BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Sunday, January 20, 2013

Delyla-My Salvation

Saturday, December 29, 2012

Miaka 51 baada ya uhuru wawekezaji wanaongezeka tuu

 Hapa sio Mkoani Simiyu bali ni Dar wawekezaji kibao lakini maisha bado kitendawili... kwa kiasi mji unakua atiii!!!



Tuesday, December 18, 2012

Vodacom Family Day..

 Meneja wa  matangazo wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Bw Nicholas Machugu (Kushoto) akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya wa mpira wa miguu kutoka idara ya biashara kwa nahodha wa timu ya idara ya biashara katika tamasha la Vodacom Family day lililofanyika katika viwanja vya kunduchi Beach Hotel lililofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Waimbaji wa Skylight Band wakitumbuiza katika tamasha la Vodacom Family Day, tamasha lililo fanyika katika viwanja wa Kunduchi Beach Hotel mwishoni mwa wiki.

Monday, December 17, 2012

Wafanyakazi wa Vodacom watoa msaada kwa kituo cha yatima Friend of Don Bosco Kimara

 wafanyakazi wa mtandao wa simu ya mkononi Vodacom Tanzania kitengo cha Customer care wakitoa msaada wa vitu mbali mbali kama vyakula, vitanda, magodoro vyenye thamani ya Sh6 million.

Saturday, November 24, 2012

Msanii wa Filamu Tanzania John Maganga afariki

John Maganga
Marehemu John Maganga mwigizaji wa filamu enzi za uhai wake.
KATIKA Tasnia ya filamu Swahiliwood wiki hii imekubwa na simanzi baada ya wasanii wake kuaga Dunia siku ya jana msanii mahiri wa maigizo Halid Mohamed ‘Mlopelo’ alizikwa na leo hii tasnia hiyo imekubwa na msiba mwingine mkubwa baada ya John Maganga kufariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
John Maganga
Marehemu John Maganga akiwa na msanii mwenzake katika moja ya sene.
John Maganga
Marehemu John Maganga enzi za uhai wake.
Taarifa za awali zinasema kuwa marehemu John amefikwa na mauti baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa tumbo, ni huzuni kwa wasanii na wadau wa tasnia hiyo ya filamu kwani wengi wamedai kuwa msanii huyo ni jana tu walikuwa naye katika matembezi na leo hatunaye tena.
Taarifa zaidi kuhusu mazishi mtazipata hapa hapa bado timu ya FC inajaribu kufuatilia kwa karibu na kuwataarifu, Bwana Mungu alitoa na ametwaha jina lake lihimidiwe.

Friday, October 26, 2012

KITU KIPYA KUTOKA D PRODUCTION "MAGIC MONEY"


""zimebaki sikuchache kuingia sokoni noma...""
ni kauli ya msanii wa filamu Daudi Michael katika wall yake ya facebook akiongelea ujio wa fila mu yake mpya ijulikanayo kama Magic Money iliyoandaliwa na D Production na wasambazaji ni Pili Pili entertainment.... JIPATIE NAKALA YAKO COMING SOOOOON!!!!! BIGUP D PROD....

Sunday, September 2, 2012

TSJ Bash ilivyo wabamba wanafunzi...

 Hao ni washiriki mashindano ya kumtafuta Miss na Mr Tsj kwa mwaka 2012/2013 yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mbalamwezi Beach na hapo wakiwa wanaingia katika steji.
 Wakiwa katika katika steji wakiwa burudisha wanafunzi wenzao kutoka chuo cha uandishi habari kiitwacho Tsj kilichopo Ilala-Sharifu shamba pamoja na Mkuu wao wa chuo cha TSJ akiwa bega kwabega akiongozana na mgeni Rasmi kutoka kitengo cha Haki za kibinaadamu{LHRC}
                                            Washiriki wa MISS na MR TSJ wakiwa katika picha ya pamoja hapo
 Picha ya pamoja wakiwepo washindi wa MISS na MR TSJ kwa mwaka huu, wakiwa pamoja  na mkuu wa chuo upande wa kulia aliyevaa nguo ya rangi nyeupe Bi Carolyne Setumbi kushoto Rais wa serikali ya wanafunzi ya TISJOSO Bi Frida Matinya.
 Picha ya pamoja wakiwepo washindi wa MISS na MR TSJ kwa mwaka huu, wakiwa pamoja  na mkuu wa chuo upande wa kulia aliyevaa nguo ya rangi nyeupe Bi Carolyne Setumbi kushoto Rais wa serikali ya wanafunzi ya TISJOSO Bi Frida Matinya.pamoja na Miss na Mr ambao wamewavalisha Taji washindi wa mwaka huu.

Sunday, August 12, 2012

TAMASHA LA DINI "LOVE TANZANIA" LILIVYOTIA FORA VIWANJA VYA JANGWANI JIJI DAR.


Pichani Juu na Chini ni Umati wa Watanzania uliofurika kwenye Tamasha la Dini lililopewa jina la LOVE TANZANIA linaloendelea katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam likiongozwa na Askofu Andrew Palau kutoka Marekani.
Vijana walioongoza na Askofu Andrew Palau wakitoa burudani na mafundisho ya dini kwa njia muziki.
Wana Dar es Salaam wakiendelea…

Saturday, August 11, 2012

MRITHI WA TAJI LA MISS &MR TSJ KUJULIKANA AUGUST 25 MWAKA HUU





SERIKALI  ya wanafunzi ya chuo cha uandishi wa habari cha Time School of Journalism (TSJ) inatarajia kuwapata wawakilishi wapya wa taji la Miss na Mr TSJ katika sherehe za ‘Bash’  ambazo zimelenga kuwakaribisha wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho.
Sherehe hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi August tarehe 25 zitafanyika katika uwanja wa Mwalamwezi Beach, na itasindikizwa na wasanii mabli mbali wa muziki wa Bongo flava.
Akizungumza na gazeti hili, Rais wa chuo hicho Bi Frida Matinya alisema kuwa sherehe hizo ni moja ya utaratibu waliojiwekea katika kuwapokea wanafunzi wapya ambao ni wameingia chuoni hapo kuchukua kozi mabli mbali.
Alisema kuwa katika sherehe hizo ambazo zitashereheshwa na michezo mbali mbali ikiwa ni pamoja na maonyesho ya mavazi, Mr na Miss TSJ, Kuimba, kuvuta kamba, kuogelea na michezo mingine mingi ya baharini.
“Lengo la sherehe hizo ni kuwa kawaweka karibu wanafunzi wageni na pia kufahamiana pamoja na kujenga mazingira rafiki kwa wanafunzi wote pia kuwapa burudani pia kujijenga kisaikolojia kwani michezo hujenga, kujumuika pamoja katika hafla hii itatuwezesha kuwa na ushirikiano wa kutosha,” alisema.
MWISHO.


TAFF YATOA TAMKO JUU YA MAHARAMIA WA FILAMU TANZANIA

 
SHIRIKISHO la Filamu nchini(TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa filamu na kazi za wasanii ‘wameapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi ya wasanii.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni kero kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.
“Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao”
“Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache ndiyo wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba.
Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.
Alisema Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.
Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubaliana kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo. 
Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwenda kwa haki ili wasanii na kazi zao