BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Saturday, August 20, 2011

SHAMSA APANIA KUMFIKIA OPRAH..


SHAMSA Ford ni msanii wa filamu nchini anayeingia kwa kasi katika tasnia hiyo huku akiwa na malengo ya kufikia mafanikio ya muongozaji maarufu wa vipindi mbalimbali vya televisheni nchini Marekani, Oprah Winfrey.


Shamsa ambaye jina la baba yake linafanana pia na jina la baba wa muigizaji maarufu nchini Marekani, Harrison Ford, ameanza kucheza filamu mwaka 2010 na kuweza kukubalika na watu wengi hasa waongozaji wa filamu ndani na nje ya nchi.



Anasema anatamani kuwa mwanamke wa heshima sana katika ulimwengu huu na baadaye kuwa muigizaji wa kimataifa kama ilivyo kwa Oprah winfrey muongozaji maarufu wa vipindi mbalimbali vya televisheni nchini Marekani.


“Maishani mwangu natamani vitu viwili tu, kuwa mwanamke wa heshima sana katika ulimwengu na muigizaji wa kimataifa. Tukizungumzia Oprah ni mwanamke anayeheshimika sana anauwezo wakufika hapa nchini na kuingia Ikulu kuzungumza na Rais na mawazo yake yakasikilizwa na kutekelezwa leo hii sisi wasanii wa Tanzania hatujaweza kufikia hatua hiyo natamani kuwa wa kwanza,” anasema.



Shamsa anasema, katika kipindi cha muda mfupi ambacho ameanza kuonekana kwenye filamu, ameona mafanikio na kwamba tayari ameanza kupata tenda za kucheza filamu nje ya nchi.

Sunday, August 14, 2011

TSJ YAANDAA MASHINDANO YA MISS & MR KWA MWAKA HUU....

SERIKALI ya wanafunzi ya Time School of Journalism (TISJOSO) kwa kushirikiana na kampuni ya kizalendo ya Zealot Entertainment Agency imeandaa mashindano ya urembo ya kumtafuta mshindi na mwakilishi ya kinyang’anyiro cha Miss na Mr TSJ 2011.
Shindano hilo litafanyika katika sherehe ya Welcome First Year Special Bash ambayo imelenga kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo kwa ngazi zote kuanzia Basic Certificate, Advanced Certificate na Diploma kwa mwaka huu.
Hafla hiyo ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza ambayo itapendezeshwa na mashindano haya inatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 3 Septemba mwaka huu katika maeneo ya Jangwani Sea Breeze Mbezi beach.

Saturday, August 13, 2011

AFRICA MAGIC YAMPA SHAVU MR CHUZI...


MWIGIZAJI na mwenyekiti wa Watengenezaji wa filamu Tanzania Tuesday Kihangala ‘Mr Chuzi’ amesema ameridhishwa na uuzaji wa kazi zake kama ya Millosis, Jasmini na jumba la dhahabu katika kampuni ya Africa Magic inayotumia kuonyesha michezo mbali mbali duniani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia hivi karibuni tamthiliya ya jumba la dhahabu inatarajiwa kurudiwa kwa mara ya pili na kituo hicho, hivyo hiyo ni nafasi ya kipekee kwa wale wote waliokuwa hawajahawi kuiona ama walikuwa wanavutiwa.

Mr chuzi alionyesha kufurahishwa kwake na mkataba alioingia na kampuni hiyo na hivyo kuahidi kufanya kazi nzuri na zenye ubora zaidi ili kuwapa watazamaji na washabiki wake kile wanachostahili.
Msanii huyu amekuwa mahiri katika kufanya kazi mbali mbali hivyo kuzidi kuijenga tasnia hiyo.


WASANII WA FILAMU WAWALALAMIKIA WASAMBAZAJI...


BAADHI ya wasanii ambao ni wanachama wa shirikisho la filamu nchini TAFF, kutoka mkoa wa Kinondoni, walikutana wiki hii kujadili mqmbo mbali mbali yanayolenga kuimarisha shirikisho hilo.
Miongoni mwa mambo waliyoyatilia mkazo ni kudharauliwa kwa wasanii wachanga na wale wasiokuwa na majina, kusambazwa kwa kazi za wenye majina pekee kukumbatiwa kwa wasanii wachache na kufanyiwa promo kwa video zao, mtandao wa magazeti ambao unaharibu tasnia.

