Francis Duru
MUIGIZAJI kutoka Nollywood, Francis Duru, amekanusha kupokea pesa kutoka kwa Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan kama takrima kwa ajili ya kampeni yauchaguzi mkuu wa awamu ya nne utakao fanyika mwaka 2011.
Imelezwa kuwa, Duru, na wasanii wengine nyota 50 kutoka Nollywood, walipokea Naila 300, 000/= kila mmoja kwa ajili ya kampeni ya Rais Jonathan, baadhi ya wasanii nyota wamekanusha habari hiyo. Wamesema kuwa wameungana kwenye kampeni hiyo kwa sababu wanaamini Jonathan ni kiongozi mwenye malengo thabiti na yenye mabadiliko.
Msanii huyo nyota amesema: “Inafurahisha kuona baadhi ya wenzangu wakishikia kidedea suala hili. Ni ajabu sana kuwa watu wameacha shughuli zao za kila siku na muda wao na kufanya hivyo kwa kuwa tuu wanaamini. Hawalipwi chochcote kwa kazi hiyo. Na ukweli ni kwamba wanafanya hivyo kwa mapenzi yao tuu, kumsapoti na kumwamini. Na kwa mimi, Jonathan ndiye mwanaume, nimemuona, nimekutana nae, nimeona kazi yake na ninajua anastahili kushika wadhfa huo.”
Mpango huo, ambao unaratibiwa na msanii Richard Ossai, ukisapotiwa na Mheshimiwa Ned Nwoko na kudhaminiwa na Sea Petroleum na Gas boss, Stella Odua, wameandaliwa kuhakikisha ushindi wa Jonathan katika ngazi ya urais.
Wakati huo huo wasanii 31 kutoka naija wamekamilisha kurekodi wimbo maarum kwa ajili hiyo utakaojulikana kama Goodluck 2011, uliotayarishwa na produzya aliyeshinda tuzo, Cobhams Asuquo, Pia wasanii wengine 20 nao pia wamekamilisha kurekodi wimbo mwingine wenye mahadhi hayo utakao julikana kama, Goodluck 2011.
Wasanii baadhi walioshiriki ni pamoja na mshindi wa tuzo za nyimbo za injili Sammie Okposo, African Chyna, Daddy Showkey, Zaaki Adzee na Tosin Martins .
Kundi la Kampeni yaGoodluck liko chini ya Barrister Gullac, ambaye anajitahidi kwa hali na mali kila wakati kuhakikisha linafanikiwa kupitia kwa wasanii hao.
No comments:
Post a Comment