BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Monday, May 28, 2012

Serikali yataka maombi ya uchunguzi wa umri wa Lulu yatupwe


UPANDE wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba umepinga maombi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu kuhusu umri wa mshtakiwa huyo na kuiomba mahakama hiyo iyatupilie mbali.

Pingamizi hilo la awali liliwasilishwa mahakamani hapo jana na mawakili wa upande wa mashtaka Elizabeth Kaganda na Shadrack Kimaro mbele ya Jaji Dk Fauz Twaib wakati wa kusikilizwa maombi hayo.
Akiwasilisha pingamizi hilo, wakili Kimaro alidai kuwa maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo kinyume cha sheria.

Alidai kuwa hata vifungu vya sheria namba 120 (ii) na 113 (i) na (ii) vya sheria ya mtoto ya mwaka 2009 ambavyo upande wa utetezi umevitumia kuwasilisha maombi hayo haviipi mamlaka mahakama hiyo kuweza kusikiliza maombi hayo.

“Namna walivyowasilisha maombi yao na sababu walizozitaja hazitoshi kuiruhusu mahakama hii kusikiliza maombi yao,”alidai Kimaro na kuongeza kuwa:

“Ni kweli kwamba mahakama hii ina uwezo wa kusikiliza suala la umri, lakini namna upande wa utetezi walivyowasilisha maombi yao hakuiwezeshi mahakama hii kuyasikiliza,”alidai.

Kimaro alidai kuwa mojawapo ya kielelezo kilichowasilishwa na upande wa utetezi wakidai ni uamuzi uliotolewa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu si uamuzi bali ni amri ya mahakama.
Akijibu hoja hizo, wakili wa utetezi Kenedy Fungamtama ambaye alikuwa akisadiana na Fulgence Massawe na Peter Kibatala, alidai kuwa maombi yao ni ya msingi kwani wamefuata taratibu zote za kisheria na kuomba mahakama iyasikilize.

“Tulichofanya tumefanya kwa kufuata amri iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kilichoko hapa ni ubishi kuhusiana na umri wa mshtakiwa,”alidai Fungamtama na kuongeza kuwa:

“Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haikutoa uamuzi bali ilitoa amri kwa mawakili wa mshtakiwa kama wana maombi yoyote wafanye hivyo kupitia mahakama kuu na ndivyo tulivyofanya,”alidai.

Wakili huyo wa utetezi aliendelea kudai kuwa, hata katika sheria ya mtoto ya mwaka 2009 imetafsiri neno mahakama ikimaanisha kuwa ni ile ya mwanzo, wilaya, mkoa ama mahakama kuu hivyo ni sahihi maombi yao kuwapo mahakamani hapo.

“Upande wa mashtaka wameshindwa kuisaidia mahakama hii ni taratibu zipi ambazo hatukuzifuata katika kuwasilisha maombi haya hivyo pingamizi lao litupiliwe mbali,”alidai Fungamtama.

Upande wa utetezi pia ulinukuu kesi mbalimbali zikiwamo rufaa ya madai namba 86/2009 kati ya Samson Mwalida na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na  kati ya Farida na Kampuni ya Scania Tanzania Ltd.

Jaji Twaibu baada ya kusikiliza hoja zote, aliwauliza maswali.Jaji: Je mnadhani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haikuwa na mamlaka ya kusikiliza maombi haya?
Jaji: Nikiangalia kumbukumbu katika jalada hili wakili Kaganda (upande wa mashtaka) alisema Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza maombi haya kwasababu kesi iliyoko mbele yake ni ya mauaji ambayo husikilizwa na mahakama kuu.

Kaganda: Mtukufu Jaji mimi nilisema hivyo nikimaanisha kwamba bado tunaendelea na upelelezi na kati ya vitu tunavyochunguza ni pamoja na suala la umri wa mshtakiwa.
Baada ya kusikiliza hoja zote Jaji Twaib aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 11 mwaka huu atakapotoa uamuzi kuhusiana na maombi hayo.