Wasanii walichangia mada kwa kusema, watu ambao walianzisha TAFF na ndio hao hao waliokuja kuivunja na kuanzisha Bongo Movie Club amabo wanasadikiwa hawalitambui shirikisho wala Rais wa shirikisho hilo. Wasanii wengine walitoa kero zao za moja kwa moja kwa kampuni yausambazaji wa filamu Tanzania ya Steps.
Wengine hawakuacha tua shutuma zao kwa wasanii ambao walimeshajijengea jina kwamba wanatumia fedha ili kuuza sura kwenye magazeti.

Monday, August 8, 2011

MSANII NYOTA WA FILAMU NIGERIA AFARIKI DUNIA…


MSANII nyota wa filamu nchini Nigeria Sam Loco Efe, amefariki dunia na kwa taarifa zilizotufikia ni kuwa msanii huyo alifariki dunia akiwa katika chumba cha hotel Imo State.
Inasemekana kuwa Sam Loco alifariki akiwa location siku hiyo na mpaka hivi sasa familia yake bado haijatoa taarifa kamili kuhusiana na taarifa za msiba huo na chanzo cha  kufariki kwake.

Msanii huyo ambaye ana umri wa miaka 66 alianza rasmi kuingia katika tasnia hii ya maigizo kupitia tamthiliya mbali mbali ziliyokuwa zikonyeshwa katika vituo mbali mbali vya televisheni nchini humo kuanzia miaka ya 70.
Kwa kifupi tuu  Sam Loco Efe-ni mzaliwa kutoka  Benin City, Edo State lakini alizaliwa Enugu. Hata vivyo alikulia katika maeneo ya Abakakili. Na alijiingiza rasmi katika fani hii baada ya kutazama kazi iliyofanya na wanafunzi wa chuo cha serikali cha Umuahia.
Na aliajiriwa huko Michelin, Ijora, Lagos lakini kwa muda mfupi aliondoka na kujiunga na Dunlop mwaka 1969. Efe alianza rasmi kufanya kazi hii mwaka 1970.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHARI PEMA PEPONI

JENIFFER MGENDI KUJIKITA ZAID KTK GAME YA FILAMU..


JENNIFER Mgendi ni kati ya waimbaji nyota wa nyimbo za Injili aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Nyota huyo anasema matarajio yake nikuwa muongozaji na muandaaji wa filamu ili kueneza injili kwa njia ya uimbaji na uigiza.
Mgendi ambaye amedumu kwa miaka 16 katika gemu la muziki wa Injili, anasema amefanikiwa kwa kiasi na kwamba kazi zake zinakubalika ndani na nje ya nchi.

Anasema, matarajio yake ni kujikita zaidi katika kutayarisha filamu na kwamba amefanikiwa kucheza filai ya Joto la Roho, Pigo la Faraja na Teke la Mama.
“Mafanikio yangu niyakawaida, namshukuru Mungu kwa kuwa naweza kuendesha familia yangu. Malengo yangu kiakili ni kujikita zaidi katika utayarishaji wa filaimu ili niifikishie jamii ujumbe kwa njia ya nyimbo na maigizo,” alisema Mgendi.

Sunday, August 7, 2011

DOKII APANIA KUFANYA VYEMA AKI-COLLABO NA MYAMBA...


Doki amepania kufanya vizuri sana endapo atapata nafasi yakucheza na Pastor Myamba kwa nafasi kama mama mchungaji...

Amesema ataonyesha kuwa yeye ni mtu sahihi wa nafasi hiyo ya umama mchungaji na wengine wanabahatisha tuuu..hayo yalielezwa na Dokii alipofanya mawasiliano na Myamba ambaye anatarajia kumshirikisha Dokii katika filamu ijayo..

ESTHER; "Tasnia ya Filamu Tz haiwezi kufika level ya Kimataifa"

