MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Haji Adam Baba Haji anajuta kupoteza muda wake kwa kuchelewa kusomea sanaa na masuala ya filamu.
Masomo hayo anayosoma kwa sasa katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo yatamgharimu miaka mitatu.
Ninaamini kuwa baada ya kumaliza masomo yangu nitakuwa ni msanii wa kimataifa kweli kwa vitendo siyo kwa maneno tu, aliiambia Mwanaspoti.
Nimekuwapo hapa na nimejifunza mambo mengi sana kuhusu sanaa tunayoifanya hususani filamu, wasanii pamoja na watayarishaji tumeshindwa kabisa kuifanya tasnia hii ilete maslahi kwetu.
Nilichogundua ni ukosefu wa elimu hali inayopoteza umakini katika katika kazi zetu.
Msanii huyo amewashauri wasanii wengine kujiendeleza kielimu badala ya kutegemea vipaji tu, kwani anaamini kuwa mambo hayo yana mwisho wake hasa katika karne hii.
Anasema kuwa jambo ambalo analiona kwa sasa ni wasanii kufurahia maslahi kidogo yanayopatikana tena bila kuwa ya uhakika nayo.
Haji hivi karibuni alichaguliwa kuwa Rais wa Wanafunzi chuoni hapo

No comments:
Post a Comment