BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Sunday, August 29, 2010

"CRAZY LOVE" KUTOKA KWA KANUMBA THE GREAT

 
Miongoni mwa mambo ambayo yanatia moyo nchini kwetu ni pamoja na kuendelea kukua kwa tasnia ya filamu kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia. Ukuaji huo unakwenda sambamba na kuona kwamba,siku baada ya siku, wapenzi wa filamu za “nyumbani” wanazidi kuongezeka na kwa maana hiyo industry nzima ya filamu inazidi kukua.
Lakini uungwaji mkono huo haukuja bure tu. Umetokana na tabia nzuri ambayo wasanii wengi wa sanaa hiyo wameionyesha.Wamekubali kukosolewa na kusikiliza maoni ya wadau mbalimbali wa masuala ya filamu na kuyafanyia kazi ipasavyo.

KANUMBA THE GREAT
 
Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Steven Kanumba ambaye bila shaka sote tunakubaliana kwamba kila kukicha ameonyesha kuwa na bidii kubwa kabisa katika kuboresha kazi zake na uigizaji wake kwa ujumla.
Mwezi huu(August),Kanumba ameweza kuthibitisha jinsi anavyozidi kukomaa katika sanaa hiyo,kwa kutoka filamu ambayo imepewa jina Crazy Love(Part 1 & 2). Kwa mujibu wake yeye mwenyewe kupitia blog yake,ili kuweza kuigiza katika filamu hiyo,ilimbidi kusoma vitabu mbalimbali vya wanafalsafa mashuhuri ulimwenguni kama vile Plato,Karl Max,Alexander The Great,Samuel Taylor nk ili kuelewa zaidi mambo yanayohusu tabia za binadamu,falsafa nk.
Je usomaji huo ulimsaidiaje Kanumba katika Crazy Love?Usikose kununua makala halisi ya filamu hiyo pindi kwani sasa inashambuliwa kama njugu.

No comments:

Post a Comment