BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Saturday, June 18, 2011

FILAMU MPYA YA MORE THAN CRAZY SOKONI MWEZI HUU.

Msanii wa filamu Daudi Michael.
Msanii wa filamu hapa nchini Tanzania, Daudi Michael amekamilisha utengenezaji wa filamu yake itakayo tambulika kwa jina la “More than Crazy”. Daudi Michael amesema kuwa yuko katika hatua za mwisho za kufanya mazungumzo na baadhi ya wasambazaji na mambo yakienda vizuri anatarajia kuingiza sokoni filamu hiyo mwezi huu wa sita. Filamu hii ya “ More than Crazy”  inazungumzia dhuruma kwa ndugu wa damu na pia kwa upande mwingine inahusu usaliti katika mapenzi kutokana na ugumu wa maisha. Daudi Michael amesema kuwa filamu hii ni ya saba kutengeneza chini ya kampuni yake ya D Production, ambayo ndani ya filamu  hii amecheza na baadhi ya nyota wa filamu kama vile Ester, Mzee Magari, Baambucha na Sudi Ally.

Msanii huyu Daudi Michael alijiingiza rasmi katika sanaa ya maigio mwaka 2007 mwezi  wa 9 siku ya Ijumaa, chini ya kundi la maigizo la Bahari Arts Group, kundi ambalo hujihusisha na kutengeneza filamu na tamthiliya mbalimbali. Kundi hili lilikuwa likisimamiwa na mwalimu Adam Joseph pamoja na Japhari Makatu amabao Daudi Michael anaeleza hawa  watu ndio chachu ya mafanikio yake hadi sasa kwani walimpatia elimu ya sanaa vya kutosha.
Daudi Michael akiwa na Msanii Heliety Kahembe.

Akizungumzia kuhusiana na Tasnia ya filamu na sanaa ya maigizo kwa ujumla Daudi Michael anasema kuwa “Sanaa ni maisha ya mwanadamu yeyote aliyeko duniani, naamini kila Mtanzania anaweza kuwa msanii kwa sababu hayo tunayocheza ni maisha halisi ya watanzania na napenda tuu kuwashauri wasanii wasikurupuke na watambue kuwa ni muhimu sana kupata elimu ya sanaa” Daudi alieleza.

Nilipofanya mazungumzo naye nilimuhoji kuhusiana na hali iliyo katika sanaa kwa nini wasanii wengi hasa maproducer hutumia majina ya kiingereza katika filamu zao kwa mfano filamu zake. Daudi allisema kuwa yeye aliangalia uelewa, upokeaji wa watu na kuhusiana na filamu zilizoandikwa majina  ya kiingereza na kugundua kuwa ‘majina ya Kiswahili hayana  mvuto, pili yanajaza eneo katika uandishi na pia lugha ya kiingereza ni lugha ya kimataifa na wanunuzi na wasambazaji ambao ni wahindi hupenda kununua filamu wanazozielewa majina. Na kitu cha mwisho ni kwamba walianzisha tasnmia nzima ya filamu walianza na lugha hii” alisema daudi.
Daudi Michael akiwa na Esther Flavian.
Alipozungumzia kuhusiana na nini wadau wa filamu watarajie kutoka kwake na neon lake la mwisho kwa wadau Daudi alisema kuwa anamtanguliza Mungu katika kila hatua anayofanya na alisema kuwa kampuni yake imejipanga vizuri crew nzima na aliwasihi wadau watarajie kazi nzuri kutoka D Production ambayo ndiyo kampuni yake anayoimiliki. Pia aliwasihi wadau wa filamu wapende kufanya research wasikurupuke na aliwaomba watanzania wa wadau wote kwa ujumla wapokee kazi zake na pia palipo na makosa washiriki kwa kumpa maoni kwa kuwa katika kila filamu zake hutoa namba za simu ili aweze kupata ushauri mbalimbali.

D Production ni kampuni yak wake mwenyewe daudi Michael na ina Crew ya watu mbalimbali akiwemo Kenny Aichi ambaye ni Editor, faridu Nankape na Fadhili Maogola ambao ni Camera man, Santana ni production Manager, Bora Arphani ni make up manager. Pia alisema chinio ya D Production alishatoa zaidi ya filamu sita ikiwemo Season of love, Noway out alizotoa mwaka huu na zingine nyingi tangu alipoanzisha kampuni hii rasmi mwaka 2008 alipotoa filamu ya Upside Down.

No comments:

Post a Comment