Kampuni ya 1plus Communication kwa kushirikiana na European Union watateremsha Bongo tamasha kubwa la filamu litakalokwenda kwa jina la European Film Festival ‘EFF’ ambalo limekuwa likichukua nafasi barani Ulaya.
Akiongea na Ijumaa juzi msemaji wa ‘event’ hiyo, Tayana Amri (pichani) alisema kuwa, jumla ya mataifa 15 ya bara la Ulaya yatashiriki huku Bongo ikiwa mwenyeji wao.
“Ni tamasha litakaloanza tarehe 14 mwezi huu mpaka Novemba 7 ndani ya New World Cinema, kwa siku za kawaida na litachukua nafasi kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja siku za wikiendi kupitia ‘Screen’ kubwa zitakazofungwa hapo,” alisema Tayana.
Katika hatua nyingine afisa huyo wa Kampuni ya 1plus, alianika kuwa, kwa kila siku katika maonesho ya filamu hizo kila taifa shiriki litakuwa na nafasi ya kuonesha filamu tatu tofauti.
Aidha, Tayana aliweka wazi kuwa kwa Jiji la Bongo tamasha hilo litaruka kwa wiki tatu kabla ya kuhamia Arusha ambako litang’aa kwa wiki moja.
No comments:
Post a Comment