BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Saturday, August 28, 2010

Nollywood DIVA, OGE OKOYE azungumzia kuhusiana na familia.


 Oge Okoye-Duru


MSANII maarufu wa kike, Oge Okoye ambaye ameolewa na mfanya biashara maarufu wa kimataifa, Stanley Duru amejifungua. Msanii huyo nyota, Oge alijifungua mototo katika hospitali Queen Elizabeth,London. Aliondoka nchini humo akiwa amebakiza mwezi mmoja ajifungue kuelekea London na alirejea akiwa na‘Bigie Bigie Bouncing Baby’. Alipata nafasi ya kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na moja ya chanzo cha habari Bi ALONGE MICHAEL na akazungumzia na furaha aliyonayo,baada ya kuwa mama. Mazungumzo yalikuwa hivi
KWA NINI UMECHAGUA KWENDA LONDON KWA AJILI YA KUJIFUNGUA?
Nimeona itakuwa rahisi sana London Uingereza kuliko nchi nyingine. Lakini usisau kuwa nilizaliwa hapa pia.

UNAJISIKIAJE SASA UMEBARIKIWA KUPATA WATOTO WAWILI WA KIUME NA WA KIKE?
Nina furaha sana na nina mshukuru mwenyezi Mungu kwa kunifanya kuwa mwanamke niliyekamiliaka. Unajua , furaha ya kila mwanamke ni kuwa na motto wa kike na wa kiume. ingawa, wazazi wengine wanapendelea jinsia moja, katika suala letu, tulikuwa na mtotot wa kwanza wa kiume na sasa wa kike, hatutarajii tena kujaaliwa kuwa na mwingine. Najisia Furaha.

JINSI GANI UTAWEZA KUWALEA WATOTO HAWA UKIZINGATIA NA MAZINGIRA HASA KATIKA FANI YAKO KWA KUWA WEWE NI MUIGIZAJI?
Hiyo sio issue sana. Nilipopata mototo wa kwanza, nilipata msaada kutoka kwa mama yangu na kwa wasaidizi wangu pia. Sikuruhusu movie kuharibu uhusiano wangu na mtoto. Nilikuwa najitahidi kuja mapema kuhakikisha motto yuko salama, ingawa, mama yangu alikuwa karibu kumwangalia  mpaka anakua.

HIVYO NI LINI HASA UNATARAJIA KURUDI KATIKA LUNINGA?
ki ukweli siwezi kususbili kurudi. Kabla sijaondoka kwenda London kwenye safari yangu, nilikuwa tayari nina kama script 9 katika shelve yangu, nilitegemea kwamba ningeweza kufanya movie kabla sijaondoka lakini haikuwa rahisi kwangu. Hata hivyo baadhi ya movie zimesogezwa na maproduzya wamenisisitiza  nirudi kuchukua nafasi yangu. Hivyo, sasa nimeshapona vizuri, sina jinsi zidi ya kurudi location na kumalizia movie hizo. Unajua, movie kwangu ni zaidi ya pesa, ni kitu napenda lazima nikikamilishe.
WATOTO WANGAPI UNATARAJIA KUWA NAO ZAIDI?
Idadi ya watoto tunayo hitaji inategemea na Mungu atatupatia wangapi. Kama akisema kumi 10, mimi ni nani nikatae?. Mungu ndiye ana maamuzi juu ya hayo.

STANLEY ANAZUNGUMZIAJE KUHUSIANA NA MAENDELEO HAYA?
Wee unahisi atajihisije? Furaha kabisa!anafuraha sana na haishi kushukuru mungu kwa kutufikisha mbali..

ALIKUWEPO KARIBU NAWE ULIPOKUWA LABOUR?
Hayo ni personal kwangu. Mashabiki wangu hawapaswi kujua kuhusu hilo, ukweli unabaki kuwa ukweli, alikuwa na mimi muda wote.

UTWABATIZA API WATOTO WAKO?
Hakuna kitu bora kama nyumbani, tunakuja Nigeria kwa ajili ya ubatizo wa wanangu. Muda ukifika tutawaalika ndugu,jamaa na marafiki kujumuika pamoja kusherekea.

No comments:

Post a Comment