BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Sunday, June 19, 2011

Filamu nyingi za Bongo zinakosa uhalisia

Kanumba akiwa na Aunt ezekiel
Filamu nyingi za Kibongo zimekuwa zikikosa mvuto hasa kwa watu makini wanaozitazama kutokana na waigizaji wengi kusahau majukumu yao ya uigizaji na badala yake kutafuta ufahali kwenye filamu zao.
Kuna maswali ambayo nimekuwa nikijiuliza kama vile kwa nini wasanii wetu wanapenda kutumia majumba ya kifahari, moja je ni ushamba au ulimbukeni, pili je ni hali ya umaskini ambao unatokana na famila nyingi za Watanzania?
Sababu za kufikiria hayo zimetokana na ukweli kwamba Watanzania wengi tumetokea katika nyumba za kawaida hivyo wasanii hao wanakuwa na fikra mgando wakifikiria iwapo wataigiza katika nyumba za kawaida filamu hazitavutia.
hemed
Wapo wengine wanaokuwa wanafikiria kwamba wakitumia nyumba za kawaida hawatauza na kuonekana tofauti na wengine.
Kuna wale wenye fikra mgando wakitumia fursa hiyo ya majumba ya kifahari wakiamini hawana uwezo wa kuyamiliki.
Wapo ambao walioathiliwa na hali ya umaskini ambao wamejikuta wakiathirika kisaikolojia wakifikiria kuonekana kwenye majumba ya kifahari ndipo watauza zaidi na konekana wa thamani machoni mwa mashabiki wao.
Wasanii wa hapa nchini wanajikuta wakitumia magari ya kifahari yenye bei za kutupwa kama vile Hammer, Vorg na mengine ya aina hiyo.
Wasanii hawa wamekuwa wakienda mbali huku wakisahau hata filamu zao zinakuwa na maudhui ya namna gani.
Waigizaji wetu wameshaathiliwa na kuigiza maisha ya kitajiri wa kupitiliza hali iliyowafanya wakati mwingine hata watazamaji kujikuta kushindwa kutazama filamu na kubaki kuangalia magari na majumba wanayotumia.
Tatizo kama hilo limeikumba tasnia hii kwa wale wanaokuwa waigiza kama mabosi hata kama ofisi ya kawaida lakini wamekuwa wakionekana wamepigilia suti kila wakati.
Yusuph mlela
Kwa mfano utamkuta mwigizaji anaigiza kama Afisa uhusiano wa benki ya NBC kila muda anapoonekana iwe nyumbani njiani amevalia suti ya gharama.
Hali kama hiyo inafikia nasema kuwa huu ni ushamba watu kama hawa ndiyo wanauwa wabishi hata kuigiza filamu zinazoonyesha mazingira ya vijijini au kuwa mfanyakazi wa ndani.
Huu usharobaro umesababisha hata wakati wanapokuwa wanapiga picha za mwigizaji akiwa anaamka usingizini akiwa amejipigilia urembo usoni ‘make up’.
Ushauri wangu tuu ni kwamba ili tuweze kuingia kikamilifu katika soko la filamu kimataifa ni lazima tuweze kuweka uhalisia kwanza ndipo tuanze kuonesha matumizi ya hivyo vitu vya thamani.
Wasanii wanatakiwa watambue kuwa watazamaji wao wanatoka maeneo mbalimbali na wengi ni wale wenye uwezo wa hali ya chini na kawaida ambao hawana uwezo wa kumiliki magari au majumba ya aina hiyo hali ambayo inawasababishia kushindwa kuangalia filamu na kubaki kuangalia aina ya gari, umba au suti aliyovaa msanii.
Ester Flavian
Wasanii wanatakiwa wawe makini kutazama aina ya hadithi wanayokuwa wanaigiza na si kutazama aina ya vitu wanavyotumia vina thamani ya aina gani na kujikuta mwisho wa siku wakishindwa kujikita katika hadithi husika.
Esterflavian,Daud michael,'Ramsey wa bongo,na Raulant Anthon 

No comments:

Post a Comment