Meneja wa kinywaji cha Grand Malt bidhaa ya TBL Bi. Consolata Adam akiongea katika uzinduzi rasmi wa Tamasha la wazi la filamu Tanzania (Grand Malt Open Film Festival) katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga. Bi Consolata Adam amesema kwamba Wiki ya maonyesho ya wazi ya Filamu inaendelea mpaka tarehe 3 Julai Mwaka huu. Maonyesho hayo ya Filamu yanafanyika kwa mara ya tatu katika historia yake.
Meya wa jiji la Tanga Mzamil Shemdoe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la wazi la filamu Tanzania (Grand Malt Open Film Festival) katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga Kulia ni Musa Kissoky mkurugenzi wa Sofia Production waratibu wa tamasha hilo na Kushoto ni Consolata Adam Meneja wa kinywaji cha Grand Malt bidhaa ya TBL ambao ndiyo wadhamini wakuu wa maonyesho hayo ya filamu Tanzania.
No comments:
Post a Comment