BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Tuesday, May 8, 2012

Red Cross yafanya maandamano na kuadhimisha siku ya Red Cross Duniani yenye lengo la kutoa elimu ya matumizi sahihi ya nembo yake.

Baadhi ya wanachama na volunteers wa red Cross wakifanya maandamano jijini Dar leo.
Baadhi ya wanachama na volunteers wa red Cross wakifanya maandamano jijini Dar leo.
Baadhi ya wanachama na volunteers wa red Cross wakifanya maandamano jijini Dar leo.
Baadhi ya wanachama na volunteers wa red Cross wakifanya maandamano jijini Dar leo.
Volunteers wakicheza nyimbo mbali mbali zinazoelezea matumizi sahihi ya nembo.
Wanafunzi wenye ulemavu wa viungo mbali mbali kutoka shule ya Uhuru Mchanganyiko wakiimba nyimbo katika sherehe za siku ya Red Cross Duniani.
 Volunteers wakionyesha matumizi sahihi ya nembo na baadhi ya nembo za chama hicho zinazotumiwa na nchi tofauti tofauti duniani
Baadhi ya wanafunzi wa first aid wakionyehs jinsi Red Cross inavyotoa huduma ya kwanza kwa waliopatwa na ajali.
Baadhi ya wanafunzi wa first aid wakionyehs jinsi Red Cross inavyotoa huduma ya kwanza kwa waliopatwa na ajali.
Mwenyekiti wa Red Cross taifa Dr Zainab Gama akihutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya Red Cross Day.

Sunday, May 6, 2012

Jamani msaidieni huyu muigizaji

   MUIGIZAJI maarufu wa filamu nchini Tanzania, Wastara Juma, amesema kuwa alikataa kuwekwa mapumziko (bed rest) kwa wakati wote wa ujauzito wake kutokana na kumuuguza mume wake Juma Kilowoko maarufu Sajuki ambaye anasumbuliwa na matatizo ya uvimbe tumboni.

Wastara, ambaye hivi sasa ana mtoto mwenye umri wa miezi miwili, anasema matatizo ya afya yake kwa wakati huo ndiyo yaliyosababisha madaktari kutaka alazwe hospitalini.

"Tangu mume wangu alipokuwa anaumwa nilikuwa nahangaika naye huku na kule kumtibia, lakini baadaye nilikuja kugundua kuwa nilikuwa mjamzito. Vipimo vya hospitalini vikaonyesha nina matatizo ya sukari ya mimba, presha pamoja na mguu wangu ulikuwa mbovu," anasema.

Anasema kutokana na ugonjwa wa mume wake, hakutaka kukubaliana na madaktari kuhusu kulazwa kwa kipindi chote atakachokuwa mjamzito na badala yake aliendelea kumuuguza mumewe.

"Nilikataa kulazwa, kwa kweli, japokuwa nilihatarisha maisha yangu, niliendelea kumuuguza na kuhangaika huku na kule, wakati huo mimba nayo ilizidi kukua. Kwa bahati mbaya ilipofikia miezi nane na wiki moja madaktari waliniamuru nifanyiwe oparesheni kwani nisingeweza kuzaa kwa njia ya kawaida, na Machi 5 mwaka huu ndipo nilipompata mtoto wangu," anasema.

Hata hivyo, anabainisha kuwa ilimlazimu kusimama kazi zake zote ili aweze kumuuguza Sajuki.

"Kutokana na ugonjwa wa mume wangu, ilinilazimu kuacha kazi, kuacha kuigiza pamoja na kusimama kwa kazi zangu binafsi ili niweze kupata wasaa wa kumuuguza mume wangu.

"Nilifunga ofisi na vitu vyangu vyote zikiwemo mashine tunazozitumia katika kazi, nilihamishia nyumbani, vitu ambavyo viliibiwa siku moja baada ya mimi kujifungua," anasema.

