BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Thursday, July 14, 2011

JB "IMANI YANGU NA KAZI UTATA"

UNAPOTAJA majina ya wasanii wakongwe wa filamu nchini,  huwezi kuacha jina la Jacob Stephen maarufu kama JB au Erick Ford. Huyu ni msanii aliyejizopatia umaarufu katika tasnia hiyo.
Unakumbuka kikundi cha Mambo hayo? Bila shaka utaafiki kuwa ni miongoni mwa vikundi vya maigizo vilivyowika na kuvuta hisia za wengi katika miaka ya 1990. JB ni mmoja wa waliounda kikundi hicho, ana umri wa mika 13 katika fani.
Kazi inayofanywa na JB si rahisi kwa maana inamlazimu kuishi kambini kwa siyo chini ya miezi sita katika mwaka na ni mume wa mtu pia ameokoka.
“Kwa sababu ninamiliki kampuni ya kutengeneza filamu, ninaongoza na kucheza filamu nakosa muda wa kulala nyumbani kwangu, katika mwaka mmoja nagawanya miezi sita kambini na miezi sita nalala kitandani kwangu,” nasema JB na kuongeza;
“Mimi ni mtumishi wa Mungu kazi yangu inanilazimisha kuingia sehemu mbalimbali ambazo hazistahili kwa mtu aliyeokoka wakati huo huo napaswa nielimishe jamii hii ni changamoto kubwa sana kwangu,”.
Anasema, wakati mwengine jamii inashindwa kumuelewa kwa sababu anaingia katika majumba ya starehe na kwamba muda wa kushiriki mambo mbalimbali na jamii yake au ndugu anakosa.
“Hata majirani ninaoishi nao siwafahamu, misiba au vikao vya ndugu nashindwa kuvimudu kutokana na kazi hii, namshukuru Mungu kwa sababu naamini kuwepo kwangu jukwaani ninapowakilisha ujumbe kwa jamii ni mchango wango mkubwa katika kushirikiana nao mambo mengi,” anasema.
JB anasema, anatarajia kuifanya kampuni ya Jerusalemu Filims kuwa ya kimataifa na kwamba atajikita katika kucheza filamu za burudani lengo likiwa ni kuwafurahisha watu baada ya kuchoka katika mizunguko ya simu nzima.
“Kama nilivyotangaza kuwa sitafanya filamu nje ya kampuni yangu nitaendelea kuboresha kampuni yangu na ninatarajia kuifanya kuwa ya kimataifa na kwa kuanza nitatengeneza nembo itakayoitambulisha hata sehemu yeyote ukiniona,”alisema.
Anasema, atabadilisha mfumo wa filamu katika kampuni hiyo na kuwa za kuburudisha ili aweze kuwaburudisha mashabiki wake na kwamba atalitaka soko la filamu kwa kiwango kikubwa.
“Ninacholenga nikuwarejezea watu mawazo mapya wanapokuwa wamechoka katika mizunguko ya kazi lakini pia kuinua vipaji vya wasanii wengi na tayari hilo nimelianza katika filamu ninazoziandaa zimetawaliwa na wasanii chipkizi,” alisema.
JB anasema, matarajio yake hayo ni kuwa msanii wa mfano wa kuigwa nchini kama ilivyo kwa msanii mashughuri wa Nigeria  Amitabh Bachchan na Bollywood.
Akizungumzia kukua kwa tasinia ya filamu nchini JB anasema Tanzania inashika nafasi ya tatu kati ya nchi tano za Afrika Mashariki na kwamba kinachochelewesha tasinia hiyo kukua ni kuchelwa kuanza kwa sanaa nchini.
“Maendeleo ya filamu yapo tatizo kuwambwa linaliifanya iwe nyuma ni kuchelewa kuanza kwa sanaa hiyo lakini tukikaza buti na kushirikiana tunaweza kufika mbali zaidi,” anasema na kuongeza:
“Filamu ya Tanzania imeanza kukua mwaka 2009 wenzetu walianza zamani na wanaelimu wanapata ushirikiano kwa jamii yao hivyo lazima waonekane wamepanua wigo wa sanaa kwa kiwango kikubwa,”.
JB anasema, wasanii wachanga wanaharaka na uigizaji, hawajichunguzi kama wanauwezo na kwamba uigizaji ni zawadi kutoka kwa Mungu.

