BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Friday, October 8, 2010

Yvonne Cheryl `Monalisa' apania kufanya kazi zenye ubora zaidi.’.

LICHA ya kuwapo kwa nyota wengi katika fani ya filamu nchini, Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) linalofanyika kila mwaka kisiwani humo, limeweka wazi kwamba, hakuna kama Yvonne Cheryl `Monalisa’ linapokuja suala la filamu za Kiswahili Tanzania.
 .

Alitangazwa kuwa bora Julai mwaka huu, baada ya kung’ara katika filamu ya Black Sunday iliyobeba jina la `Kizungu’.

Katika mazungumzo yaliyozaa makala haya, Monalisa mwenye utajiri wa vipaji kuanzia vya uigizaji, utangazaji na hata uimbaji, alisema kwamba baada ya kupata tuzo ya ZIFF, imemwongezea kujiamini na sasa amepania kuongeza bidii na kufanya kazi za sanaa zenye ubora zaidi, akitolea mfano wa filamu yake binafsi ya Binti Nusa.

Mungu akinipa afya na uhai, kamwe sitawaangusha mashabiki wangu na Watanzania kwa ujumla. Nimepania kuitangaza Tanzania kupitia filamu kwa kufanya kazi bora ambazo nashirikiana na wasanii wa nchi mbalimbali wa ndani na nje ya Afrika,” anasema.

Anasisitiza kwamba, ameamua kuachana na fani zake nyingine ili aweze kujikita katika sanaa kwa lengo la kutengeneza filamu ambazo zitaingia katika ushindani wa soko la kimataifa.

Anazungumza kama utani, lakini kwa wanaomfahamu Monalisa, watakubaliana na ukweli kwamba, ni msanii mwenye kipaji, anayejua anachokifanya na mwenye kujituma.

Huyu ni miongoni mwa wasanii maarufu walioibuka na mwishoni mwa miaka ya 1990, akiwa na kikundi cha Mambo Hayo kilichokuwa kinarusha michezo yake kupitia kituo cha televisheni cha ITV.

No comments:

Post a Comment