Changamoto anazokutana nazo Wastara ni kubwa. Anasema kuwa anahitaji zaidi ya Sh 25 milioni pesa za Kitanzania ili kuweza kuokoa maisha ya Sajuki ambaye kwa sasa anatumia dawa zenye thamani ya Dola 1,000 kwa wiki moja alizozinunua nchini India.

"Nahitaji Sh 25 milioni ili Sajuki aweze kupona, kwani kwa sasa anatumia dawa ambazo alizipata nchini India tulizonunua dola 8,000, lakini zikiisha anatakiwa kurudi tena ili akapewe nyingine na matibabu zaidi, sina pesa na vifaa vyangu vyote niliibiwa.�

Anasema na kuongeza: "Tuna maisha ya kawaida kama watu wengine, lakini ninavyoomba msaada watu wananishangaa, kwa kuwa wanatuona tunacheza filamu katika majumba ya kifahari wanadhani ndiyo maisha yetu, siyo hivyo, mimi nafanya hivi ili mume wangu apone.�

Wastara aliweka bayana nambari za akaunti yake ya benki kwa wale wenye mapenzi mema wanaotaka kumsaidia kuwa ni Wastara Juma, Akaunti Namba 050000003047 iliyopo Akiba Commercial Bank.

�Tatizo kubwa zaidi linalomsumbua Sajuki lilikuwa ni kukauka kwa damu ambapo ilifikia hatua anakuwa na damu 5 mpaka 4, hali ambayo ni hatari, lakini nashkuru Mungu kwani ameanza kutumia dawa na kwa sasa ana damu 9,� anaeleza Wastara.

Anasema kuwa, katika maisha yao wamekutana na mitihani mingi ikiwemo yeye kukatwa mguu siku chache kabla ya ndoa yake na kwa sasa kuugua kwa wote wawili kwa wakati mmoja.


Ramsey yuko juu sana


RAMSEY Nouah ametamka hadharani kwamba hakuna jinsi utakavyoitaja fani ya filamu Nigeria uache kumgusa, lakini anafikiria kukaa pembeni kabla hajachuja.

Msanii huyo alisema; "Najua mashabiki wangu watataka kuniona siku zote kwenye runinga, lakini kama ilivyo kawaida, lazima ung'atuke ukiwa bado unapendwa.

Najua nimefanya mambo makubwa sana kwenye hii tasnia, hakuna jinsi utakavyotaja jina Nollywood uache kunitaja."

"Nitakuwa naigiza hapa na pale lakini kidogo sana, nitakuwa nafanya sana mambo ya uongozaji, kuna kipindi kirefu sasa sijaonekana kwenye runinga kwa sababu sitaki kufanya kazi ambazo hazina viwango.

"Sitaki kufanya kazi ilimradi, nataka kuhusishwa na filamu zenye viwango na heshima kwenye hii fani."

Baba azuia mali za Kanumba mahakamani

MZEE Charles Kanumba ambaye ni baba mzazi wa marehemu Steven Kanumba, amezuia kuuzwa kwa mali zilizoachwa na mkali huyo wa filamu nchini.

Mzee Kanumba anataka kitu chochote kisiuzwe mpaka mahakama itakapoamua mrithi wa mali hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa, mzazi huyo alisema kuwa ameamua kutoa tamko hilo baada ya kusikia mzazi mwenzake, Flora Mutegoa, ameanza kuuza mali zilizoachwa na marehemu Kanumba kabla ya mahakama kutoa uamuzi.

Mali hizo ni pamoja na gari la kifahari lenye thamani ya Sh 75 milioni.

�Nimesikitishwa na kitendo cha kusikia mama wa Kanumba ameanza kuuza mali za marehemu, nimeamua kutoa tamko kwa Watanzania wote kuwa wasinunue mali yoyote ya marehemu mpaka mahakama itakapotoa uamuzi," Mzee Kanumba alisema.

