BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Saturday, March 16, 2013

TSJ yang'ara mashindano ya Utangazaji 2013




Frank Aman, Mwananchi
Dar es Salaam. Chuo cha uandishi wa habari cha Time School of Journalism (TSJ) kibeibuka kidedea kwa kupata alama za juu katika vipingele vyote katika mashindano ya utangazaji yaliyohusisha vyuo vya uandishi wa habari yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Vipengele ambavyo vilikipatia ushindi chuo hicho ikiwa ni mara ya pili kupata ushindi huo tangu mashindano hayo yaanzishwe mwaka 2011 vilikuwa ni pamoja na uchambuzi wa magazeti, Kusoma taarifa ya habari, kuendesha vipindi maalum, Michezo pamoja na vipindi vya burudani.
Akizungumza mara ya baada ya kutangazwa washindi, Rais wa chuo hicho Bi Frida Matinya alisema kuwa licha ya maandalizi ya muda mfupi kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao ushindi huo umepatikana kutokana na mafunzo waliyoyapata chuoni hapo pamoja na vipaji vya wanafunzi walioshiriki katika mashidano hayo.
Alisema kuwa asilimia kubwa ya washiriki katika shidano hilo walio wakilisha chuo hicho wengi wao walikuwa ni wanafunzi walioingia muhula wa kwanza mwaka huu hivyo hali hiyo imedhihilisha vipaji na uwezo wa wanafunzi binafsi.
“Toka kuanza kwa shindano hili mara zote tumeibika kidedea kwani mwaka 2011 lilipoanza shindano hili ambalo lilifanyika katika chuo cha uandishi wa habari cha Royal College of Tanzania (RCT) tulikuwa washindi wa kwanza, mwaka jana yalifanyika chuo cha uandishi wa habari cha Mlimani eneo la Mbezi tulikuwa washindi wa pili,” alisema na kuongeza;
“Hii pekee imedhihilisha kuwa kuwa wanafunzi wa chuo hiki wana uwezo mkubwa katika fani ya utangazaji na pia taaluma inayotolewa katika chuo chetu inakidhi vigezo vya sisi kuingia katika ushindani wa aina yoyote hata katika ngazi ya ajira.”

Bi Matinya alisema kuwa katika shindano hilo chuo cha RCT kimekuchukua nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikishikwa na chuo cha Dar es Salaam City College (DACISO).
Mashindano hayo yalifanyika katika viwanja vya TSJ maeneo ya Ilala Sharifu Shamba yalijumisha idadi ya vyuo sita (6) lakini vyuo ambavyo vilishiriki jana katika kinyang’anyiro hicho ni vitatu ambavyo ni RCT, DACICO pamoja na TSJ.

Wakiongee na Mwananchi baadhi ya wanafunzi wa Tsj walisema “ sisi ndio sisi ushindi kwetu daima kwani tulijiandaa vya kutosha japokuwa muda tuliyofanya mazoezi ni mdogo mno ila tumestahiki kuwa washindi wa nafasi ya kwanza”
MWISHO.

No comments:

Post a Comment