BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Saturday, November 5, 2011

WAZEE WATATU VICHWA KATIKA TASNIA YA FILAMU KWA SASA...

KILA unapokutana na filamu yoyote ya Bongo, si rahisi kuzikosa sura hizi katika filamu hizo. Sura hizo ni za wasanii Hashim Kambi �Ramsey�, Charles Magali �Mzee Magali� na Ahmed Olotu �Mzee Chilo�.

Wakongwe hao hata kama watakuwa wameigiza japo kwa ufupi, lakini ndiyo wasanii wa kiume wanaoongoza katika kushiriki filamu nyingi za Bongo, ukiachilia Ray na Kanumba, ambayo hufanya kazi zao wenyewe. 

Uchunguzi unaonesha kuwa wasanii hao wamekuwa wakihusishwa katika filamu mbalimbali kutokana na uhusika wao, kwa maana watu wenye mwonekano wa kiutu uzima.

Pengine kama wangekuwa wanalipwa vizuri, ni wazi tungezungumza mambo mengine kwa sasa. Walistahili kuwa matajiri wa kutupwa. 

Lakini kwa bahati mbaya, Bongo, pamekuwa na mfumo usioeleweka. Hollywood, Bollywood na kwingineko wasanii kama hawa hutengeneza fedha nyingi kwa kila hatua, kuanzia mikataba ya ushiriki wa filamu husika, maonyesho ya filamu katika majumba ya sinema na uuzaji wa filamu katika DVD. 


No comments:

Post a Comment