BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Saturday, April 14, 2012

Ini Edo ala kiapo.....


Mwigizaji huyo anasema ingawa ndoa yake ni ngumu kwa kuwa mume anaishi Marekani na yeye Nigeria, anajitahidi kwa nguvu zote kuhakikisha haiyumbi.

Siyo rahisi kuimudu ndoa ya aina hii, lakini nimejiwekea mipaka ya kazi na maisha binafsi, unapokuwa muda wa kupiga kazi nafanya hivyo na unapofika wa kuwa na mume wangu, nakwea pipa kumfuata, anasema Edo.

Anaongeza kuwa pamoja na kuwa anatumia nguvu nyingi kuifanya ndoa yake idumu, lakini anashukuru kwa kupata mume muelewa ambaye anapohisi kazidiwa na kazi huwa anamfuata Nigeria kuwa naye pamoja.

Edo ameongeza kuwa ni miaka mitatu sasa tangu afunge ndoa na mwanamume huyo kwa hiyo kilichopo katika mpango ni kutafuta mtoto na kuanzisha familia.

BABA MZAZI WA LULU AFUNGUKA...


BABA mzazi wa Muigizaji wa kike wa filamu nchini maarufu kama Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake. Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta (49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro 

BABA mzazi wa Muigizaji wa kike wa filamu nchini maarufu kama Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake.
Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta (49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, kaiambia Globu ya Jamii leo huko Moshi kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mtoto wake Lulu, lakini hakuamini masikio yake baada ya kupata taarifa za kifo hicho, huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu, anahusika.
Lulu alifikishwa mahakamani juzi Aprili 11, 2012 akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya Marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada ya kifo cha msanii huyo.
Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Midway mwaka jana na kwamba hivi sasa ana umri wa miaka 17.
Bw. Kimemeta alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika uchunguzi wao kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven Kanumba.
Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu, huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi.
“Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth”, alisema baba mtu.
“Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na kusaidia katika kupatikana kwa haki dhidi ya shitaka la mauaji linalomkabili binti yangu Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake” alisema.
Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo, ambapo chanzo kinasemekana ni ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa wivu wa kimapenzi na haiyumkini hakukusudia kumuua hivyo yeye anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji.
“Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uhai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa Lulu na kusema kuwa ataendelea kubaki kama mwalimu.. lakini leo nasikia alikuwa ni mpenzi - nilishtushwa” alisema Kimemeta.
Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa kushindwa kuhudhuria mazishi ya marehemu Steven Kanumba kuhofia usalama wake, na kusema mazingira yatakaporuhusu hata sitaki kufika nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba na kutoa pole.
Bw. Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo mkubwa ambao haukutarajiwa.
Kasema kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla.
 
HABARI KWA HISANI YA BONGOFLAVALINK.BLOGSPOT.COM

MCT yawaonya wanahabari kuhusu ‘Lulu’


BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limewaasa waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi yao  hususan wakati huu wa kuripoti kesi inayomhusu Elizabeth Michael ‘Lulu’.


Akizungumza Jijini Dar es Salaam Jana na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya MCT Jaji Mstaafu Thomas Mohayo alisema wadau wa tasnia ya habari wamekuwa wakimhukumu moja kwa moja Lulu kuwa ndiye aliyemuua Steven Kanumba.


“Kwa mjibu wa sheria na maadili ya uandishi wa habari mtu yeyote anayekamatwa kwa tuhuma yoyote ile ni mtuhumiwa mpaka atiwe hatiani na mahakama” alisema Jaji Mohayo na kuongea:


MCT inasikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa ukiukwaji mkubwa wa maadili uliojitokeza hivi karibuni wakati vikiripoti kuhusu kifo cha Kanumba vimemuhukumu Lulu kuwa amemuua kinyume na maadili ya kazi yao.


Jaji Mihayo  alisema MCT kwa nyakati tofauti imekuwa ikitoa matamko yanayowakumbusha wanahabari kujiepusha na uandishi wa habari au vichwa vya habari vinavyohukumu.


“MCT inatambua fika kesi zilizoko mahakamani ni kivutio kwa umma kutaka kujua kinachopendelea ili kuona haki ikitendeka na pia wanahabari wana haki ya kujua na kuripoti yanayojiri huko na katika vyombo vingine vya sheria” alisema Jaji Mihayo na kuongeza:


Wanahabari ni lazima watambue kunataratibu na makubalianao ya kijamii juu ya namna gani taarifa zinavyopaswa kuripotiwa ili kutowadhuru watu wengine.


Katibu Mkuu wa (MCT) Kajubi Mukajanga alisema mwandishi wa habari anauwezo wa kuifanya jamii ikaamini na kumfikilia Lulu moja kwa moja kuwa ndiye aliyemuua Kanumba kitu ambacho si kweli mpaka sasa.


