BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Sunday, August 29, 2010

"Siwezi kuwa na mahusiano na mtu asiye kuwa na pesa!!" asema Uche Iwuji



Uche Iwuji


Siku kadhaa zimepita tangu mwanadada huyu aachane na boyfriend wake waliokuwa wakitoka pamoja kwa kile kinachodhaniwa kuwa jamaa ni choka mbaya,hii inatokana na maelezo kutoka kwa mwanadada huyu alivyo mzungumzia ex wake kwa waandishi wa habari walipo mhoji kisa cha kupigana chini na bwana wake na alikuwa na haya ya kusema.


"Nimeachana nae kwa kuwa hakuweza kunitimizia mahitaji yangu niliyohitaji na siwezi kuvumilia kuona nafsi yangu inahangaika kumuhudumia mwanaume. Kama unataka kunioa mimi nafikiri uwe na uwezo wa kunihudumia. Huhitaji kunipa kitu chochote. Usinipatie mahitaji yote ya dunia,naihitaji unipe kidogo tuu, kama chukua pesa hii, nenda katengeneze nywele. Chukua pesa hii, safiri, chukua usafiri wa ndege. Lazima uoneshe unajali, nionyeshe kuwa wewe ni mwanaume.Acha nione na nihisi nina mwanaume ndani ya nyumba. Huna haja ya kuniambia kuwa wewe ni mwanaume, unatakiwa unionyehse hivyo. Kwa nini niendelee kuteseka  kwa mwanaume ambaye hawezi kunitimizia mahitaji yangu? Aliyekuwa mpenzi wangu alikuwa anajua kupenda lakini ni mtu asiye weza kunitimizia mahitaji yangu na ndio sababu kubwa nimeachana nae." Muigizaji wa kike Uche Iwuji akizungumza na mwandishi wa habari kuhusiana na kwa nini ameachana na boyfriend wake?.

Amesema - "chukua pesa hii, nenda salon katengeneze nwyele"? nahisi amenukuu vibaya.
Hii si kitu ambacho wasanii wachanga wanaweza kusoma na kujifunza kutoka kwa mkongwe kama huyu ambaye wanategemea kujifunza kutoka kwake”.maoni ya mmoja wa waandishi aliye kuwa akizungumza na dada huyu kuhusiana na skendo hiyo.

No comments:

Post a Comment