Shirika la utangazaji la Tanzania TBC leo limetangaza uzinguzi rasmi wa tamthiliya ya kichina mbayo imetafsiriwa kwa Kiswahili na wantanzania waishio nchini humo na wafanyakazi wa kituo cha radio cha China radio International (CRI).
Tamthiliya hiyo ambayo itajulikana kwa jina la ‘Dou Dou na Visa vya Mama Wakwe zake’ itaanza kuonyeswa rasmi TBC 1 tarehe 23 mwezi huu wa kumi na moja.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mkuu wa TBC Mr Clemence Mshana alisema kuwa lengo kubwa la tamthiliya hiyo ni kuonyesha jinsi lugha adhimu ya Kiswahili inavyoweza kutumika moja kwa moja bila kuweka tafsiri za maandishi katika filamu au tamthiliya kuelezea utamaduni wa mataifa mengine.
Alisema kuwa kupita tamthiliya hii, ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi wiki ya mwisho wa mwezi huu wa November, itawasaidia wasanii wa Tanzania ninsi wanavyoweza kutengeneza tamthiliya nzuri zenye ubora na zikaweza kuuzwa nchi za nje na hivyo kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili nje ya Tanzania.
“ Vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuitangaza lugha ya Kiswahili kwa kueleza jamii kuwa inatosheleza katika Nyanja mbali mbali za maisha ya binadamu bila kujali taifa lake,” alisema.
No comments:
Post a Comment