BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Friday, October 28, 2011

WASAMBAZAJI WANAZINGUA ASEMA ROSE...


MTAYARISHAJI na mwigizaji nyota wa filamu wa Bongo, Rose Ndauka, amesema kuwa filamu yake ya Diary imeshindwa kuingia sokoni mapema kwa sababu ya matatizo ya usambazaji.

Badala yake ameamua kuigiza filamu ya Ruben n� Angel wakati akijaribu kumtafuta msambazaji anayefaa.

Filamu ya Diary ilikuwa itoke mapema kabla ya filamu ya Ruben n� Angel, lakini kutokana na matatizo ya usambazaji ameamua kusitisha zoezi hilo. 


Mwanadada huyu ambaye anamiliki kampuni yake inayojulikana kwa jina la Rose Ndauka Entertainment, anatayarisha filamu zake mwenyewe pia na kushiriki filamu nyingine.

�Nilikuwa nimewaahidi wapenzi wa kazi zangu kuwa filamu ya Diary inatoka mwezi huu, na watu walikuwa wanasubiri kwa hamu itoke, lakini ratiba imebadilika badala yake nimetoa filamu nyingine ya Ruben n� Angel,� alisema Ndauka.

Filamu ya Ruben wameshiriki wasanii kama Khaleed Tajiri, Irene James, Ndauka na wasanii wengine filamu hiyo ipo mtaani ikiendelea kuuzwa.


Saturday, October 15, 2011

Aunt Ezekiel asema hajafungiwa...


BAADA ya uvumi wa kufungiwa kwa mwigizaji Aunty Ezekiel kuenea , mwenyewe amefunguka na kusema kuwa huo ni uvumi tu ambao hata yeye amekuwa akiusikia tu bila kujua chanzo chake.

“Sijui nani aliyeanzisha habari hizi, lakini mimi sijafungiwa na sasa ninapozungumza na wewe nipo mzigoni nikiandaa filamu yangu mpya ambayo nitaiingiza sokoni muda si mrefu,” alisema Aunty.

Aunty amesema filamu yake hiyo itaitwa House Boy and House Boy na itakuwa ikielezea maisha ya kila siku ya wafanyakazi wa ndani.

Mwenyekiti wa Bongo Movie, Jacob Steven amesema umoja wao huo haukumfungia kuigiza, bali asingeruhusiw akufanya kazi na msanii yoyote wa umoja huo.

Hata hivyo alisema Aunty ameshajirekebisha kwahiyo anaweza kuendelea na kazi kama kawaida.

Hata hivyo kufungiwa kwa Aunty kuna leta utata kutokana na waigizaji kuwa na vyama mbalimbali ambvyo mpaka sasa hakijukani kipi chenye nguvu ya kuweza kumfungia msanii.

Kipindi cha nyuma kulikuwa na shirikisho la wasanii wa filamu TAFF ambalo inasemekana liliundwa baada ya serikali kuamuru uundwe umoja utakaowawakilisha kwenye shughuli mbalimbali.

Baadae ukaundwa umoja huu uitwao Bongo Movie ambao wasanii wengine wanadai kutoutambua kutokana na mazingira yake nakusema kuwa umeundwa kwaajili ya maslahi ya wasanii wachache.

Saturday, October 1, 2011

Kitu Kipya kabisa kwenye game...

 
RATIFA MTOBI (TANITA)
Amezaliwa Tanga miaka kumi na tisa iliyopita. Mwigizaji wa Tuesday Entertainment. anapendelea kuogelea na riadha.
 
Ni Mwanadada Chipukizi ambaye yuko pamoja na actors wengine katika tamthiliya ya Millosis inayorushwa TBC1 kutoka kwa Director Tuesday Kihangala.

Shirley; Nyota anayetikisa kwenye tamthiliya ya Millosiss...


Jina halisi la chipukizi huyo ni Celina Victor, lakini mashabiki wa filamu wanamfahamu kwa 'Shirley', msanii ambaye aliweza kuonesha uwezo katika tamthilia ya 'Jumba la Dhahabu'.
Nyota huyo anajitahidi kusaka umaarufu lakini bado ana changamoto nyingi za kucheza filamu ambazo zitazidi kumweka juu kama ilivyo kwa The Sandy kazi ambayo inafanya vizuri.


