake mpya ijulikanayo kama Magic Money iliyoandaliwa na D Production na wasambazaji ni Pili Pili entertainment.... JIPATIE NAKALA YAKO COMING SOOOOON!!!!! BIGUP D PROD....
Hao
ni washiriki mashindano ya kumtafuta Miss na Mr Tsj kwa mwaka 2012/2013
yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mbalamwezi Beach na hapo
wakiwa wanaingia katika steji.
Wakiwa
katika katika steji wakiwa burudisha wanafunzi wenzao kutoka chuo cha
uandishi habari kiitwacho Tsj kilichopo Ilala-Sharifu shamba pamoja na
Mkuu wao wa chuo cha TSJ akiwa bega kwabega akiongozana na mgeni Rasmi
kutoka kitengo cha Haki za kibinaadamu{LHRC}
Washiriki wa MISS na MR TSJ wakiwa katika picha ya pamoja hapo
Picha
ya pamoja wakiwepo washindi wa MISS na MR TSJ kwa mwaka huu, wakiwa
pamoja na mkuu wa chuo upande wa kulia aliyevaa nguo ya rangi nyeupe Bi
Carolyne Setumbi kushoto Rais wa serikali ya wanafunzi ya TISJOSO Bi
Frida Matinya.
Picha
ya pamoja wakiwepo washindi wa MISS na MR TSJ kwa mwaka huu, wakiwa
pamoja na mkuu wa chuo upande wa kulia aliyevaa nguo ya rangi nyeupe
Bi Carolyne Setumbi kushoto Rais wa serikali ya wanafunzi ya TISJOSO Bi
Frida Matinya.pamoja na Miss na Mr ambao wamewavalisha Taji washindi wa
mwaka huu.
Pichani
Juu na Chini ni Umati wa Watanzania uliofurika kwenye Tamasha la Dini
lililopewa jina la LOVE TANZANIA linaloendelea katika viwanja vya
Jangwani jijini Dar es Salaam likiongozwa na Askofu Andrew Palau kutoka
Marekani.
Vijana walioongoza na Askofu Andrew Palau wakitoa burudani na mafundisho ya dini kwa njia muziki.
SERIKALIya wanafunzi ya chuo cha uandishi wa habari
cha Time School of Journalism (TSJ) inatarajia kuwapata wawakilishi wapya wa
taji la Miss na Mr TSJ katika sherehe za ‘Bash’ambazo zimelenga kuwakaribisha wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza katika
chuo hicho.
Sherehe hizo ambazo zinatarajiwa
kufanyika mwishoni mwa mwezi August tarehe 25 zitafanyika katika uwanja wa
Mwalamwezi Beach, na itasindikizwa na wasanii mabli mbali wa muziki wa Bongo
flava.
Akizungumza na gazeti hili, Rais
wa chuo hicho Bi Frida Matinya alisema kuwa sherehe hizo ni moja ya utaratibu
waliojiwekea katika kuwapokea wanafunzi wapya ambao ni wameingia chuoni hapo
kuchukua kozi mabli mbali.
Alisema kuwa katika sherehe hizo
ambazo zitashereheshwa na michezo mbali mbali ikiwa ni pamoja na maonyesho ya
mavazi, Mr na Miss TSJ, Kuimba, kuvuta kamba, kuogelea na michezo mingine mingi
ya baharini.
“Lengo la sherehe hizo ni kuwa
kawaweka karibu wanafunzi wageni na pia kufahamiana pamoja na kujenga mazingira
rafiki kwa wanafunzi wote pia kuwapa burudani pia kujijenga kisaikolojia kwani
michezo hujenga, kujumuika pamoja katika hafla hii itatuwezesha kuwa na
ushirikiano wa kutosha,” alisema.
SHIRIKISHO la Filamu nchini(TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa filamu na kazi za wasanii
‘wameapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi
ya wasanii.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam
jana, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi
za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni
kero kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia
aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa
kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku
wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.
“Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka
mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa
masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi
zao” “Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri,
tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa
sanaa hii kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu
wachache ndiyo wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba.
Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza
kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato
linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii. Alisema
Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa
wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini
walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.
Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema
Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari
Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubaliana kuweka
mikakati ya kupamba na suala hilo.
Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana
pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwenda kwa haki ili
wasanii na kazi zao
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili msanii wa
filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye anakabiliwa
na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba umepinga maombi
yaliyowasilishwa Mahakama Kuu kuhusu umri wa mshtakiwa huyo na kuiomba
mahakama hiyo iyatupilie mbali.
Pingamizi hilo la awali
liliwasilishwa mahakamani hapo jana na mawakili wa upande wa mashtaka
Elizabeth Kaganda na Shadrack Kimaro mbele ya Jaji Dk Fauz Twaib wakati
wa kusikilizwa maombi hayo. Akiwasilisha pingamizi hilo, wakili Kimaro alidai kuwa maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo kinyume cha sheria.
Alidai
kuwa hata vifungu vya sheria namba 120 (ii) na 113 (i) na (ii) vya
sheria ya mtoto ya mwaka 2009 ambavyo upande wa utetezi umevitumia
kuwasilisha maombi hayo haviipi mamlaka mahakama hiyo kuweza kusikiliza
maombi hayo.
