BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Wednesday, May 2, 2012

Martin Lukanga
Tin White.
MCHEKESHAJI mahiri wa vichekesho Swahiliwood Martin Lukanga ‘ Tin White’ ameamua kuachana na komedi za kushirikishwa bali ni kuandaa komedi zake mwenyewe kama ambavyo ufanya wasanii wenzake na kuuza kwa wasambazaji, akiongea na Jukwaa la filamu Tin White amesema ameshiriki Komedi nyingi lakini hapati nafasi nzuri ya kuwakilisha mawazo yake.
“Nimetumwa sana na mimi zamu yangu kuwatuma vijana wangu nimetayarisha Komedi yangu kali inayokwenda kwa jina la Mr. Lover ni hadthi nzuri ina mtiririko mzuri kama zilivyo filamu, ni komedi ya kipekee mtu anacheka humo kwa ajili ya hadithi na si vinginevyo, nimeanza na spidi yangu haina mwisho,”anasema Tin White.
Kama ilivyo tabia ya wachekeshaji ya kujikusanya na kushiriki kwa wingi katika filamu moja na humu namo wapo wachekeshaji kama Bambo, Kingwendu, Ringo, Tin White mwenyewe, Mtanga, alipoulizwa kwani nini wachekeshaji wengi ujazana katika filamu moja alisema kuwa si wao bali ni fikra finyu za wasambazaji wanaamini
kuwa wachekeshaji wengi ndio kuuza, lakini yeye anaamini kuwa hata msanii mmoja tu anatosha.

No comments:

Post a Comment