“Kama sasa munaripoti kuwa Kanumba ameuwawa na Lulu lakini baada ya kesi yake kumalizika ikagundulika hakumuua hatuoni atakuwa katika mazingira ya hatari katika mazingira yanayomzunguka” alihoji Mukajanga.


Mukajanga akifafanua kuhusu taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa na mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha Kanumba kuwa zimesabishwa na Lulu alisema MCT  hawahusiki na mitandao hiyo.


“Katiba ya MCT inahusisha vyombo vya habari vya Magazeti,radio na runinga pekee lakini  mitandao ya kijamii inaendeshwa na watu tofauti kutokana na katika ya nchi ya kila mtu kuwa na uhuru wa kupata na kutoa habari bila kujalisha kama anataaluma ya uandishi wa habari” alisema Mukajanga.


Mukajanga alisema kutokana na polisi kutotoa taarifa ya wapi   Lulu alitakiwa kufikishwa mahakamani ili waandishi wa habari wapate nafasi ya kufanya kazi yao alisema atafuatilia kujua nini kilisababiaha kuwepo kwa usiri huo.


“Nitafuatilia na kuchukua hatua sehemu husika ili kujua kwa nini Polisi walifanya siri kumfikisha Lulu katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kuwafanya waandishi kutokudhuria na kuwasababishia usumbufu wa kupata habari kuona ni hatua gani MCT itachukua” alisema Mukajanga.

Wednesday, April 11, 2012

AFRICA MAGIC SWAHILI KUMUOMBOLEZA KANUMBA MWEZI MZIMA.

KITUO cha televisheni cha Africa Magic Swahili kimetangaza kumuomboleza msanii maarufu wa filamu Tanzania Steven Charles Kanumba ambaye alifariki mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuanza kuonyesha filamu za msanii huyo kwa mwezi mzima kutokana na kifo chake ambacho kime washtua mashabiki filamu Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Kama sehemu ya kumbukumbu ya kifo chake kituo hicho kitakuwa kikionyesha sinema zake kuanzia mwishoni mwa wiki hii kama zawadi kwa mchango wake katika tasnia ya filamu Afrika.
Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano na mawasiliano kutoka Multichoice Tanzania Limited Bi Barbara Kambogi alisema kuwa mpango huo utaanza siku ya Jumamosi Aprili 14 saa 19:30 kwa saa za Afrika Mashariki (EAT) ambapo watazamaji wataanza kuangalia filamu ya Uncle JJ, na siku ya Jumapili Aprili 15 muda wa saa 20:00 EAT watangalia filamu ya This is it (sehemu ya 1 na 2).
Alisema kuwa siku ya Jumamosi Aprili 21 saa 19:30 EAT watazamaji wataangali sinema ya More than Pain na siku ya Jumapili Aprili 22 wataangalia filamu ya Young  Billionaire (sehemu ya 1 na 2) ambapo filamu zingine zitaendelea kuonyeshwa siku zinazofuatia.
Marehemu Kanumba akizungumza katika moja ya walsha zilizoandaliwa na Africa magic swahili.
Akimzungumzia Kanumba kutokana na kipaji chake alichokuwa nacho, Mkurugenzi mtendaji wa M-Net Africa Bi Biola Alabi alisema, "Ni lazima tutambue nguvu kijana ambaye amekuwa akifanya vizuri katika tasnia hii. Kifo chake ni hasara kubwa kwa sekta ya burudani Afrika na sisi tunatoa rambirambi zetu kwa familia yake, marafiki na wapendwa wake. "
MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba alifariki dunia siku ya Jumamosi usiku kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.

Lulu apandishwa kizimbani na kusomewa shitaka lake

MSANII Elizabeth Michael (Lulu) Leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashitaka ya mauwaji yanayomkabili dhidi ya Steven Kanumba.
Leo hakutakiwa kujibu lolote, kesi imeahirishwa hadi Aprili 24 mwaka huu, amerudishwa rumade kutokana na kesi za mauaji hazina dhamana. Ungana nasi baadaye kwa habari zaidi.
=============================
Alichoeleza Lulu polisi hiki hapa
Mwandishi Wetu
MSANII Elizabeth Michael (Lulu), ameiambia polisi
kuwa kifo cha Steven Kanumba kimetokana na ugonvi kati yao, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa huenda Lulu akafikishwa mahakamani leo.

Habari zilizopatikana jana kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay zilieleza kuwa, Lulu alisema kuwa kulitokea ugomvi kati yake na Kanumba baada yeye kuzungumza na simu
kutoka kwa mtu maarufu anayetajwa kuwa mpenzi wake.