MSANII gwiji wa filamu Ester Flavian Mushi, ameweka bayana kuwa tasnia ya filamu nchini haiwezi kufikia kiwango cha kimataifa kutokana na uzembe unaofanywa na wakuu wa kazi hizo.
Flavian (22) ambaye mwaka 2009 alishiriki masuala ya urembo katika ngazi ya kitongoji mjini Tanga na kushika nafasi ya pili na baadaye Miss Dar Indian ocean, alisema viongozi wa filamu wanachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya filamu na kwamba wanaangalia sura badala ya kipaji.
“Filamu ya Tanzania inauwezo mkubwa wa kukua lakini kutokana na tatizo la kutokupeana nafasi kwa wasanii wenye vipaji haiwezi kufikia ngazi ya kimataifa,” anasema.
Flavian anasema, baadhi ya wazalishaji (Producer) na wakurugenzi hawaangalii vipaji vya wasanii badala yake wanaangalia uzuri wa mtu hata kama hana kipaji.
“Hili ni tatizo kubwa kwa kuwa hawaangalii kazi hiyo itapeleka ujumbe gani kwa jamii bali yeye anaangalia ninamna gani atauza kazi yake. Maadili yanapaswa kuzingatiwa katika kazi,” anasema.
Kwa mujibu wa Flavian, alianza kushiriki filamu mwaka 2008 ambapo alianza na filamu ya is too late, Fack pregnant, Zawadi ya oparetion, Miss Zinduna, No way Out, Ant Suzi, Big Brother na nyinginezo.

Saturday, August 6, 2011

Mlela afunguka kuhus wazalishaji (Producers)...


MSANII machachari wa filamu nchini Yusuph Mlela ameamua kuvunja ukimya baada ya kudai kuwa wazalishaji wa filamu (Producer) wanashusha viwango vya utendaji kazi wa wasanii.
Mlela anasema asilimia kubwa ya wazalishaji hao wamekosa uaminifu katika kazi hiyo hali ambayo ni kinyume na maadili ya kazi na inayokatisha tamaa kwa wasanii.

“Sanaa yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya maproducer kushindwa kuwalipa wasanii fedha zao kwa muda, unaweza kucheza filamu ukamaliza lakini usilipwe fedha halali uliyokuwa umeahidiwa, hili ni tatizo,” anasema.
Anasema, wazalishaji wanatakiwa kuwa waaminifu ili tasnia ya filamu iweze kukua na kutoa motisha kwa wasanii utakaosaidia kuwafanya waipende kazi na kubadilisha mfumo mzima wa sanaa nchini.

 “Gemu ya sanaa imekuwa sana hata soko limekuwa kiasi ingawa bado unyonyaji upo, hatuna hatimiliki na ndio maana hata kazi zetu hazitoki nje ya Tanzania,”anasema.
Anasema, serikali inatakiwa kuingilia kazi za wasanii ili kusaidia kulinda faida yao na kwamba sanaa inaajiri vijana wengi.

Akizungumzia mafanikio yake Mlela anasema, amefanikiwa kumiliki kampuni yake mwenyewe (Mlela Production) itakayoshughulika na masuala ya picha na matangazo.
“Kampuni ndio imeanza kufanya kazi hivi karibuni, tumeanza kushuti filamu itakayotambulika kwa jina la Mayenzo, imechezwa na Hemed Suleiman, Slimu, Nishi na mimi mwenyewe,”anasema.


WAREMBO WAANDAA FUTARI KWA WAANDISHI..


WAREMBO wa  Redds Miss Ilala, Kinondoni na Temeke, mwishoni mwa wiki hii waliandaa futari kwa wahariri na wandishi  kama sehemu ya shukrani kwa ushirikiano waliopata kihabari muda wote waliokua katika michuano ya kanda zao pamoja na kuwaaga wanahabari hao tayari kwa kuanza kambi ya taifa August 8.

 warembo wa Miss Kinondoni, Ilala na Temeke wakibadilishana mawazo katika hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari na warembo hao.
Baadhi ya warembo walioshiriki Mashindano hayo ya Urembo ya kanda tatu za Dar es Salaam wakichukua chakula (ftari) wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajli ya warembo hao pamoja na waaandishi wa habari iliyofanyika katika hotel ya city garden. (Picha na Frank Aman).

. Meneja wa kinywaji cha Redds, Victoria kimaro akizungumza na waandishi wa habari ijumaa jioni jijini Dar wakati wa hfla fupi ya ftari iliyoandaliwa kwa ajili ya waandihsi wa habari na warembo wa kanda tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni Temeke, Ilala na Kinondoni. (Picha na Frank Aman). 
 Mzigo ulivyoendeka...
Kushoto ni Redds Miss Kinondoni Stella Mbuge, katikati ni Salha Israel Redds Miss Ilala na kuria ni Husna Twalib Miss Temeke 2011.
 Redds brand manager Victoria Kimaro akiwa na mdau Evancy ngingo.
 Warembo wakipatiwa maneno ya mwisho na Meneja wa Redds Vick katika hafla hiyo.