BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Friday, November 26, 2010

FILAMU CENTRAL ONLINE YAANDA BORA ZA 2010 KATIKA TASNIA YA FILAMU.


Mwaka unaisha na mengi yametokea ndani ya Swahiliwood. Na sasa Filamucentral.co.tz inawapa nafasi wadau na wapenzi wa Tasnia hii nafasi ya kuwapongeza wasanii ambao wameweza kufanya kazi kubwa katika kulijaza soko la filamu. NI shughuli nzito wameifanya na sasa ni muda wa kuwapa heshima zao. Kuanzia Tarehe 1/12/2010 mpaka 24/12/2010. Tutawapa nafasi nyie wadau kupiga kura kwa wale wasanii na kazi za filamu ambazo zimeonyesha utofauti katika mwaka huu.


Wapiga kura pia mtapata nafasi ya kujishindia filamu kibao za kibongo ambazo tutakuwa tukizitoa kila siku kwa kipindi chote hiki cha kupiga kura. Soon Tutatangaza makundi ambayo tumeyaweka na pia ni wakina nani ambao wapo humo ndani.
Ili kukusadia kuweza kumpa yule anayestahili kura yako, Mwezi huu wa kumi na mbili tutakuwa tukiwaletea Biographies za wasani na pia list za filamu zote zilizotoka mwaka huu. Pia tutaandika kuhusu matukio yote makubwa ambayo yamachangia tasnia kufika hapa hivi leo. Pia tutawaletea mahojiano ya video kwa wasanii kila siku ya mwezi huu wa kumi na mbili.
BORE ZA 2010, zinakuja kaa tayari

Thursday, November 25, 2010

FILAMU YA OFF SIDE YAWAKUTANISHA MASWAHIBA WAWILI RAY THE GREATEST NA KANUMBA THE GREAT; JE NANI MKALI??



KATIKA tasnia ya filamu hapa nchini majina ya Kanumba na Ray yamekuwa ni majina yaliyozoeleka katika ulingo huu mahili ambao kwa hivi sasa unachukua sura mpya kwa kuweza kushika sana kupitia kazi zao wasanii hawa pia wasanii wengine mbali mbali wanaojihusisha na tasnia hii.

Kitu ambacho watu wengi hujiuliza kwa sasa ni yupi msanii mkali kuzidi mwenzake baina ya wasanii hawa wawili yaani Kanumba pamoja na Ray kigosi kwani wasanii hawa wamekuwa wakifanya vizuri katika fani hii na pia ni maswahiba ambao walianza kazi katika kitovu cha sanaa cha Kaole sanaa group kwa pamoja hivyo ni watu waliopitia njia nyingi hadi kufika hapo walipo ambapo kila mmoja anamiliki kampuni yake binafsi. Kanumba anamiliki kampuni yake inayojulikana kama Kanumba the great film pia Ray nae ana miliki kampuni yake walioshirikiana na johari inayojulikana kama RJ company.

Majibu ya maswali hayo ya wadau wa tasnia hii juu ya ukweli kuwa nani ni mkali yanajibika katika filamu inayotarajiwa kutoka hivi karibuni ambayo ndani yake vichwa hivyo viwili vimeshiriki. Filamu ya OFF SIDE ni moja ya filamu ambayo imeandaliwa chini ya kampuni ya Kanumba na ina vichwa vingine vikali kama Johari, na JB ambao pia ni waasisi wa filamu hapa TZ na wameshafanya kazi kibao kwa pamoja lakini hii ni kali kwa imewakutanisha maswahiba hawa wawili pamoja na mastaa wengine.

Sijui kwa upande wako ni nani mkali? Ila kwangu nasubili nione filamu hiyo ndipo nitoe maoni yangu ila kwa sasa nawakubali wote kwa kazi kali wanazozifanya.

MPIGIE KURA PETER MSECHU PATA HABARI HII KUPITIA www.thazealottz.blogspot.com

WATANZANIA TUSHIRIKI KUMPIGIA KURA PETER MSECHU ABAKI KATIKA TUSKER PROJECT FAME SEASON 4


 Peter Msechu
HII ni season ya nne tangu shindano la kusaka vipaji vya uimbaji la TUSKER PROJECT FAME lianzishwe na kampuni ya bia ya EAST AFRICA BREWELIES LIMITED kupitia kinywaji chake cha Tusker, tumeweza kuona baadhi ya watanzania wakijitahidi kushiriki katika ushindani huo kwa hali na mali ili kuweza kufanikisha kuchukua ushindi huo lakini kwa bahati mbaya nchi yetu haijawahi kupata ushindi kutoka kwa hao wawakilishi wetu walioenda kushiriki katika TUSKER PROJECT FAME.

