BAADA ya kufanya vizuri katika filamu ya Blue Monday, muandaaji wa filamu hiyo, Abui Ahmed amewataka wapenzi wa filamu nchini kukaa tayari kwa ujio wa filamu mpya itakayokwenda kwa jina la Lost Hope.
Ahmed ambaye pia ni Mkurugenzi wa Abui Production alisema kuwa filamu hiyo iliyobeba ujumbe mzito wa familia na mapenzi kwa ujumla itakuwa sokoni mapema wiki ijayo.
“Filamu hii imebeba ujumbe mzito ambao nina uhakika utaelimisha jamii kwa ujumla na vilevile kumfanya kila mtu ajifunze kwa nafasi yake kutokana na kile kilichopo ndani ya filamu hii”alisema Ahmed.
Aliwataja wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ni pamoja na Michael Philipo (Kojack) ,Nila Sultani (Jasmin) ambao ni wahusika wakuu na wengine ni Flora Mvungi,Mainda,Abdala Agosi, Badi pamoja na wengine wengi.
Abui Production imehusika kuandaa filamu mbalimbali zikiwemo Zindiko,Tension of Love na Blue Monday ambayo inafanya vizuri katika soko la filamu nchini.
NEC YAWANOA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI BAGAMOYO,,DAR ES
SALAAM,MKURANGA,RUFIJI,CHALINZE
-
Na Magrethy Katengu, Dar es salaam
TUME huru ya Taifa ya uchaguzi NEC imewataka waratibu wa uchaguzi wa mikoa
,wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidi...
2 weeks ago
No comments:
Post a Comment