“Usanii sio rahisi kama unavyofikiria hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, sio kila mtu anaweza na kupenda sio sababu ya wewe kuweza kuigiza kinachotakiwa ni kujichunguza kama anaweza na baadaye aanza kwa kufuata utaratibu wa sanaa,” aliasema.
Anasema wasanii wengi wanaharaka ya kupata mafanikio na kuwa wanasahau kuwa kila kitu ambacho ni mpango wa Mungu kinapaswa uende taratibu.
JB (40) ambaye alifanya bishara ya mahindi katika kipindi cha miaka 10 kabla hajaanza kazi ya sanaa anasema, amefanikiwa kwa kiasi na kwamba anamiliki kampuni yake ya filamu na maduka mawili ya nguo.”
Anasema anachojivunia katika maisha yake ni wokovu na tuzo ya ymsanii bora wa kiume aliyoipata mwaka 2009 na kwamba ni msanii anayeheshimiwa na kupendwa na kila mtu.
“Katika maisha yangu ya usanii sijawahi kuwa na skendo chafu, napendwa na watu wa kila aina kutokana na ucheshi wangu nilionao, yote hii ni kwa sababu Mungu anasimamia maisha na kazi zangu pia.
JB alifanikiwa kuchukua mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mwaka 1992 ingawa hakuweza kuajiriwa, ni mzali, elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya St Joseph, kidato cha kwanza hadi cha sita aliipata katika shule ya Popatlal.

CATHY AAHIDI KUWAELIMISHA WANAWAKE..

MCHEZA sinema wa bongo, Sabrina Rupia (Cathy) amesema atahakikisha anawaelimisha wananawake kuhusu kujitambua ili wafanye kazi kwa bidii na kuondokana na utegemezi.
Cathy ambaye anazaidi ya miaka 13 katika sanaa anasema wanawake wengi wamekata tamaa ya maisha kutokana na kuachwa na waume zao hali inayosababisha kuwepo na wimbi kubwa la watoto wa mitaani.

Anasema, kutokana na hali yake ya kuwa mwanamke mtafutaji katika maisha, ameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kutoa ajira kwa watu wengi zaidi.
“Katika maisha yangu naumizwa sana na ninapowaona watoto wanaombaomba barabarani na kukosa haki zao za msingi kama shule, natamani kuwaelimisha wanawake walioachwa na waome zao juu ya kujitambua ili wafanye kazi kwa bidii,” anasema.

Saturday, July 9, 2011

RIYAMA AWAPONDA WASANII WANAOKAA UCHI...


Nyota wa filamu na mshindi wa zamani wa Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike nchini, Riyama Ally a.k.a Riyama amewataka wasanii wenzake kuacha tabia alizoziita za kijinga kwa kuiga maisha na uigizaji wa wasanii wa ng’ambo.

Riyama ambaye sifa yake kubwa kwenye ‘game’ ni kuvaa uhusika, hasa wa kumwaga machozi, alisema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalum na gazeti hili jijini Dar es Salaam.



“Usanii si kukaa uchi, unajua baadhi ya wasanii wenzetu wanashindwa kufahamu hilo. Kukaa uchi hakumaanishi ndiyo utaonekana mzuri zaidi,” alisema kwa masikitiko Riyama.

Akizidi kushusha ‘maskadi’ Riyama alisema, tatizo kubwa walilonalo wasanii wa Kibongo ni kuiga, mwenyewe anafafanua: “Haijakatazwa kuiga, lakini unatakiwa kujua unaiga nini. Hatuwezi kuchukua tamaduni za watu na kuleta kwetu. Wao wana miiko yao, nasi pia. Kwanini tuige ujinga?”

