BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Monday, April 9, 2012

HISTORIA YA STEVEN KANUMBA


HISTORIA YAKE:

Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.

Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.

Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.

Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.

Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.

Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.

Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.

Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.

Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.

Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.

Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.

YANAYOENDELEA KATIKA MSIBA WA KANUMBA...

 MAREHEMU STEVEN KANUMBA ENZI ZA UHAI WAKE.
 mdogo wa marehemu akizungumza na waandishi wa habari
 kamati ya inayoshughulikia msiba wa kanumba pamoja na mazishi yake
 baadhi ya wasanii wa kike walioko msibani
 hii ni picha iliyowekwa msibani katika kitabu cha mahudhulio na rambi rambi.
 msanii wakipelekwa sehemu ya hewa baada ya kuzirai msibani
 baadhi ya wasanii, watanzania wapenzi wa filamu na marehemu Steven kanumba.
 Baadhi ya watu waliohudhulia msibani
 Mainda mmoja wa wasanii wa filamu na aliyekuwa msanii wa karibu na kanumba eznzi wakiwa Kaole Sanaa group.
 Mama wa marehemu akiwa katika majonzi.
 Msanii wa filamu Johari
Mke wa aliyekuwa Spika wa Bunge Samuel Sitta..

Saturday, April 7, 2012

BAADHI YA MATUKIO KATIKA MSIBA WA KANUMBA NYUMBANI KWAKE SINZA VATICAN..





Blog ya filamutanzania.blogspot.com ikishirikiana na watanzania wengine na shrikisho la filamu tanzania inakuomba mdau kutoa mchango wako wa rambi rambi ili kuwezesha mazishi ya msanii nyota wa filamu tanzania Steven Kanumba... waweza kutoa mchango wako kupitia namba zinazotolewa nan vyombo vya habari fuatilia...

YANAYO ENDELEA BAADA YA KIFO CHA KANUMBA.

YANAYO ENDELEA BAADA YA KIFO CHA KANUMBA.

PICHA YA MAREHEMU STIVIN KANUMBA PEMBENI YAKE KUKIWA NA MSHUMAA IMEWEKWA UKUMBINI NYUMBANI ALIPOKUWA AKIISHI SINZA VATICA.
 Baasdhi ya watu wa karibu na msanii huyo wakiwasili nyumbani kwa msanii huyo leo mapema asbuhi.
 Wasanii waliowahi kufika mapema leo asubuhi nyumbani kwa kanumba wakiwa wamekaa kwenye mikeka kabla hapajafungwa matent wala viti vikiwa havijaletwa bado. Huzuni na vilio ni kitu kilichokuwa kimejiri kwenye eneo hilo.
 Mwanamitindo Mashuhuri nchini Tanzania Hapiness Magese, akiwasili nyumbani hapo huku akiwa na huzuni.
 Wema Sepetu zao la Msanii Kanumba alikua hajiwezi kabisa akitokwa na machozi muda wote nyumbani hapo.
 Kwauujumla idadi kubwa ya watu waliofika muda wa asubuhi ni wasanii wenzake majirani na mashabiki wake wa eneo la Sinza.
 Mawasiliano yalikuwa ni muhimu ilikutoa taarifa na kuwaelekeza watu eneo husika, huyu ni mchekeshaji maarufu kwa jina la Mboto.

Vijana mbalimbali walijitokeza kusaidia kazi, hapa vijana hawa wakibeba choo cha kuhamisha ikiwa ni maandalizi ya kuweka huduma muhimu kwa watu watakao fika nyumbani hapo.

ENDELEA KUFUATILIA TAARIFA HIZI ZITAKUJIA KILA WKATAI.

