BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Sunday, December 4, 2011

MABINTI WANAOTETEMESHA VIDUME NOLLYWOOD..

MERCY Johnson ameshaolewa. Nani anafuata? Ndiyo swali wanalojiuliza mashabiki wa filamu za Nollywood, asilimia kubwa ya wasanii wa kike hawajaolewa na wengine hawana hata mpango na hayo mambo.
Wengine walishaolewa wakaachika kutokana na kuendekeza starehe na kushindwa kutulia kwenye ndoa zao. Hii ni orodha ya mabinti ambao hawajaolewa na wanaotetemesha wanaume Nollywood. 

Funke Akindele
Huyu binti ana mafanikio makubwa kikazi na ni miongoni mwa wasanii wanaolipwa sana. Ana umri wa miaka 35, hana skendo nyingi za mapenzi kama walivyo mastaa wengine wa Nollywood.
Yuko kwenye uhusiano wa kudumu na huenda muda wowote akatamka jambo kwa marafiki zake.
Amesomea sheria kwenye Chuo Kikuu cha Lagos. Baadhi ya filamu alizowahi kufanya ni kama Jenifa, Omo Ghetto na Return of Jenifa Part 2. 

Rita Dominic
Sura na umbo lake vinadanganya watu wengi sana, ukimwangalia kwa haraka unaweza kudhani ana umri wa miaka 25, lakini kwa taarifa yako ana miaka 37 sasa na bado pia yumo kwenye kundi hilo la mabachela.
Mambo yake ya uhusiano wa zamani hayajafunuliwa sana lakini aliwahi kuwa na uhusiano na msanii mwenzie, Jim Iyke, hususani alipokuwa anaishi maeneo ya Wemabod Estates, Ikeja. 

Genevieve Nnaji
Miaka yake ni 32 na anatafsiriwa kama nembo ya filamu za Nollywood Afrika na Dunia nzima. Ni miongoni mwa mabinti matajiri Nigeria, lakini bado hajabahatika kufanya maamuzi magumu ya kuachana na ubachela.
Ana mtoto mmoja wa kike na awali alishavumishwa kuwa na uhusiano na Makamu wa Rais wa zamani wa Nigeria, Abubakar Atiku. 

Chika Ike
Ni mzuri na ana mvuto. Aliolewa lakini baada ya muda akaachika kwa sababu ambazo marafiki zake wa karibu waliziita za kitoto na ni binti wa kuendekeza sana starehe. Amenunua Range Rover ya kisasa na amefungua saluni za kisasa jijini Abuja, kama ni fedha anayo. 

Uche Jombo
Anawatoa udenda wengi. Lakini rafiki yake wa karibu amedokeza kwamba huyu binti hana mpango wa kuolewa sasa hivi, akili yake imekaa kibiashara zaidi. Anatengeneza fedha sana na anajua kuzitumia.
Anaishi maeneo ya Lekki jijini Lagos. Ametamba na filamu kama Secret Fantasy, Endless Lies, Kiss and Tell, Silent Scandal na Home in Exile. Miaka yake ni 32 na ni msomi wa Chuo Kikuu cha Calabar, Nigeria. Aliwahi kuwa na uhusiano na Ikechukwu Uche ambaye ni mchezaji. 

Monalisa Chinda
Ni bachela mzoefu. Aliolewa akazaa mtoto mmoja maisha yakamshinda akaamua kurudi kwao na sasa maisha yanaendelea kwa staili ya kujirusha kwa wingi.
Mwanaume waliyeachana naye ameshaoa lakini Monalisa bado yupo yupo ingawa inaelezwa wanaume wengi sana wanamnyemelea. Amesomea sanaa kwenye Chuo Kikuu cha Port Harcourt kwao Nigeria. 

Stephanie Okereke
Kila kukicha ana skendo na sura yake haikosekani kwenye kurasa za mbele za magazeti ya udaku. Kwenye masuala ya urefu na uzuri kote amesheheni.
Alishawahi kuolewa pia akaachika sasa hivi yuko kwenye penzi zito na jamaa mmoja anaitwa Linus Idahosa. Hakuna anayejua ni lini wana mpango wa kuoana.

No comments:

Post a Comment