BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Sunday, May 6, 2012

Jamani msaidieni huyu muigizaji

   MUIGIZAJI maarufu wa filamu nchini Tanzania, Wastara Juma, amesema kuwa alikataa kuwekwa mapumziko (bed rest) kwa wakati wote wa ujauzito wake kutokana na kumuuguza mume wake Juma Kilowoko maarufu Sajuki ambaye anasumbuliwa na matatizo ya uvimbe tumboni.

Wastara, ambaye hivi sasa ana mtoto mwenye umri wa miezi miwili, anasema matatizo ya afya yake kwa wakati huo ndiyo yaliyosababisha madaktari kutaka alazwe hospitalini.

"Tangu mume wangu alipokuwa anaumwa nilikuwa nahangaika naye huku na kule kumtibia, lakini baadaye nilikuja kugundua kuwa nilikuwa mjamzito. Vipimo vya hospitalini vikaonyesha nina matatizo ya sukari ya mimba, presha pamoja na mguu wangu ulikuwa mbovu," anasema.

Anasema kutokana na ugonjwa wa mume wake, hakutaka kukubaliana na madaktari kuhusu kulazwa kwa kipindi chote atakachokuwa mjamzito na badala yake aliendelea kumuuguza mumewe.

"Nilikataa kulazwa, kwa kweli, japokuwa nilihatarisha maisha yangu, niliendelea kumuuguza na kuhangaika huku na kule, wakati huo mimba nayo ilizidi kukua. Kwa bahati mbaya ilipofikia miezi nane na wiki moja madaktari waliniamuru nifanyiwe oparesheni kwani nisingeweza kuzaa kwa njia ya kawaida, na Machi 5 mwaka huu ndipo nilipompata mtoto wangu," anasema.

Hata hivyo, anabainisha kuwa ilimlazimu kusimama kazi zake zote ili aweze kumuuguza Sajuki.

"Kutokana na ugonjwa wa mume wangu, ilinilazimu kuacha kazi, kuacha kuigiza pamoja na kusimama kwa kazi zangu binafsi ili niweze kupata wasaa wa kumuuguza mume wangu.

"Nilifunga ofisi na vitu vyangu vyote zikiwemo mashine tunazozitumia katika kazi, nilihamishia nyumbani, vitu ambavyo viliibiwa siku moja baada ya mimi kujifungua," anasema.

Changamoto anazokutana nazo Wastara ni kubwa. Anasema kuwa anahitaji zaidi ya Sh 25 milioni pesa za Kitanzania ili kuweza kuokoa maisha ya Sajuki ambaye kwa sasa anatumia dawa zenye thamani ya Dola 1,000 kwa wiki moja alizozinunua nchini India.

"Nahitaji Sh 25 milioni ili Sajuki aweze kupona, kwani kwa sasa anatumia dawa ambazo alizipata nchini India tulizonunua dola 8,000, lakini zikiisha anatakiwa kurudi tena ili akapewe nyingine na matibabu zaidi, sina pesa na vifaa vyangu vyote niliibiwa.�

Anasema na kuongeza: "Tuna maisha ya kawaida kama watu wengine, lakini ninavyoomba msaada watu wananishangaa, kwa kuwa wanatuona tunacheza filamu katika majumba ya kifahari wanadhani ndiyo maisha yetu, siyo hivyo, mimi nafanya hivi ili mume wangu apone.�

Wastara aliweka bayana nambari za akaunti yake ya benki kwa wale wenye mapenzi mema wanaotaka kumsaidia kuwa ni Wastara Juma, Akaunti Namba 050000003047 iliyopo Akiba Commercial Bank.

�Tatizo kubwa zaidi linalomsumbua Sajuki lilikuwa ni kukauka kwa damu ambapo ilifikia hatua anakuwa na damu 5 mpaka 4, hali ambayo ni hatari, lakini nashkuru Mungu kwani ameanza kutumia dawa na kwa sasa ana damu 9,� anaeleza Wastara.

Anasema kuwa, katika maisha yao wamekutana na mitihani mingi ikiwemo yeye kukatwa mguu siku chache kabla ya ndoa yake na kwa sasa kuugua kwa wote wawili kwa wakati mmoja.


No comments:

Post a Comment