BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Monday, November 21, 2011

Wema amdondokea Linex

MWIGIZAJI na mrembo aliyewahi kushikilia taji la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, wiki hii amegeuka na kuamua kumwangukia msanii, Sunday Mangu Linex baada ya kumkashifu wiki kadhaa zilizopita kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Wema sasa amemwomba msamaha Linex kutokana na kitendo cha kumwingiza katika ugomvi aliokuwa nao na msichana mwenzake.

Amekiri na kusema kuwa ilikuwa ni hasira tu na alijikuta ameandika ujumbe uliomhusisha Linex kimakosa.

Ni hali ya kawaida na si mpango wangu kumkosea Linex, ila nilikuwa nikitolea mfano tu na sikumaanisha vile, ameandika Wema. 

Wakati huohuo, Linex wiki hii ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook kwamba amemsamehe mwigizaji huyo.

Linex alipokuwa Kigoma kwenye msiba wa babu yake aliyemlea, anasema alipata simu kutoka kwa watu wakimtaka kuingia katika ukurasa wa Blackberry Messenger maarufu kama BBM wa Wema Sepetu ili asome nini mlimbwende huyo amekiandika kuhusu yeye.

Kwa kweli nilijisikia vibaya sana baada ya kusoma ujumbe aliokua ameuandika,alisema Linex.

Umekosa watu mpaka unatembea na mtu wa ajabu kama Linex,ni ujumbe ambao Linex anadai uliandikwa na Wema na kusomwa na watu wengi.
Lakini sasa wameshasameheana.


No comments:

Post a Comment