Bastola ambayo inadaiwa
ilikuwa ikitumiwa kihalali na staa wa filamu barani Afrika, Steven
Charles Kanumba, inasakwa na Jeshi la Polisi Tanzania.Kamanda wa Mkoa
wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Charles Kenyela amesema kuwa
anafuatilia kumbukumbu za silaha hiyo, kwani haijarejeshwa kwenye jeshi
lake.Kenyela alisema juzi kuwa anafuatilia umiliki wa Kanumba juu ya
umiliki huo na baada ya hapo, jeshi la polisi litawahoji ndugu“Bastola
ni mali ya serikali. Kuna hatua ambazo hufuata mpaka mtu aruhusiwe
kumiliki bastola,” alisema Kenyela na kuongeza:Endapo mmiliki halali wa
silaha hiyo atafariki dunia, ndugu zake lazima waikabidhi kwa jeshi la
polisi na baada ya hapo, kama kuna ndugu anataka aimiliki, inabidi
afanye maombi upya na atakapokidhi vigezo ndiyo anaruhusiwa.“Kutokana
na hali hiyo, bastola ya Kanumba lazima irudi kwetu haraka na kama kuna
ndugu yake yeyote anataka kuimiliki, itabidi awasilishe maombi.”Kenyela
aliongeza kuwa hivi sasa anafuatilia kumbukumbu za jeshi la polisi ili
awe na uhakika kama kweli msanii huyo alikuwa anamiliki silaha
hiyo.“Tukithibitisha tutawahoji ndugu zake pamoja na wengine
wanaohusika ili tuwe na taarifa za hiyo silaha. Ila kwa sasa tunafanyia
kazi taarifa hizi kwa kupitia kumbukumbu za jeshi,” alisema.Kenyela
alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa na ripota wetu kama jeshi lake
limeshapokea bastola ambayo alikuwa anaitumia Kanumba enzi za uhai wake.
NDUGU WANASEMAJE?
Mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa, aliulizwa na paparazi wetu kuhusu bastola inayodaiwa kutumiwa na mwanaye alipokuwa hai, na haya ni majibu yake:“Sijaiona hiyo bastola humu ndani tangu nimefika hapa. Sijui ipo wapi na sijui kama kweli Kanumba alikuwa anamiliki hiyo silaha.“Najua sheria za silaha hiyo, kwa hiyo ingekuwepo ningeiwasilisha polisi haraka. Baba yangu alikuwa na silaha hiyo, alipofariki dunia tuliikabidhi kwa jeshi la polisi.”
NANI ANAJUA ILIPO?
Taarifa zinaonesha kuwa mdogo wa Kanumba, Seth Bosco alikuwa karibu zaidi na marehemu lakini kwa sababu umiliki wa silaha hiyo ni siri, siyo rahisi kujua ilipo.Mtu mwingine ambaye alikuwa karibu na marehemu mpaka nyakati za mwisho za uhai wake, kama ripoti zinavyoonesha ni muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, ingawa naye inawezekana akawa hajui kutokana na unyeti wa silaha yenyewe.
BASTOLA NA KANUMBA
Akiwa hai, Kanumba aliwahi kuripotiwa mara kadhaa kumiliki silaha hiyo, japo haikufafanuliwa kama ni kihalali au batili.Kanumba aliripotiwa kwa mara ya kwanza kumiliki bastola miaka minne iliyopita, akidaiwa kuichomoa baada ya kuvamiwa na kundi la watu aliohisi wanataka kumteka.Licha ya stori hiyo kuandikwa gazetini na nyingine ambazo zilimhusisha na umiliki wa bastola, bado Kanumba hakuwahi kufafanua chochote kuhusu silaha hiyo.
IPO WAPI?
1. Je, aliiacha sehemu ambayo hakuna mtu ameweza kupafikia?
2. Aliirejesha kabla mauti hayajamkuta ndiyo maana haionekani?
3. Je, Kuna mtu aliiwahi baada ya kifo chake akiona ni dili?
Kanumba alifariki dunia Aprili 7 na kuzikwa Aprili 10, 2012 kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. wa msanii huyo kuhusu kurejesha bastola hiyo jeshini.

No comments:
Post a Comment