"Lulu alisema kuwa ugomvi ulitokana na simu aliyopigiwa na mpenzi wake mwingine, ambaye ni mtu maarufu nchini, ndipo
Kanumba akamfokea na ndiyo ugomvi ukaanzia hapo," chanzo hicho kimesema.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa baada ya Kanumba kuanguka, Lulu alitoka nje na kuondoka kwa gari lake hadi maeneo ya Coco Beach, lakini baadaye daktari wa Kanumba alimpigia simu akimtaka arudi ili wampeleke hospitali.

"Alipororudi Sinza ndipo akakamatwa, lakini walikuja Kituo cha Polisi Oysterbay kuchukua PF3," kilisema chanzo hicho.

Chanzo kiliongeza kuwa tangu Lulu alipofikishwa kituoni hapo amekuwa mtulivu asiye na wasiwasi wowote hata katika mahojiano na polisi.

Katika hatua nyingine, Polisi wa kituo hicho jana walipata wakati mgumu baada ya kuibuka kundi la vijana waliotokea makaburi ya Kinondoni kumzika Kanumba, walioandamana wakidai wanamtaka Lulu.

"Tunataka jembe letu", waliimba vijana hao waliofikia 100 wakitokea Barabara ya Ali Hassan Mwinyi huku wakishika majani na kufanya askari waliokuwapo kituoni hapo kuwahi kuchukua silaha na mabomu ya machozi kujiandaa kutuliza ghasia kama zingezuka.

Hata hivyo vijana hao walitawanyika baada ya kuona askari wakiwa tayari kupambana nao na kukimbia maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Patricia Kimelemeta anaripoti kuwa,
Msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu huenda akafikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma za kuhusika na kifo cha Steven Kanumba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela aliliambia gazeti hili jana kuwa Lulu atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mara baada ya polisi kupata ripoti ya vipimo kutoka Mkemea mkuu wa Serikali.

“Tunasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu kubaini chanzo cha kifo hicho kwa sababu wamechukua baadhi ya sampuli za marehemu kwenda kupima na kwamba tutakabidhiwa leo(jana). Kimsingi tukipata tu taarifa hiyo tutamfikisha mahakamani,” alisema Kenyela.

Aliongeza ripoti hiyo itaweza kuwasaidia kuandika mashtaka ili yaweze kufikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kumfikisha mahakamani.

Kamanda Kenyela alisema kuwa, ripoti ya madaktari imewasilishwa juzi na kwamba imeonyesha kuwa Kanumba amefariki kwa ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo.

Msanii Stephen Kanumba alifariki usiku wa Ijumaa Kuu.

Tuesday, April 10, 2012

LIVE KUTOKA LEADERS CLUB KWENYE MAZISHI YA STEVEN KANUMBA


 Wanakwaya wakiimba nyimbo za uzuni.

Hii ndio sehemu ambayo mwili wa marehemu Kanumba unatarajiwa kuwekwa 

 Hawa watoto wanaopita ndio watoto waliokuwa wakicheza movie na marehemu Kanumba enzi ya uhai wake

 Mama yake Kanumba aliyenyoosha mkono juu kuwapungia watu waliokuja uwanjani

 Huyu dada hapa mbele alikuwa akilia kwa uchungu sana hadi nilikuwa namuonea huruma

 Hemed na Yusuph Mlela wakiingia

Makamu wa rais Dk. Mohamed Ghalib Bilali 

 Mke wa rais Mama Salma Kikwete

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akitoa heshima zake za mwisho kwenye mwili wa marehem.

LIVE KUTOKA KINONDONI MAKABURINI KWENYE MAZISHI YA STEVEN KANUMBA


Hii ni barabara ya Kinondoni kuingia kwenye makaburi ya Kinondoni ilikuwa ni balaaaa yani dah, kule mbele ndio mwili wa marehemu Steven Kanumba ndio unakuja

 Kwa wingi wa watu ilibidi watu wapande juu ya miti lakini baadae waliamuriwa washuke chini na kamanda Kova

 Ray akiwa aamini kama swaiba wake ndio anakwenda kwenye nyumba yake ya milele

 Charlz Baba akiwa na wenzake kutoka Mashujaa Band, Charz ameniambia walikuwa wanatokea Morogoro so waliweza kuwahi makaburini

HAPA NDIPO ATAKAPO PUMZIKA MAREHEMU STEVEN CHARLES KANUMBA...!!!


Uwiii Kanumba tunakulilia never to see u again but nina matumaini ile siku parapanda itakapo lia tuakutana tena.
Upumzike kwa amani. Tulikupenda sana lakini Baba Yetu aliye Mbinguni amekupenda zaidi.