"Sisi wazazi wote tuna haki kwa sababu ndiyo tuliomzaa, mtu yeyote atakayenunua mali hiyo atakuwa ametenda kosa la jinai."

Pia alisema ametoa kauli hiyo kufuatia kupata taarifa kuwa kuna wasanii ndiyo madalali wa kuuza mali hizo za Kanumba.

Mzee huyo pia ametoa wito kwa mzazi mwenzake kuacha kusikiliza watu wanaopotosha kuwa kifo cha mtoto wao kilitokana na imani za ushirikina.

�Kuna kijana mmoja ambaye ni mtoto wa dada yangu (anamtaja jina) nimesikia anamdanganya kuwa mtoto wetu karogwa, mara amechukuliwa msukule asimsikilize huyo," aliongeza Mzee Kanumba.
"Tuliwahi kumwita ili kumhoji lakini hakutokea."

Kanumba alfariki dunia Aprili 7 mwaka huu katika kifo kilichozua utata. Msanii Lulu yuko rumande akiendelea na kesi inayomtuhumu kuhusika na kifo hicho.

Wednesday, May 2, 2012

KENYELA AMESEMA ANAFUATILIA BASTOLA ILIYOKUWA IKIMILIKIWA NA KANUMBA

Bastola ambayo inadaiwa ilikuwa ikitumiwa kihalali na staa wa filamu barani Afrika, Steven Charles Kanumba, inasakwa na Jeshi la Polisi Tanzania.Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Charles Kenyela amesema kuwa anafuatilia kumbukumbu za silaha hiyo, kwani haijarejeshwa kwenye jeshi lake.Kenyela alisema juzi kuwa anafuatilia umiliki wa Kanumba juu ya umiliki huo na baada ya hapo, jeshi la polisi litawahoji ndugu“Bastola ni mali ya serikali. Kuna hatua ambazo hufuata mpaka mtu aruhusiwe kumiliki bastola,” alisema Kenyela na kuongeza:Endapo mmiliki halali wa silaha hiyo atafariki dunia, ndugu zake lazima waikabidhi kwa jeshi la polisi na baada ya hapo, kama kuna ndugu anataka aimiliki, inabidi afanye maombi upya na atakapokidhi vigezo ndiyo anaruhusiwa.“Kutokana na hali hiyo, bastola ya Kanumba lazima irudi kwetu haraka na kama kuna ndugu yake yeyote anataka kuimiliki, itabidi awasilishe maombi.”Kenyela aliongeza kuwa hivi sasa anafuatilia kumbukumbu za jeshi la polisi ili awe na uhakika kama kweli msanii huyo alikuwa anamiliki silaha hiyo.“Tukithibitisha tutawahoji ndugu zake pamoja na wengine wanaohusika ili tuwe na taarifa za hiyo silaha. Ila kwa sasa tunafanyia kazi taarifa hizi kwa kupitia kumbukumbu za jeshi,” alisema.Kenyela alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa na ripota wetu kama jeshi lake limeshapokea bastola ambayo alikuwa anaitumia Kanumba enzi za uhai wake.
NDUGU WANASEMAJE?
Mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa, aliulizwa na paparazi wetu kuhusu bastola inayodaiwa kutumiwa na mwanaye alipokuwa hai, na haya ni majibu yake:“Sijaiona hiyo bastola humu ndani tangu nimefika hapa. Sijui ipo wapi na sijui kama kweli Kanumba alikuwa anamiliki hiyo silaha.“Najua sheria za silaha hiyo, kwa hiyo ingekuwepo ningeiwasilisha polisi haraka. Baba yangu alikuwa na silaha hiyo, alipofariki dunia tuliikabidhi kwa jeshi la polisi.”
NANI ANAJUA ILIPO?