NINI KILITOKEA HADI KANUMBA AKAPOTEZA MAISHA

 

TAARIFA za tukio zima nilizona baada ya kuhangaika tangu saa 11:30 alfajiri hadi sasa kwa kuanzia kule Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi sasa ni kwamba kanumba alikwaruzana na rafikiyake wa Kike ambaye ni Elizabeth Michael (Lulu) Pichani.
Mikwaruzano hiyo ambayo ilianza majira ya saa saba za usiku iliendelea wakaamua kujifungia chumbani ambako walikua wakirushiana maneno ambayo hata hivyo kwa mujibu wa mdogo wa marehemu hakuwa tayari kuielezea kikamilifu.

Baada ya hapo Lulu alitoka Chumbani na kumwabia mdogowake Kanumba kuwa Kanumba ameanguka nnjoo, baada ya kwenda akakuta haliyake ni mbaya akaamua kumpigia simu daktari wake kanumba.

"Nilivyo mpigia daktari wake akiniambia sina usafiri saivi, basi mimi nikachukua gari nikamfuata, alipofika daktari wake akampima akasema muwaishe Muhimbili saivi," alisema

Hata hivyo alisema alionekana akiwa tayari ameshafariki kabla hata hajafikishwa Muhimbili.

POLISI
KAMANDA wa polisi wa Wilaya ya Kipolisiya Kinondoni Charles Kenyera, alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema wanamshikiria rafiki wa kike wa Muigizaji huyo ambae yupo kitujo cha Polisi cha Osterbay.
Kamanda Kenyera alisema bado wanaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo na mara upelelezi utakapo kamilika watatoa taarifa kaili.

MASHUHUDA


Watu waliowahi kufika nyumbani kwa kanumba waliona polisi wakifungua chumba cha kanumba na kutoka na Chupa ya Pombe aina ya Jack Daniel ikiwa na pombe kama robo imebaki, glasi ikiwa na kiasi cha pombe kidogo pamoja na Panga pichani.

Hata hivyo wanandugu pamoja na kamati nzima ya mazishi ikiongozwa kwa kiasi kikubwa na wasanii pamoja na watu wa karibu wa kanumba wanasema taarifa za namna ya kifo kilivyotokea kwa jeshi la polisi hivyo kwa sasa familia.


ENDELEA KUFUATILIA TAARIFA ZAIDI.
 
Habari hii ni kwa hisani ya blog ya saidpowa.blogspot.com tembelea kwa taarifa zaidi.

Tuesday, December 6, 2011

Ramsey awaasa wasanii wa muvi bongo..


VIPAJI vina nafasi kubwa katika ulimwengu wa sanaa, lakini kuna wakati lazima mhusika atafute elimu kwa ajili ya kulinda na kuendeleza kipaji chake.

Hayo ni maneno ya mwigizaji mahiri wa filamu Bongo, Hashim Kambi Ramsey aliyoyatoa hivi karibuni katika mazungumzo yake na Mwanaspoti.

Wakati naanza kuigiza nilikuwa najua ni kitu cha kujifurahisha tu, nilifanya hivi huku nikiendelea na shughuli nyingine, anasema Ramsey.

Lakini nimebaini uigizaji ni kazi. Inakuhitaji mtu uwe na taaluma hiyo ili uweze kudumu nayo katika kiwango bora.

Kinachosikitisha tu ni kuwa kuna hili tatizo la gharama kuwa kubwa kwa masomo ya filamu.

Akielezea zaidi, anasema kwamba wasanii wanaweza kujiendeleza kwa njia ya mitandao ya filamu, kama anavyofanya yeye.

MAGIC MONEY SOKONI HIVI KARIBUNI.


