BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Wednesday, July 6, 2011

MABINTI WANAOKUJA JUU KATIKA TASNIA YA FILAMU BONGO...

Hawa ni wale chipukizi wa kike wa filamu wanaowaumiza vichwa wakongwe na kazi zao nyingi zinafanya vizuri ukiachilia mbali urembo wa sura zao.

JENNIFER DAUDI


Ni muigizaji chipukizi ambaye ameweza kucheza filamu mbili ambazo ni 'This is it' na 'Uncle JJ' za Kanumba na kuweza kupata tuzo ya ZIFF akiwa kama muigizaji bora chipukizi kwa 2010.


HERIETH.

Ukitazama filamu ya 'Seasons Of love' hapo ndipo utakapoona kipaji cha mwanadada huyo ambaye anatumia umbo lake katika kupendezesha kazi na ndiyo maana yupo katika nyota chipukizi wanaofanya vizuri.


SALOME.

Jina halisi la chipukizi huyo ni Sabrina Omary, lakini mashabiki wake wanamfahamu kama 'Salome', ukitazama kazi ya 'Red Valentine' basi utaweza kuona kipaji cha msanii huyo.


Msanii huyo ameweza kuonesha uwezo wake katika filamu kadhaa kama vile The Romantic na The Justice, Zuadiswa, Honeymom, Ukiwa na One by one.

ESTHER FLAVIAN.


Ni nyota ambaye kipaji chake kilianza kuonekana katika filamu ya 'Nyabo', ikiwa na maana ya 'mrembo', lakini baada ya kazi hiyo uwezo wake ukaonekana zaidi na ndipo alipocheza kazi nyingine kama Mrembo, Is too late, Zawadi ya Oparesheni, Mrs Zinduna, Where is Love, Aunty Suzy, No way out na nyingine nyingi.


FLORA MVUNGI.


Kama ni mfuatiliaji wa michezo mbalimbali ya televisheni basi jina la nyota huyo si geni kwako kwa sababu aliwahi kutamba na mchezo wa 'Bongo Dar es Salaam' uliokuwa ukirushwa na kituo cha TBC1.

Kipaji chake kiliweza kuonekana katika mchezo huo na hadi kucheza filamu iliyokwenda kwa jina la 'September 11'.

LISA JENSEN.


Ni mwanadada anayeshiriki katika matamasha mbalimbali ya urembo lakini kipaji chake cha filamu unaweza kukiona katika kazi kama More than Pain, Full moon, Fake Pastors na nyingine ambazo zote zinamuweka katika chipukizi wanaokuja juu.

SHIRLEY.

Jina halisi la chipukizi huyo ni Celina Victor, lakini mashabiki wa filamu wanamfahamu kwa 'Shirley', msanii ambaye aliweza kuonesha uwezo katika tamthilia ya 'Jumba la Dhahabu'.

Nyota huyo anajitahidi kusaka umaarufu lakini bado anachangamoto nyingi za kucheza filamu ambazo zitazidi kumweka juu kama ilivyo kwa The Sandy kazi ambayo inafanya vizuri.

SHILOLE.


Jina halisi la nyota huyo ambaye kwa sasa anakuja juu ni Zena Mohamed Yusuf 'Shilole', kiwango chake kinaonekana katika filamu kama Fair Decision, akiwa na nyota kama 'Ray', Johari ‘Crazy Of Love’, ‘Pigo’, ‘Bed Rest’ na ‘Cut Off’ kazi ambazo hadi sasa zinaanza kumtoa katika uchipukizi kutokana na uwezo wake.



NAJMA.

Ni muigizaji mahiri katika tasnia hii na jina lake halisi ni Najma Suleiman, ni msanii ambaye hana makuu kwa sababu anajua nini anachokitafuta hasa katika tasnia hii.

No comments:

Post a Comment