Upande wa utetezi umewasilisha maombi hayo ukiiomba mahakama kuu iangalie na kuona kama mahakama ya kisutu ina uwezo wa kuamua suala hilo.

Sunday, May 27, 2012

UPEPO WA RECHO NA SHILOLE NDANI YA MAISHA CLUB


MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA H BABA AENDELEZA MASHAMBULIZI KANDA YA KASKAZINI.


 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya H Baba akiwapa raha ya burudani ya muziki wake wakazi wa Tarakea Rombo kwenye akiwa kwenye ziara ya Promosheni mbalimbali za kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo.
 H Baba akiwapa zawadi za T shirt watoto kabla nao hawajacheza pamoja nae.
 Akihamasisha mashabiki wake kucheza.
Hapa sasa anaonyesha uwezo wake mbele ya mashabiki.

MASHINDANO YA JUDO YAANZA JIJINI DAR, ZANZIBAR KAMA KAWAIDA YAZIDI KUITESA BARA.


 Baadhi ya Viongozi wa Mchezo wa Judo wakifuatlia kwa makini namna wachezaji wanavyo pambana.
 Mchzaji wa Judo kutoka Zanzibar Ahmad Shah (juu) akimkandamiza mchezaji wa magereza Athumani Ally wakati wa michuano hiyo ilionza leo kwenye Hoteli ya Land Marck jijini Dar es Salaam.

 Hawa ni Mohamed Kolagonde wa na Nickolaus Faustine (kulia) wakionyeshana Ubabe kwenye mchezo wa judo.
Waamuzi nao walikua na vifaa maalum vya kukusanya points.

MSAFARA WA SIMBA KWENDA DAR LIVE..

Msafara wa wachezaji, wadau wa mpira na mashabiki wa club ya Simba kuelekea mbagala leo... shughuli hiyo imesababisha kuwepo na msongamano mkubwa wa gari amahali ambapo wamepita kama ratiba yao ilivyokuwa....

Friday, May 25, 2012

STEVE NYERERE KUSOMESHA WATOTO YATIMA WAWILI KWA MIAKA SABA

MSANII wa filamu nchini ambaye pia huiga sauti za viongozi mbalimbali, Steve Mengele 'Steve Nyerere' jana amezindua filam yake  mpya inayojulikana kama 'Mwalim Nyerere'.

Filam hiyo ameizindua kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua Ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filam hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 3 ikiwa ni pamoja na kujitolea kuwasomesha watoto wawili katika kituo hicho.

Akizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Steve Nyerere alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba Baba wa Taifa Mwali Nyerere hakubagua watu.

Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha anamuenzi Baba wa Taifa kwa kutoa filamu itakayokuwa inaonesha mambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya Baba wa Taifa.

"Jina lililonibeba zaidi katika tasnia hii ya filamu ni jina la Steve Nyerere kiasi ambacho hata jina la Baba yangu halijanizoea, hivyo kutokana na ukubwa wa jina hili limenifanya mimi kutambulika na jamii nzima ya Tanzania hivyo ili kulienzi jina hili nimeamua kutoa filamu hii ya Mwalim Nyerere,"alisema Steve.

Alisema msaada alioutoa kwa watoto yatima hautaishia kwao bali ataendelea kutoa kile atakachokipata kupitia filamu hiyo kuwasaidia na wale wasiojiweza.

Alisema filam ya Mwalim Nyerere ameifanyia Butiama alipozaliwa Baba wa Taifa ili kujenga uhalisia wa kile alichodhamiria na kwamba ameitengeneza filamu hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu huku akishirikiana vema na mke wa Hayati Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.

Alisema jumla ya sh. milioni 25 ametumia katika kuikamilisha filam hiyo ambayo itaanza kuingia sokoni leo ikiwa chini ya usambazaji wa Steps Entertaiment.