'PESA SHETANI ASIYE EPUKIKA KATIKA DUNIA HII YA SASA NA USIOMBE ABISHE HODI NDANI YA FAMILIA KABISA'' ...KUMKANYWA NA KUPEWA TAHADHALI KWA MTU NDIYO KUMTIA HAMASA NA MUWASHAWASHA KUITIKIA KIU YA NAFSI YAKE YA TAMAA YA PESA NA HAPO MAISHA YA KUKIMBIA DAIMA HUANZA NA NDIYO MATOKEO YAKE KAMA SIO KUKOSANA NA NDUGU AU MPENZI/MUME/MKE WAKO...MTIZAME BINTI HUYU NAMNA NDOA YAKE INAVYO TIBULIWA NA SHETANI (PESA)


CAST
Daudi Michael (DAUDI)
Hemed Suleiman (ERICK)
Halima Yahaya (SANTANA)
Msafili Njechele (BUGO)
Ibrahim Lipili(NYANGO)
Ratifa Idabu (BADRA)


STORY
Daudi Michael
SCRIPT
Daudi Michael
EXCTIVE PRODUCER
D.Production
(A DAUDI MICHAEL FILM PROMO)

Sunday, December 4, 2011

SAJUKI AFUNGUKA KUGAWANYIKA KWA WASANII...

MWIGIZAJI na mwongozaji wa filamu Bongo, Juma Kilowoko Sajuki, amesema watayarishaji wa filamu wamegawanyika katika makundi, ingawa ni vugumu mwingine kulibaini hilo.

Akizungumza na jukwaa hili nyumbani kwake Tabata Bima, jijini Dar es Salaam, msanii huyo ambaye kwa sasa anasumbuliwa na tumbo, anasema kuwa mara nyingi wale ulio karibu nao ndiyo hukuzunguka.

Sisi wasanii tayari tuna makundi japo tunafanya kazi moja, kwa mfano mimi rafiki zangu labda Frank au Dino, basi watakuwa ni hao tu, hata linapotokea jambo kama la msaada wao ndiyo watawajibika, alisema.

Hata kama mtu akiongea na mwingine atasema kuwa huyu jamaa hajichanganyi na watu, lakini ukweli tunajuana kuwa kila mtu na mtu wake. Msanii huyo alisema japo jambo hilo lipo, lakini si rahisi kuyataja makundi hayo. Kutokana na hali hiyo, anawataka wasanii kujilazimisha kujenga umoja wa kweli kuliko ilivyo sasa.

MABINTI WANAOTETEMESHA VIDUME NOLLYWOOD..

MERCY Johnson ameshaolewa. Nani anafuata? Ndiyo swali wanalojiuliza mashabiki wa filamu za Nollywood, asilimia kubwa ya wasanii wa kike hawajaolewa na wengine hawana hata mpango na hayo mambo.
Wengine walishaolewa wakaachika kutokana na kuendekeza starehe na kushindwa kutulia kwenye ndoa zao. Hii ni orodha ya mabinti ambao hawajaolewa na wanaotetemesha wanaume Nollywood. 

Funke Akindele
Huyu binti ana mafanikio makubwa kikazi na ni miongoni mwa wasanii wanaolipwa sana. Ana umri wa miaka 35, hana skendo nyingi za mapenzi kama walivyo mastaa wengine wa Nollywood.
Yuko kwenye uhusiano wa kudumu na huenda muda wowote akatamka jambo kwa marafiki zake.
Amesomea sheria kwenye Chuo Kikuu cha Lagos. Baadhi ya filamu alizowahi kufanya ni kama Jenifa, Omo Ghetto na Return of Jenifa Part 2. 

Rita Dominic
Sura na umbo lake vinadanganya watu wengi sana, ukimwangalia kwa haraka unaweza kudhani ana umri wa miaka 25, lakini kwa taarifa yako ana miaka 37 sasa na bado pia yumo kwenye kundi hilo la mabachela.
Mambo yake ya uhusiano wa zamani hayajafunuliwa sana lakini aliwahi kuwa na uhusiano na msanii mwenzie, Jim Iyke, hususani alipokuwa anaishi maeneo ya Wemabod Estates, Ikeja. 