Katika mawasiliano na mdada huyu na blog hii kupitia mtandao wa Facebook Shirley alifunguka na kutaja kazi mbali mbali ambazo aliwahi kufanya na bado zingine zinazotarajiwa kutoka hivi karibuni.


“Kazi nilizowahi kucheza ni jumba la dhahabu (series) + movies nilizoshiriki kuna mboni yang ya kina sajuki, zingine indecency, jasho la kifo, hostell na XXL ambayo haijatoka bado. Also nipo kwny drama inaitwa millosis inaruka Tbc kwa sasa,” alisema Shirley.

Tuesday, September 27, 2011

Loveness afunguka kuhus mahusiano...


MUIGIZAJI wa filamu za Bongo, Loveness Watson amebainisha kuwa yeye katika maisha yake hapendi kabisa kuolewa kwani hawezi kuwa huru kama alivyo sasa.
Amesema kulingana na kazi yake ya utayarishaji wa filamu anaamini akiwa mke wa mtu hatapata fursa ya kufanya kazi zake zinamfanya akose muda wa kuwepo sehemu tofauti.
�sipendi kuolewa kabisa kutokana na ndoa za watu ninazoziona, lakini mimi kazi zangu za kushinda sana sehemu ambazo tunarekodi na kurudi muda wa usiku, mume gani atakubali kusubiri mke mwenye kazi nyingi hivyo? "Najikuta nashindwa kujigawa katika ya mume na kazi, sanaa naipenda ipo katika damu,� alisema msanii huyo.
Loveness aliwahi kudaiwa mara nyingi hujifanananisha na Rose Ndauka na hata kutumia jina la mwanadada huyo kwa ajili ya kujipatia sifa, lakini yeye anakataa jambo hilo na kusema kuwa hawezi kufanya hivyo, kwani kazi anazofanya Rose naye anafanya.
Msanii huyo ameigiza filamu kama Sheria Mkononi, Impossible Promise, Fake Love, Penzi la Utata, Blood in the City na Doctor Thomas.

Sunday, September 18, 2011

MSISIMKO WA FILAMU YA CPU UMEFIKA.

 Mmoja kati wasanii waliofika katika usahili wa filamu ya CPU.
ULE msimu wa mapinduzi ya tasnia ya filamu Tanzania unakuja, tunasema kuwa Msisimko wa CPU umefika, na tayari watu kila kona wanasubiri ili waone filamu ya kwanza Tanzania kurekodiwa kwa teknorojia ya kisasa kabisa, kama umepata kusikia habari hizi basi si filamu nyingine ni CPU.
Wasanii wakisubiri kuingia chumba cha usahili.
Timu ya wataalamu kutoka sehemu mbalimbali, wiki hii walikuwa na kazi kubwa kwa ajili ya kufanya usahili wa wasanii wenye sifa na muonekano wa kuigiza filamu ya CPU, timu hiyo tayari imeshawapata wasanii kadhaa na zoezi linaendelea chini ya usimamizi wa kampuni ya Haak Neel Production.
Akiongea na vyombo vya habari meneja masoko wa kampuni hiyo God Mahendeka amsema kuwa
“Wasanii wanaohitajika ni wengi na kuna wasanii ambao tayari wamepita katika usahili na kuanzia sasa timu iliyofanya kazi hiyo itaanza kutangaza majina ya wasanii waliopita katika usahili, na kuhusu vifaa kwa ajili ya urekodiji wa filamu hiyo vipo tayari, watalaamu wanasubiri tu kazi ianze, ” anasema God.
Filamu ya CPU ni filamu ya kwanza ambayo inatarajia kuonyeshwa katika majumba ya sinema Afrika Mashariki, filamu hiyo inashirikisha kampuni mbili kubwa za utayarishaji wa filamu yaani Haak Neel Production na Wegos works ltd, kuanzia sasa kila mara tembelea mtandao huu kupata habari za kusisimua kuhusu filamu ya CPU. USIKOSE!!

