BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Tuesday, November 8, 2011

AKUTWA CHUMBANI KWA DBANJI....


AWALI alikanusha kwamba hana uhusiano wowote wa kimapenzi na msanii Fally Ipupa wa Congo, lakini sasa Nadia Buari amefumwa nyumbani kwa mwanamuziki Dbanj wa Nigeria.

Msanii huyo raia wa Ghana alifumwa ndani ya jumba la mwanamuziki huyo usiku hivikaribuni akiwa amejivinjari kwenye kigauni cha kulalia huku akigonga mvinyo.

Chanzo kingine kimethibitisha kwamba mastaa hao wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi muda mrefu na hata Ghana wamekuwa wakionekana pamoja. Nadia anayekaribia miaka 30.

Kama ni kweli wawili hao wana mpango wa kuoana utakuwa ni mwisho wa uvumi uliokuwa umeenea kwamba D'banj alikuwa kwenye penzi zito la muigizaji Genevieve Nnaji.

No comments:

Post a Comment