Genevieve Nnaji
Miaka yake ni 32 na anatafsiriwa kama nembo ya filamu za Nollywood Afrika na Dunia nzima. Ni miongoni mwa mabinti matajiri Nigeria, lakini bado hajabahatika kufanya maamuzi magumu ya kuachana na ubachela.
Ana mtoto mmoja wa kike na awali alishavumishwa kuwa na uhusiano na Makamu wa Rais wa zamani wa Nigeria, Abubakar Atiku. 

Chika Ike
Ni mzuri na ana mvuto. Aliolewa lakini baada ya muda akaachika kwa sababu ambazo marafiki zake wa karibu waliziita za kitoto na ni binti wa kuendekeza sana starehe. Amenunua Range Rover ya kisasa na amefungua saluni za kisasa jijini Abuja, kama ni fedha anayo. 

Uche Jombo
Anawatoa udenda wengi. Lakini rafiki yake wa karibu amedokeza kwamba huyu binti hana mpango wa kuolewa sasa hivi, akili yake imekaa kibiashara zaidi. Anatengeneza fedha sana na anajua kuzitumia.
Anaishi maeneo ya Lekki jijini Lagos. Ametamba na filamu kama Secret Fantasy, Endless Lies, Kiss and Tell, Silent Scandal na Home in Exile. Miaka yake ni 32 na ni msomi wa Chuo Kikuu cha Calabar, Nigeria. Aliwahi kuwa na uhusiano na Ikechukwu Uche ambaye ni mchezaji. 

Monalisa Chinda
Ni bachela mzoefu. Aliolewa akazaa mtoto mmoja maisha yakamshinda akaamua kurudi kwao na sasa maisha yanaendelea kwa staili ya kujirusha kwa wingi.
Mwanaume waliyeachana naye ameshaoa lakini Monalisa bado yupo yupo ingawa inaelezwa wanaume wengi sana wanamnyemelea. Amesomea sanaa kwenye Chuo Kikuu cha Port Harcourt kwao Nigeria. 

Stephanie Okereke
Kila kukicha ana skendo na sura yake haikosekani kwenye kurasa za mbele za magazeti ya udaku. Kwenye masuala ya urefu na uzuri kote amesheheni.
Alishawahi kuolewa pia akaachika sasa hivi yuko kwenye penzi zito na jamaa mmoja anaitwa Linus Idahosa. Hakuna anayejua ni lini wana mpango wa kuoana.

MATANGAZO YA BIASHARA HAYA LIPI.... Ray

NYOTA katika tasnia ya filamu Bongo, Vincent Kigosi (Ray), amesema matangazo ya biashara hayalipi na ndiyo maana hashiriki katika kutengeneza matangazo hayo kwa sababu hayana faida kwake.

Si kama sipati matangazo ya biashara kwa ajili ya kutangaza bidhaa, fedha wanayotoa wahusika ni ndogo sana kiasi cha kukatisha tamaa, siwezi kutumika katika matangazo kwa pesa ndogo wakati nikitengeneza filamu naipata zaidi ya hiyo, alisema Ray.

Kwa wale wanaopenda sifa za kuonekana bila faida waache tu wafanye, lakini mimi msimamo wangu upo kimaslahi zaidi.

Msanii huyo alisema kuwa tatizo la matangazo hayo pamoja na kuwa malipo ni kidogo, lakini hayana ukomo wa muda wa kutumika. 

Mwenye bidhaa husika ana uwezo wa kulitumia hata milele bila kuendelea na malipo mengine, sasa hii si halali kabisa, aliongeza.

Mara nyingi makampuni hunifuata, lakini kila linapofika suala la malipo na ukomo wa tangazo wanakimbia, kuna tangazo ilitakiwa nilifanye, lakini baada kuambiwa kuwa nitalipwa dola 2,500 (Sh 223,864 za Kenya) na litatumika milele bila malipo ya ziada nilikataa.

Msanii huyo alisema kama kuna kampuni inataka kufanya kazi naye anaikaribisha, lakini ikubali kutimiza masharti yake kwa kuwa na mkataba unaoeleweka na si wa kuuza sura.