Frank Aman, Mwananchi
Dar es Salaam. Chuo cha uandishi
wa habari cha Time School of Journalism (TSJ) kibeibuka kidedea kwa kupata
alama za juu katika vipingele vyote katika mashindano ya utangazaji yaliyohusisha
vyuo vya uandishi wa habari yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
Vipengele ambavyo vilikipatia ushindi chuo hicho ikiwa ni mara ya pili
kupata ushindi huo tangu mashindano hayo yaanzishwe mwaka 2011 vilikuwa ni
pamoja na uchambuzi wa magazeti, Kusoma taarifa ya habari, kuendesha vipindi
maalum, Michezo pamoja na vipindi vya burudani.
Akizungumza mara ya baada ya kutangazwa washindi, Rais wa chuo hicho Bi
Frida Matinya alisema kuwa licha ya maandalizi ya muda mfupi kutokana na sababu
zilizokuwa nje ya uwezo wao ushindi huo umepatikana kutokana na mafunzo waliyoyapata
chuoni hapo pamoja na vipaji vya wanafunzi walioshiriki katika mashidano hayo.
Alisema kuwa asilimia kubwa ya washiriki katika shidano hilo walio wakilisha
chuo hicho wengi wao walikuwa ni wanafunzi walioingia muhula wa kwanza mwaka
huu hivyo hali hiyo imedhihilisha vipaji na uwezo wa wanafunzi binafsi.
“Toka kuanza kwa shindano hili mara zote tumeibika kidedea kwani mwaka
2011 lilipoanza shindano hili ambalo lilifanyika katika chuo cha uandishi wa
habari cha Royal College of Tanzania (RCT) tulikuwa washindi wa kwanza, mwaka
jana yalifanyika chuo cha uandishi wa habari cha Mlimani eneo la Mbezi tulikuwa
washindi wa pili,” alisema na kuongeza;
“Hii pekee imedhihilisha kuwa kuwa wanafunzi wa chuo hiki wana uwezo
mkubwa katika fani ya utangazaji na pia taaluma inayotolewa katika chuo chetu
inakidhi vigezo vya sisi kuingia katika ushindani wa aina yoyote hata katika
ngazi ya ajira.”
Bi Matinya alisema kuwa katika shindano hilo chuo cha RCT kimekuchukua
nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikishikwa na chuo cha Dar es Salaam City
College (DACISO).
Mashindano hayo yalifanyika katika viwanja vya TSJ maeneo ya Ilala
Sharifu Shamba yalijumisha idadi ya vyuo sita (6) lakini vyuo ambavyo
vilishiriki jana katika kinyang’anyiro hicho ni vitatu ambavyo ni RCT, DACICO
pamoja na TSJ.
Wakiongee na Mwananchi baadhi
ya wanafunzi wa Tsj walisema “ sisi ndio sisi ushindi kwetu daima kwani
tulijiandaa vya kutosha japokuwa muda tuliyofanya mazoezi ni mdogo mno ila
tumestahiki kuwa washindi wa nafasi ya kwanza”
MWISHO.
No comments:
Post a Comment