KATIKA Tasnia ya filamu Swahiliwood wiki hii imekubwa na simanzi
baada ya wasanii wake kuaga Dunia siku ya jana msanii mahiri wa maigizo
Halid Mohamed ‘Mlopelo’ alizikwa na leo hii tasnia hiyo imekubwa na
msiba mwingine mkubwa baada ya John Maganga kufariki katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Taarifa za awali zinasema kuwa marehemu John amefikwa na mauti baada
ya kusumbuliwa na ugonjwa wa tumbo, ni huzuni kwa wasanii na wadau wa
tasnia hiyo ya filamu kwani wengi wamedai kuwa msanii huyo ni jana tu
walikuwa naye katika matembezi na leo hatunaye tena.
Taarifa zaidi kuhusu mazishi mtazipata hapa hapa bado timu ya FC
inajaribu kufuatilia kwa karibu na kuwataarifu, Bwana Mungu alitoa na
ametwaha jina lake lihimidiwe.