Kabla ya kutoa filam hiyo Steve Nyerere alitamba na filam ya 'Mr President' aliyoitunga kwa kuvaa uhusika wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete ambayo aliitaja kama zawadi kwa Rais Kikwete katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika


Diamond Kutumbuiza Big Brother this Sunday


Msanii Diamond(jina kamili Naseeb Abdul), wikiendi hii anatarajiwa kuwa nje ya mipaka ya Tanzania wakati atakapopanda jukwaa kuburudisha wakati wa Live Eviction Show ya Big Brother Africa(BBA) huko Johanesburg, South Africa siku ya Jumapili saa mbili usiku kwa saa za Afrika ya Kati.
Diamond ambaye mapema mwaka huu aliongoza kwa kutwaa Tuzo za Kilimanjaro nchini Tanzania, ametangazwa hivi karibuni kuwemo katika orodha ya wasanii wanaowania tuzo za MTV African Music Awards(MAMA). Way to go Diamond!

Thursday, May 17, 2012

GARI ALILOPATANALO AJALI PATRICK MAFISANGO

 PIR MAFISANGO
 GARI LAKE MAREHEMU LIKIWA LIMEHARIBIKA VIBAYA

 ENEO ALILOPATIA AJALI MAFISANGO

Tuesday, May 8, 2012

BANANA ARTS GROUP-KEMONDO WAZINDUA FILAMU MPYA IJULIKANAYO KWA JINA LA SIRI YA MAMA

JENNIFER KYAKA "ODAMA" AMEACHIA FILAMU YAKE MPYA-"RUDE"

 
Filamu yangu inayoitwa RUDE niliyoicheza na Stanley Msungu,Ruth Suka a.k.a Mainda, Mzee Jengua, Herrieth Chumila,Rachel Haule na wasanii wengineo kibao.

Ni story nzuri sana ( Lamata hajawahi kuniangusha kwenye hilo) inayoonyesha mambo halisi yanayotokea katika jamii yetu.

Utajiuliza utofauti wake ni nini? ni ubora wa picha( shukrani kwa Farid Uwezo) mpangilio mzuri wa story, soundtracks zilizopangiliwa vizuri, ubora wa sauti na kikubwa zaidi FINE ACTING.

Muone jinsi Msungu alivyodhihirisha u- mwamba wake wa kuweza kucheza roles tofauti tofauti (picha ya cover inajieleza)
Utaona jinsi MAINDA alivyokuwa Good girl gone bad( get ur copy umuone msichana huyo mdogo lakini mkongwe kwenye movie za bongo)

Utaniona mimi pia ( makamuzi yangu si unayafahamu?)

JIPATIE COPY YAKO SASA

Tembelea blogu yake: www.odama1.blogspot.com

Red Cross yafanya maandamano na kuadhimisha siku ya Red Cross Duniani yenye lengo la kutoa elimu ya matumizi sahihi ya nembo yake.

Baadhi ya wanachama na volunteers wa red Cross wakifanya maandamano jijini Dar leo.
Baadhi ya wanachama na volunteers wa red Cross wakifanya maandamano jijini Dar leo.
Baadhi ya wanachama na volunteers wa red Cross wakifanya maandamano jijini Dar leo.
Baadhi ya wanachama na volunteers wa red Cross wakifanya maandamano jijini Dar leo.
Volunteers wakicheza nyimbo mbali mbali zinazoelezea matumizi sahihi ya nembo.
Wanafunzi wenye ulemavu wa viungo mbali mbali kutoka shule ya Uhuru Mchanganyiko wakiimba nyimbo katika sherehe za siku ya Red Cross Duniani.
 Volunteers wakionyesha matumizi sahihi ya nembo na baadhi ya nembo za chama hicho zinazotumiwa na nchi tofauti tofauti duniani
Baadhi ya wanafunzi wa first aid wakionyehs jinsi Red Cross inavyotoa huduma ya kwanza kwa waliopatwa na ajali.
Baadhi ya wanafunzi wa first aid wakionyehs jinsi Red Cross inavyotoa huduma ya kwanza kwa waliopatwa na ajali.
Mwenyekiti wa Red Cross taifa Dr Zainab Gama akihutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya Red Cross Day.