“Namna walivyowasilisha maombi yao na sababu
walizozitaja hazitoshi kuiruhusu mahakama hii kusikiliza maombi
yao,”alidai Kimaro na kuongeza kuwa:
“Ni kweli kwamba mahakama
hii ina uwezo wa kusikiliza suala la umri, lakini namna upande wa
utetezi walivyowasilisha maombi yao hakuiwezeshi mahakama hii
kuyasikiliza,”alidai.
Kimaro alidai kuwa mojawapo ya kielelezo
kilichowasilishwa na upande wa utetezi wakidai ni uamuzi uliotolewa na
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu si uamuzi bali ni amri ya mahakama. Akijibu
hoja hizo, wakili wa utetezi Kenedy Fungamtama ambaye alikuwa
akisadiana na Fulgence Massawe na Peter Kibatala, alidai kuwa maombi
yao ni ya msingi kwani wamefuata taratibu zote za kisheria na kuomba
mahakama iyasikilize.
“Tulichofanya tumefanya kwa kufuata amri
iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kilichoko hapa ni
ubishi kuhusiana na umri wa mshtakiwa,”alidai Fungamtama na kuongeza
kuwa:
“Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haikutoa uamuzi bali
ilitoa amri kwa mawakili wa mshtakiwa kama wana maombi yoyote wafanye
hivyo kupitia mahakama kuu na ndivyo tulivyofanya,”alidai.
Wakili
huyo wa utetezi aliendelea kudai kuwa, hata katika sheria ya mtoto ya
mwaka 2009 imetafsiri neno mahakama ikimaanisha kuwa ni ile ya mwanzo,
wilaya, mkoa ama mahakama kuu hivyo ni sahihi maombi yao kuwapo
mahakamani hapo.
“Upande wa mashtaka wameshindwa kuisaidia
mahakama hii ni taratibu zipi ambazo hatukuzifuata katika kuwasilisha
maombi haya hivyo pingamizi lao litupiliwe mbali,”alidai Fungamtama.
Upande
wa utetezi pia ulinukuu kesi mbalimbali zikiwamo rufaa ya madai namba
86/2009 kati ya Samson Mwalida na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) na kati ya Farida na Kampuni ya Scania Tanzania Ltd.
Jaji
Twaibu baada ya kusikiliza hoja zote, aliwauliza maswali.Jaji: Je
mnadhani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haikuwa na mamlaka ya
kusikiliza maombi haya?
Jaji: Nikiangalia kumbukumbu katika
jalada hili wakili Kaganda (upande wa mashtaka) alisema Mahakama ya
Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza maombi haya kwasababu kesi iliyoko
mbele yake ni ya mauaji ambayo husikilizwa na mahakama kuu.
Kaganda:
Mtukufu Jaji mimi nilisema hivyo nikimaanisha kwamba bado tunaendelea
na upelelezi na kati ya vitu tunavyochunguza ni pamoja na suala la umri
wa mshtakiwa. Baada ya kusikiliza hoja zote Jaji Twaib aliahirisha
kesi hiyo hadi Juni 11 mwaka huu atakapotoa uamuzi kuhusiana na maombi
hayo.
Upande wa utetezi umewasilisha maombi hayo ukiiomba
mahakama kuu iangalie na kuona kama mahakama ya kisutu ina uwezo wa
kuamua suala hilo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya H Baba akiwapa raha ya burudani ya
muziki wake wakazi wa Tarakea Rombo kwenye akiwa kwenye ziara ya
Promosheni mbalimbali za kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo.
H Baba akiwapa zawadi za T shirt watoto kabla nao hawajacheza pamoja nae.
Akihamasisha mashabiki wake kucheza.
Hapa sasa anaonyesha uwezo wake mbele ya mashabiki.
WASANII WA FILAMU TEMEKE KULAMBA DILI KUBWA – GABO
-
MWIGIZAJI mahiri katika tasnia ya filamu Swahilihood Salim Ahmed ‘Gabo
Zigamba’ amefunguka kuwa ni wakati wa wasanii wenye makazi na maisha yao,
kulamba du...
WANAHARAKATI WAJUMUKA.
-
*Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali
Kivulini Hassan Ally akielezea juu ya mradi wa we can ambao unalenga
kuondoa chang...
HARD PRICE COMING SOON
-
* Samahanini sana wadau wangu... Naombeni sana mnisamehe kwa kupotea kwa
kipindi kirefu, na yote haya yanatokana na majukumu ya hapa na pale. Ila
nisinge...
TSJ yaibuka kidedea Mashindano ya Utangazaji 2013
-
*Frank Aman, *Mwananchi
*Dar es Salaam*. Chuo cha uandishi wa habari cha Time School of Journalism
(TSJ) kibeibuka kidedea kwa kupata alama za juu katika...
STAY TUNED... BACK sooon...
-
Its been a year now since my last post on this blog.... nimepata comments
nyingi sana watu wakinisema kuhusiana na ukimya wangu tena wengi
wakinichamba h...
QUEEN SPEAR NI BALAA
-
*Hii ni Poster ya Queen Spear,iliyosheheni mastaa kibao..inatabiliwa kuwa
ni filamu itakayofanya vizuri sana katika soko la filamu Tanzania..Usikose
kunu...
STILLS FROM RED APPLE BEHIND THE SCENES
-
Unajua kuna vitu kama Framing, hasa rule of third na vitu kama hivyo Camera
Boy akiangalia kupitia Camera flipping LCD screen 'BabKubwa!'
Haya Time for...
AILEEN
-
star wa filamu wa kifilipino ambaye ameingarisha filamu ya from china with
love akitumia jina la aileen, fanya mpango uipige jicho halafu rejea hapa
umwage...