Kuna wawakilishi tofauti tofauti walioshiriki kuweza kuiwakilisha TZ mmoja wapo ni hemed, Alex, na wengine wengi.Lakini katika season hii ya nne tuliwakilishwa na Aneth pamoja na Leah Mou, Cynthia na Peter msechu na waliobahatika kufika nafasi nzuri katika shindano hili ni Leah,Aneth ambao walitoka hivi karibuni kwa kukosa kura za kutosheleza. Mpaka hivi sasa Tanzania bado inawakilishwa na Mwana kaka PETER MSECHU ambaye kwa wiki iliyopita aliingia katika probation  na kwa sasa anaelekea kutoka endapo waTanzania hatutashirikiana kumpigia kura ili aendelee kuwepo.
 Leah 
Aneth
Ni ombi langu kuwa ili muwakirishi wetu aendelee kubaki katika mashindano ni vyema tumpie kura ili azidi kuwepo na kufanya vizuri na mwisho wa siku arudi na ushindi nyumbani ili kufuta historia iliyopo katika mashindano hayo kwa TZ.
Jinsi ya kumpigia kura PETER MSECHU aendelee kuiwakilisha TANZANIA andika neno TUSKER 9 tuma kwenda 15522 kupitia kura yako utakuwa umeweza kumpa nafasi  PETER MSECHU kubaki katika TPF 4 na kuzidi kufanya vizuri na kurudi na ushindi.
WATANZANIA TUSHIRIKI KUPIGA KURA NA PIA TUOMBE MUNGU MUWAKIRISHI WA TANZANIA PETER MSECHU AFANYE VIZURI….

Tuesday, November 23, 2010

FILAMU MPYA YA DON'T CRY KUTOKA KWA BABA HAJI

       
MUIGIZAJI mahiri na nyota wa filamu hapa nchini Haji Adam almaarufu kama Baba Haji amerudi kwa kishindo na filamu yake ya Don’t Cry, Baba Haji ambaye kwa sasa yupo chuo cha Sanaa Bagamoyo akiongeza ujuzi zaidi, kwa muda kidogo msanii huyu alikuwa ametoweka kwa kutoonekana katika filamu akishiriki kwa sehemu kubwa ya filamu zaidi kushiriki scene chache tu.
       Safari hii katika filamu hii ameshirika kama Steringi na pia akiongoza filamu hii filamu ya Don’t Cry inasambazwa na kampuni ya Al Riyamy Production Limited ya jijini Dar es Salaam..
       Don’t Cry imetoka hivi karibuni na kusambazwa nchi nzima katika filamu hii unakutana na wasanii wakali wa filamu walioshiriki katika filamu hii ni kama mwanadada ambaye kwa sasa ni tishio kwa wasanii wa kike mwenye mvuto wa kufa mtu, muigizaji mahiri Rose Ndauka, Diana Nsumba na wengine wengi.

Friday, November 19, 2010

TV SIBUKA ON AIR NOW KUPITIA STARTIME DIGITAL SATELITE..


Kuanzia majira ya mchana leo tarehe 19 november 2010, kupitia katika king'amuzi cha startime kituo cha Television cha SIBUKA TV kilianza kurusha matangazo yake ya awali(TEST SIGNAL) Kwa Dar es salaam pekee.
Kwa wadau na wapenzi wa filamu na documentary kibao waweza kupata burudani kupitia TV yako ya Sibuka kwenye king'amuzi cha startime.

Thursday, November 18, 2010

FILAMU YA DNA KUITWA HIDDEN TRUTH.


FILAMU ya DNA iliyoripotiwa kutoka hivi karibuni kutoka kampuni ya SAM Enterprises ya jijini Dar es Salaam imebadilishwa jina na haitaitwa DNA tena bali kwa sasa itaitwa Hidden Truth, badiliko hilo limefuatiwa na ombi lilotoka kwa mtayarishaji mwingine William Mtitu kumuomba mtayarishaji wa filamu hii Seleman Mkangara.

