MZEE
Charles Kanumba ambaye ni baba mzazi wa marehemu Steven Kanumba,
amezuia kuuzwa kwa mali zilizoachwa na mkali huyo wa filamu nchini.
Mzee Kanumba anataka kitu chochote kisiuzwe mpaka mahakama itakapoamua mrithi wa mali hizo. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa, mzazi huyo alisema kuwa ameamua kutoa tamko hilo baada ya kusikia mzazi mwenzake, Flora Mutegoa, ameanza kuuza mali zilizoachwa na marehemu Kanumba kabla ya mahakama kutoa uamuzi. Mali hizo ni pamoja na gari la kifahari lenye thamani ya Sh 75 milioni. �Nimesikitishwa na kitendo cha kusikia mama wa Kanumba ameanza kuuza mali za marehemu, nimeamua kutoa tamko kwa Watanzania wote kuwa wasinunue mali yoyote ya marehemu mpaka mahakama itakapotoa uamuzi," Mzee Kanumba alisema. "Sisi wazazi wote tuna haki kwa sababu ndiyo tuliomzaa, mtu yeyote atakayenunua mali hiyo atakuwa ametenda kosa la jinai." Pia alisema ametoa kauli hiyo kufuatia kupata taarifa kuwa kuna wasanii ndiyo madalali wa kuuza mali hizo za Kanumba. Mzee huyo pia ametoa wito kwa mzazi mwenzake kuacha kusikiliza watu wanaopotosha kuwa kifo cha mtoto wao kilitokana na imani za ushirikina. �Kuna kijana mmoja ambaye ni mtoto wa dada yangu (anamtaja jina) nimesikia anamdanganya kuwa mtoto wetu karogwa, mara amechukuliwa msukule asimsikilize huyo," aliongeza Mzee Kanumba. "Tuliwahi kumwita ili kumhoji lakini hakutokea." Kanumba alfariki dunia Aprili 7 mwaka huu katika kifo kilichozua utata. Msanii Lulu yuko rumande akiendelea na kesi inayomtuhumu kuhusika na kifo hicho. |
WASANII WA FILAMU TEMEKE KULAMBA DILI KUBWA – GABO
-
MWIGIZAJI mahiri katika tasnia ya filamu Swahilihood Salim Ahmed ‘Gabo
Zigamba’ amefunguka kuwa ni wakati wa wasanii wenye makazi na maisha yao,
kulamba du...
5 years ago
No comments:
Post a Comment