Alisema, wasanii kuvaa nguo fupi zisizo na heshima, huua soko la filamu bila la wasanii wenyewe kujua kwani watu wenye heshima zao hawawezi kununua na kwenda nazo majumbani mwao.


Kwa muda mrefu sasa, magazeti Pendwa yamekuwa yakiandika habari kuhusu kero za wasanii kuvaa nguo fupi ambazo zinaacha sehemu za miili yao wazi, lakini wenyewe wamekuwa wakiweka pamba masikioni.

kutoka kwa wadau Global publisher

SYLIVIA ASHINDA TAJI LA UREMBO...


Mwanadada Mrembo Sylivia Nduka amabaye pia ni mwanafunzi anayesomea accountancy undergraduate kutoka Anambra State ameibuka mshindi katika shindano la Most Beautiful Girl In Nigeria 2011.

Mbali na Taji hilo alilopata pia Sylivia amejishindia kitita cha milioni 3 fedha za Kinaigeria pamoja na gari aina ya Hyundai.


Shindano hili la kuwasaka wrembo wenye mvuto nchini humo hufanyika kila mwaka na mwaka huu mdada huyo kaondoka na zawadi hizo nono.


Mashindano ya Most Beautiful Girl in Nigeria (MBGN) yalifanyika June 25, 2011 na mwana dada huyu ndie aliyemrithi mshindi wa mwaka jana aliyekuwa Fiona Aforma shindano hilo lilifanyika katika maeneo ya Eko Hotels and Suites, Victoria Island, Lagos.

KATE APANGA KUSHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE ISIVYO KAWAIDA...

Msanii wa kike wa filamu nchini Nigeria Kate Henshaw Nuttal amepanga kusherekea birthday yake kwa gharama za juu na itakuwa sherehe ambayo haijawhi kutokea..
Akizungumza na waandidhi nchini humo amesema kuwa atakuwa anatimiza umri wa miaka 40 itakapo fikia tarehe 19 july mwaka huu.

Mbali  na kufikia umri huo pia atakuwa anasherekea anniversary ya ndoa yake iliyodumu kwa miaka 10 sasa..

Kama wadau wa fani hii tunampa pongezi dada huyu kwa kufikisha umri huu na pia miaka yote hyo katika ndoa..

Wednesday, July 6, 2011

MABINTI WANAOKUJA JUU KATIKA TASNIA YA FILAMU BONGO...

Hawa ni wale chipukizi wa kike wa filamu wanaowaumiza vichwa wakongwe na kazi zao nyingi zinafanya vizuri ukiachilia mbali urembo wa sura zao.

JENNIFER DAUDI


Ni muigizaji chipukizi ambaye ameweza kucheza filamu mbili ambazo ni 'This is it' na 'Uncle JJ' za Kanumba na kuweza kupata tuzo ya ZIFF akiwa kama muigizaji bora chipukizi kwa 2010.


HERIETH.

Ukitazama filamu ya 'Seasons Of love' hapo ndipo utakapoona kipaji cha mwanadada huyo ambaye anatumia umbo lake katika kupendezesha kazi na ndiyo maana yupo katika nyota chipukizi wanaofanya vizuri.


SALOME.

Jina halisi la chipukizi huyo ni Sabrina Omary, lakini mashabiki wake wanamfahamu kama 'Salome', ukitazama kazi ya 'Red Valentine' basi utaweza kuona kipaji cha msanii huyo.


Msanii huyo ameweza kuonesha uwezo wake katika filamu kadhaa kama vile The Romantic na The Justice, Zuadiswa, Honeymom, Ukiwa na One by one.

ESTHER FLAVIAN.