“Filamu hii niliita DNA kulingana na kisa cha filamu yenyewe, sasa akatokea jamaa akidai na yeye ana filamu ambayo ipo tayari kutoka na ina jina kama la filamu yangu DNA kwa hiyo akaniomba nibadili jina hili na kuita jina lingine, sikuwa na jinsi maana hawa wenzetu wanategemea kuuza kwa majina sasa uking’ang’ani filamu yake ikifanya vibaya wewe ndio utaonekana tatizo, kwa filamu hii sasa itaitwa Hidden Truth”
Alisema Mkangara.
Filamu hiyo ambayo imeigizwa kwa ustadi na mwanadada nyota na mshindi wa tuzo za Risasi mwaka 2005/ 2006 Riyama Ally imetabiriwa kuwa ni moto wa kuotea mbali, hata mtayarishaji wa filamu hii alisema kuwa kwa sababu ya uzuri wa filamu hii ndio maana hata alivyoambiwa na mtayarishaji mwenzake abadili jina alifanya hivyo haraka kwani anaamini kuwa haitaharibu chochote.
Binafsi nilikuwa sielewi kama majina nayo yanakuwa issue kubwa hivyo, suala la kugongana majina ya filamu wakati visa tofauti inawezekana isiwe tatizo, labda itokee kuwa hata visa vilingane, ukija kwa upande mwingine lazima vyombo husika vilivyopo vijitahidi kuwa na kalenda ya kuwaongoza watayarishaji ikiwa na utaratibu wa kuzipitia script kabla ya kwenda kurekodi.
Tukio hili si kwanza kutokea lilishawahi kutokea kati ya mtayarishaji Mohamed Nurdin na Gumbo Kihorota, ambapo Gumbo alitoa filamu iliyoitwa Machozi na Mohamed Nurdin naye baadae akatoa filamu iliyoitwa Machozi vile vile, sikufuatilia huko mbele sina kumbukumbu kama kuna mmoja wao aliathirika na hilo.
Watayarishaji mjitahidi kubuni majina ya Kiswahili inawezeka kabisa utata wa kugombea majina ukapotea kwani Lugha yetu ina uwanda mpana na wenye maana tofauti, tofauti na Lugha tunayoikimbilia.

Tuesday, November 16, 2010

Binti Nusa sehemu ya pili imekamilika


Binti Nusa sehemu ya pili imekamilika na ipo tayari kwa ajili ya kuingia sokoni kwa ajili ya mauzo, filamu inakuja baada ya Binti Nusa nambari moja kufanya vizuri katika tasnia hii na kuwashika watazamaji ambao walikuwa na kiu ya kujua binti huyu anayesadikiwa kuwa ni muuaji na anatafutwa na polisi atapatwa na nini?

Katika sehemu ya kwanza katika filamu hii ya Binti Nusa ‘Monalisa’ kacheza kama binti kutoka kijijini kuja kwa mjomba wake na kukutana na mauaji ya familia yake yote na yeye kunusurika na kukimbilia katika nyumba ya kulala wageni. Dereva Taksi anafanya mpango kumuibia fedha zake alizochukua kwa mjomba wake na akiwa hotelini anampata Bosi anayempenda na bosi huyu anataka awe mpenzi wake, na huyu ni afisa wa polisi. Shughuli ipo hapo!!!!

Akiongea na Fc mtayarishaji wa filamu hii Yvonne Cherryl aka Monalisa amesema kuwa
“Filamu hii imekamilika kuanzia uhariri na kila kitu kimeenda sawa, na nilikuwa na kazi ngumu sana kwani sikutaka nipoteze ladha ya Binti Nusa ya kwanza, katika kulinda ubora wa filamu ya kwanza imenibidi kwa kila hatua ninayofikia niwe makini kwa ajili ya kusonga mbele na kutoa kitu bora zaidi”
Aidha filamu hiyo ambayo inasemekana baada ya kuhaririwa ilipekwa Nchini Kenya na kuangaliwa na watalamu wa mambo ya filamu nchini humo na tayari wamefanya kazi yao na baada ya kuikubali imeletwa kwa ajili kuisambaza hapa nchini.
Filamu hii imeshirikisha wasanii nyota wa filamu hapa nchini kama Hashimu Kambi, Susan Lewis, Vanita Omary, Yvonne Cherryl, pamoja na Keneth Ambari aka Baraza.

FILAMU YA BEAUTIFULLY KUTOKA TUESDAY ENTERTAINMENT.


KAMPUNI ya Tuesday Entertainment inakuja na filamu inayokwenda kwa jina la Beautifully filamu hii imeshirikisha wasanii wakali kama Charles Magali (Mzee Magali) na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Bongo fleva Rehema Chalamila (Ray C).

“Ray C mzigo aliopiga katika filamu hii ni simulizi hata mimi sikujua kama mwanadada huyu anauwezo mkubwa namna hii katika uigizaji, ameigiza katika kiwango cha juu sana, na inawezekana akawa tishio zaidi kwa waigizaji wa kike”
Alisema mkurugenzi wa kampuni hiyo Mr. Chuzi.

Filamu imechezwa na Suddy, Asnat, Tony na Mr. Chuzi mwenyewe imerekodiwa Matombo Mkoani Morogoro, filamu hii inayosubiriwa kwa hamu na watazamaji inatarajiwa kutoka mwezi ujao na kusambazwa na kampuni ya Steps Entertanment.