Habari hii ni kwa hisani ya filamucenteral.co.tz

Wednesday, September 14, 2011

WASANII WAONYWA KUHUSU MAKUNDI WANAYOFANYA YA KUPONDANA...

MSANII mwenye fani lukuki sokoni, Mshindo Jumanne amebainisha kuwa katika sakata linaloendelea sasa kuhusu maslahi ya wasanii tatizo lipo kwa Wasanii na si kwa Wasambazaji.
Mshindo ambaye pia husambaza filamu ambazo anazitengeneza mwenyewe na baadhi ya filamu za watayarishaji wengine alibainisha hayo kuwa mara nyingi wasanii wanajitenga na kutengeneza makundi ambayo yanapingana yenyewe kwa yenyewe badala ya kuwa na kauli ya pamoja.
Tatizo kubwa ni sisi wenyewe wasanii kwa sababu hatuna umoja ambao unaweza kutuongoza katika kuzalisha filamu zenye ubora huku tukipata maslahi kwa kila mhusika, kwa sasa hali ni mbaya kuliko awali maana unafanya kazi hata hauna uhakika wa kuuza filamu yenyewe.
"Kuna msambazaji mmoja tu mwenyewe nguvu ambaye analalamikiwa lakini watu wanasahau kuwa yeye ni mfanyabiashara na hakuna mtu anayefanya biashara kwa ajili ya mtu mwingine,alisema na kuongeza kuwa wasanii ambao ni nyota ndiyo kikwazo cha ukuaji wa tasnia ya filamu Bongo.
Anasema mara nyingi mtu akiandaa filamu na kuwashirikisha kwa sehemu chache hawataki bali huhitaji kucheza kila filamu kama ni waigizaji wakuu, jambo ambalo yeye anapingana nalo kwani haiwezekani muswada (script) umfuate msanii.

Wabongo wanammendea Funke Akindele...

INAWEZEKANA wabongo wamo pia. Mamia ya wanaume mabachela wamefumuka kutoka kila kona ya Nigeria na Afrika wakiomba kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa Nollywood, Funke Akindele.
Msanii huyo aliliambia gazeti moja maarufu jijini Lagos wiki iliyopita kwamba anahitaji mwanaume wa kumuoa na yuko tayari kwa yoyote atayejitokeza mwenye msimamo na anayeeleweka, ila akatoa angalizo kuwa awe anamuogopa Mungu. Habari hiyo ilichapishwa pia na kwenye ukurasa huu Jumanne iliyopita.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, mabachela zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali za Afrika wamepiga simu, kutuma barua pepe na ujumbe wa simu wakimuwania msanii huyo.
Katika orodha ya wanaume zaidi ya 200 iliyochapishwa kufikia juzi jioni, wengi wametoa namba zao za simu, ahadi na kila mmoja alikuwa akijinadi kwa maneno matamu na kuomba mawasiliano ya binti huyo.

Lucy.. kazi za sanaa zamkosesha muda wa kumuhudumia mtoto...


IMEKUWA furaha kwa wasanii wa kike pale wanapofanikiwa kupata mtoto au watoto ambapo wengi wao hupenda kuwahudumia watoto wao kwa asilimia kubwa.
Lengo ni kuweza kumpatia mtoto wake huduma anazostahili na kuweza kuwa karibu naye zaidi ingawa baadhi husema ni njia ya kujigamba kwa wengine.
Lakini kwa Msanii gwiji wa filamu Lucy Komba (31)amekuwa tofauti sana kwani yeye mtoto wake Strom Mbasha (2) anakosa muda mwingi wa kumhudumia kutokana na kutingwa na kazi hivyo mara nyingi anahudumiwa na wasichana wa kazi.
Wiki kati msanii huyo alizungumza kwa kirefu na mwandishi wa habari hii Minael Msuya kuhusu maisha yake nje ya sanaa.

Mwandishi: Wewe ni mama wa mtoto mmoja vipi, unamhudumiaje mtoto wako kabla ya kwenda kazini?
Lucy: Napenda kuwa mkweli siku zote, mimi naamka saa kumi na moja alfajiri hapo najiianda kwenda kazini, mwanangu anakuwa amelala bado. Hivyo sina ninachomuandalia.

