BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Tuesday, April 10, 2012

KANUMBA KUZIKWA BILA KUAGWA NA MASHABIKI WAKE...!!!

Kwa habari zilizo tufikia na aliyepo eneo la tukio (Viwanja vya Leaders) ambako mwili wa marehemu Steven Kanumba uliwasili majira ya saa tatu kwa ajili ya misa na kuagwa.
Zoezi la kuaga limeshindikana kwa upande wa umati mkubwa wa wananchi waliohudhuria hapo baada ya viongozi pekee kupata fursa ya kuaga na kufuatiwa fujo na polisi kushindwa kudhibiti kulingana na idadi kubwa ya waombolezaji.
Hivyo mwili wa msanii huyo maarufu wa filamu unaelekea kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku gari iliyobeba mwili wake ikisukumwa na wananchi  waliojipanga barabarani kuelekea makaburini.
Huu ni umati wa watu unao elekea makaburini
Gari lililo beba mwili wa marehemu Steven Kanumba likielekea makaburini
Imeshindikana kabisa kwa jeneza kuingizwa makaburini Kinondoni.Kamati iko busy kuangalia nini cha kufanya

No comments:

Post a Comment