Ni nyota ambaye kipaji chake kilianza kuonekana katika filamu ya 'Nyabo', ikiwa na maana ya 'mrembo', lakini baada ya kazi hiyo uwezo wake ukaonekana zaidi na ndipo alipocheza kazi nyingine kama Mrembo, Is too late, Zawadi ya Oparesheni, Mrs Zinduna, Where is Love, Aunty Suzy, No way out na nyingine nyingi.


FLORA MVUNGI.


Kama ni mfuatiliaji wa michezo mbalimbali ya televisheni basi jina la nyota huyo si geni kwako kwa sababu aliwahi kutamba na mchezo wa 'Bongo Dar es Salaam' uliokuwa ukirushwa na kituo cha TBC1.

Kipaji chake kiliweza kuonekana katika mchezo huo na hadi kucheza filamu iliyokwenda kwa jina la 'September 11'.

LISA JENSEN.


Ni mwanadada anayeshiriki katika matamasha mbalimbali ya urembo lakini kipaji chake cha filamu unaweza kukiona katika kazi kama More than Pain, Full moon, Fake Pastors na nyingine ambazo zote zinamuweka katika chipukizi wanaokuja juu.

SHIRLEY.

Jina halisi la chipukizi huyo ni Celina Victor, lakini mashabiki wa filamu wanamfahamu kwa 'Shirley', msanii ambaye aliweza kuonesha uwezo katika tamthilia ya 'Jumba la Dhahabu'.

Nyota huyo anajitahidi kusaka umaarufu lakini bado anachangamoto nyingi za kucheza filamu ambazo zitazidi kumweka juu kama ilivyo kwa The Sandy kazi ambayo inafanya vizuri.

SHILOLE.


Jina halisi la nyota huyo ambaye kwa sasa anakuja juu ni Zena Mohamed Yusuf 'Shilole', kiwango chake kinaonekana katika filamu kama Fair Decision, akiwa na nyota kama 'Ray', Johari ‘Crazy Of Love’, ‘Pigo’, ‘Bed Rest’ na ‘Cut Off’ kazi ambazo hadi sasa zinaanza kumtoa katika uchipukizi kutokana na uwezo wake.



NAJMA.

Ni muigizaji mahiri katika tasnia hii na jina lake halisi ni Najma Suleiman, ni msanii ambaye hana makuu kwa sababu anajua nini anachokitafuta hasa katika tasnia hii.

JENGUA AAMUA KURUDI TENA SASA...

Msanii wa filamu ambaye alijipatia umaarufu kupitia kundi la Chemchem Arts Group maarufu kama Kidedea, amesema anarudi tena kwa kasi katika mtindo mwingine wa filamu. anasema kwa hivi sasa anatoka na filamu mpya inayokwenda kwa jina la Gamba la nje.
alisema kwa sasa yupo chini ya meneja mpya Abdull Makarama ambaye ndiye mwenye kundi la Mkarama Group analoofanyia kazi yeye

Tuesday, July 5, 2011

MSANII WA NIGERIA AVAMIWA NA MAJAMBAZI

Habari kutoka katika vyanzo vya habari mbali mbali nchini Nigeria vinaeleza kuwa mwigizaji wa kike Hassanat Taiwo Akinwande wa Yoruba maarufu kama Wunmi alivamiwa na majambazi na kuporwa hivi karibuni siku ya Jumapili, Julai 3, 2011 katika makazi yake maeneo ya  Ijede, Ikorodu Lagos.


Kulingana na vyanzo hivyo, wezi hao walivunja nyumba yake saa 10:45 na kuiba vitu mbali mbali pamoja fedha na vitu vya thamani visivyojulikana.

Wakati wa uvamizi huo, ambayo ulidumu kwa saa kadhaa, wakazi wa mji huo ambao wanaishi maeneo ya karibu na nyota huyo hawa kuweza kutoa ushirikiano wala kusaidia.

sio tuu kuiba vitu hivyo pia waliweza kumjeruhi kwa kiasi kidogo staa huyo wa Nigeria.