Mwandishi: Kwa hiyo mtoto wako anahudumiwa na nani kama wewe unapoamka hufanyi shughuli yoyote tena ukizingatia bado mdogo?
Lucy: Pale nyumbani tuna wasichana wawili wa kazi, mmoja ni maalumu kwa kumhudumia mtoto na mwengine anafanya kazi zingine hivyo mwanangu anahudumiwa zaidi na wasichana wa kazi.
Mwandishi: Hujisikii vibaya mwanao anavyohudumiwa na wasichana hao,

Lucy: Nammis sana mwanangu na ninampenda zaidi hivyo jioni ninaporudi nyumbani na siku za mapumziko namhudumia muda wote, kwani napenda nimhudumie mwanandu wakati wote mwenyewe isipokuwa kazi zinanibana.
Mwandishi: Kwani unafanya shughuli gani zaidi mpaka ukose muda wa kumhudumia mwanao?
Lucy: Kama unavyoniona hapa ofisini, mimi ni Katibu Muhtasi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, muda wangu unabana sana hata baadhi ya kazi zangu za sanaa nashindwa kuzimudu.

Mwandishi: Una muda gani na kazi yako hii, vipi kuhusu familia yako inakutegemeaje?
Lucy: Muda mrefu kidogo nilianza hapa tangu mwaka 2003, kwenye familia kwa kweli nahudumia kawaida, mama yangu ndiye anayeitunza familia na kwa sasa bado niko chini ya himaya ya mama yangu siwezi kujigamba kwa chochote.

Mwandishi: Baba wa mtoto unaishi naye au vipi?
Lucy: Siishi na mume hata hivyo sina mpango wa kuishi naye kwa sasa labda baadaye sana.
Mwandishi: Matarajio yako baadaye ni yapi?
Lucy: Matarajio yangu ni kuwa msanii na mtunzi mahiri wa kimataifa ili niweze kuonyesha kipaji change na kuongeza kipato changu zaidi ili familia yangu hasa watoto wangu niweze kuwahudumia na kupata elimu bora.

Mwandishi: Tofauti na sanaa unamatarajio gani mengine?
Lucy: Mh! Mimi naipenda kazi yangu ya uigizaji zaidi hata hii niliyonayo ni kwa sababu tu nimesomea lakini nafikiria kuifanya sanaa kuwa kazi yangu pekee na nitafanya ndani na nje ya nchi. Naamini ndoto yangu itakuwa imetimia kwani hivi sasa sanaa inakuwa kwa kiwango kizuri na ninapenda kuibua vipaji vya wasanii wengi zaidi kama ilivyokuwa kwa wasanii mahiri na wanaokubalika Mzee Chilo, Iren Uwoya, Mkwere na wengine wengi.
Mwandishi: Nikitu gani ambacho usipokifanya kwa siku unaona kama hujafanya kazi siku hiyo?
Lucy: Dah! Nimelipenda swali lako maana umeigusa mboni ya jicho langu, napenda sana kuandika na kufikiria stori mpya kichwani na kuiandaa. Kila siku moja najitahidi niandike japo mistari kadhaa ya stori zangu ili niweze kuandaa filamu zangu na kazi yangu isidumae, nisipofanya hivyo kwangu sioni kama siku  imeisha hii ni kwasababu naipenda kazi ya uigizaji kuliko vitu vingine vyote.
Mwandishi: Maishani mwako unampango wa kumiliki kitu gani ambacho unaona kitakuwa na manufaa kwako?
Lucy: Ninampango wa kumiliki nyumba ya ghorofa moja, tayari nimeanza ujenzi wa nyumba nyangu hiyo maeneo ya Bunju. Wasanii wengi wa bongo wanapenda ufahari wa magari mimi nahitaji kuwa na gari aina ya sports nafikiri litanisaidia kwa shughuli zangu.  
Mwandishi: Je ungependa kuwa na watoto wangapi na mume atakayekuoa awe na vigezo gani?
Lucy: Napenda Mungu akinisaidia niwe na watoto watatu, pia mume wangu asiwe na tabia chafu, anizidi mimi urefu, awe mweupe, mtanashati, mpole na mwenye uwezo wa kutunza familia.