Taarifa zinaonesha kuwa mdogo wa Kanumba, Seth Bosco alikuwa karibu zaidi na marehemu lakini kwa sababu umiliki wa silaha hiyo ni siri, siyo rahisi kujua ilipo.Mtu mwingine ambaye alikuwa karibu na marehemu mpaka nyakati za mwisho za uhai wake, kama ripoti zinavyoonesha ni muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, ingawa naye inawezekana akawa hajui kutokana na unyeti wa silaha yenyewe.
BASTOLA NA KANUMBA
Akiwa hai, Kanumba aliwahi kuripotiwa mara kadhaa kumiliki silaha hiyo, japo haikufafanuliwa kama ni kihalali au batili.Kanumba aliripotiwa kwa mara ya kwanza kumiliki bastola miaka minne iliyopita, akidaiwa kuichomoa baada ya kuvamiwa na kundi la watu aliohisi wanataka kumteka.Licha ya stori hiyo kuandikwa gazetini na nyingine ambazo zilimhusisha na umiliki wa bastola, bado Kanumba hakuwahi kufafanua chochote kuhusu silaha hiyo.
IPO WAPI?
1. Je, aliiacha sehemu ambayo hakuna mtu ameweza kupafikia?
2. Aliirejesha kabla mauti hayajamkuta ndiyo maana haionekani?
3. Je, Kuna mtu aliiwahi baada ya kifo chake akiona ni dili?
Kanumba alifariki dunia Aprili 7 na kuzikwa Aprili 10, 2012 kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. wa msanii huyo kuhusu kurejesha bastola hiyo jeshini.
Martin Lukanga
Tin White.
MCHEKESHAJI mahiri wa vichekesho Swahiliwood Martin Lukanga ‘ Tin White’ ameamua kuachana na komedi za kushirikishwa bali ni kuandaa komedi zake mwenyewe kama ambavyo ufanya wasanii wenzake na kuuza kwa wasambazaji, akiongea na Jukwaa la filamu Tin White amesema ameshiriki Komedi nyingi lakini hapati nafasi nzuri ya kuwakilisha mawazo yake.
“Nimetumwa sana na mimi zamu yangu kuwatuma vijana wangu nimetayarisha Komedi yangu kali inayokwenda kwa jina la Mr. Lover ni hadthi nzuri ina mtiririko mzuri kama zilivyo filamu, ni komedi ya kipekee mtu anacheka humo kwa ajili ya hadithi na si vinginevyo, nimeanza na spidi yangu haina mwisho,”anasema Tin White.
Kama ilivyo tabia ya wachekeshaji ya kujikusanya na kushiriki kwa wingi katika filamu moja na humu namo wapo wachekeshaji kama Bambo, Kingwendu, Ringo, Tin White mwenyewe, Mtanga, alipoulizwa kwani nini wachekeshaji wengi ujazana katika filamu moja alisema kuwa si wao bali ni fikra finyu za wasambazaji wanaamini
kuwa wachekeshaji wengi ndio kuuza, lakini yeye anaamini kuwa hata msanii mmoja tu anatosha.

CLOUD KATIKA HARAKATI ZA UZINDUZI WA TOBA

 Cloud.
MWIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Issa Mussa ‘Cloud 112’ yupo katika maandalizi ya kuzindua filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Toba uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Salama uliopo Zanzibar tarehe 18/05/2012 siku ya Ijumaa.
Cloud anakuwa ni msanii wa kwanza kwa mwaka huu kufanya tamasha kwa ajili ya uzinduzi wa filamu yake hiyo ya Toba baada ya utaratibu huo kusimama kwa muda mrefu kidogo, kwani siku hizi filamu zikitengenezwa zinaingizwa sokoni moja kwa moja bila kufanyiwa uzinduzi.
Filamu ya Toba imeshirikisha wasanii nyota kama Suleiman Barafu, chiki, Sandra, Eshe, Bi. Hindu na wasanii wengine wakali katika tasnia ya filamu Swahiliwood hongera kwa Cloud 112 kwa kufanya uzinduzi wa filamu yake