BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Tuesday, November 16, 2010

Binti Nusa sehemu ya pili imekamilika


Binti Nusa sehemu ya pili imekamilika na ipo tayari kwa ajili ya kuingia sokoni kwa ajili ya mauzo, filamu inakuja baada ya Binti Nusa nambari moja kufanya vizuri katika tasnia hii na kuwashika watazamaji ambao walikuwa na kiu ya kujua binti huyu anayesadikiwa kuwa ni muuaji na anatafutwa na polisi atapatwa na nini?

Katika sehemu ya kwanza katika filamu hii ya Binti Nusa ‘Monalisa’ kacheza kama binti kutoka kijijini kuja kwa mjomba wake na kukutana na mauaji ya familia yake yote na yeye kunusurika na kukimbilia katika nyumba ya kulala wageni. Dereva Taksi anafanya mpango kumuibia fedha zake alizochukua kwa mjomba wake na akiwa hotelini anampata Bosi anayempenda na bosi huyu anataka awe mpenzi wake, na huyu ni afisa wa polisi. Shughuli ipo hapo!!!!

Akiongea na Fc mtayarishaji wa filamu hii Yvonne Cherryl aka Monalisa amesema kuwa
“Filamu hii imekamilika kuanzia uhariri na kila kitu kimeenda sawa, na nilikuwa na kazi ngumu sana kwani sikutaka nipoteze ladha ya Binti Nusa ya kwanza, katika kulinda ubora wa filamu ya kwanza imenibidi kwa kila hatua ninayofikia niwe makini kwa ajili ya kusonga mbele na kutoa kitu bora zaidi”
Aidha filamu hiyo ambayo inasemekana baada ya kuhaririwa ilipekwa Nchini Kenya na kuangaliwa na watalamu wa mambo ya filamu nchini humo na tayari wamefanya kazi yao na baada ya kuikubali imeletwa kwa ajili kuisambaza hapa nchini.
Filamu hii imeshirikisha wasanii nyota wa filamu hapa nchini kama Hashimu Kambi, Susan Lewis, Vanita Omary, Yvonne Cherryl, pamoja na Keneth Ambari aka Baraza.

No comments:

Post a Comment