BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Saturday, June 18, 2011

'MAOGOLA' MIAKA 12 KATIKA SHUGHULI YA KU-SHOOT VIDEOS Kinachomkela ni dharau kutoka kwa wasanii.

Camera man fadhili maogola.
Fadhili Maogola ni mmoja wa baadhi ya watu wanaojihusisha na shughuli za uchukuaji wa picha za Video na za mnato (Cameraman). Alijiingiza rasmi katika tasnia hii mwaka 1999 chini ya kampuni ya Cool Multmedia na baadae alihamia katika kampuni ya Kijitonyama Upendo group (KUG) akiwa kama camera man na Editor  wa video. Akiwa hapo alifanya kazi nyingi  kama kurekodi video za nyimbo za injili zikiwemo album mbalimbali kama “ Mungu Anakupenda”, “ Bam Bam”  kutoka Kijitonyama Upendo Group Choir,  “Uwe macho” ya rose Muhando, “Mapito ya Bahati Bukuku na nyingine nyingi, ambapo anaeleza baada ya kukomaa katika kazi hii alianzisha kampuni yake binafsi.

Focus media company ni kampuni yake binafsi aliyoianzisha na kuisajili serikalini mwanzoni mwa mwaka huu 2011. Chini ya kampuni yaake amefanya documentary na filamu mbalimbali zikiwemo Question mark, Adhabu ya kaburu ambazo zintarajiwa kutoka hivi karibuni. Mbali na filamu hizo pia amefanya Documentary mbalimbali na watu tofauti tofauti wa ndani na nje ya nchio. Pia akiwa kama mpiga picha wa kujitegemea amewahi kufanya kazi na Hemed katioka filamu ya “Johnson”, amefanya na Yusuph Mlela katika filamu ya “Mtumwa wa mapenzi” na pia amefanya kazi na wasanii wengine wengi kama Jackline Wolper, Mzee Magali, Miriam Migomba na pia amefanya na daudi Michael katika filamu ya “More than Crazy”.

Fadhili Maogola ambaye ni motto wa sita katika familia ya mzee Maogola, alizaliwa miaka 33 iliyopita na kupata elimu yake hapahapa Dar es Salaam na kufikia kidato cha nne baada ya hapo alijiunga na kozi ya electronics katika chuo cha VETA, fadhili ameeleza kuwa kwa sasa bado anasema katika chuo kimoja nchini Kenya Nairobi kinachotoa elimu ya video Production. Kwa upande wa maisha yake binafsi Fadhili ana mchumba na alibahatika kupata watoto mapacha wa kike na wakiume ambao ni Faiza fadhili na Fahami fadhili.

Akizungumzia kuhusiana na Changamoto mbalimbali wanazopata camera Man, alisema kuwa anakerwa sana na dharau kutoka kwa wasanii, anasema kuwa CameraMan anaonekana ni mtu wa mwisho hivyo hata mapato wanayopata ni kidogo nah ii inasababishwa sana na wengi wao kutokuwa na elimu ya ufanisi wa fani hiyo( sio professional). Hivyo alishauri kwa wapiga piccha wenzake wajifunze, na watafute ushauri kwa waliotangulia katika kazi hii na pia wafahamu mambo yanayowahusu katika Production kwani Cameraman sio kujua kushika na  kuwasha camera tuu bali kuna vitu vingi, alisema fadhili.

Katika mazungumzo Fadhili Maogola alizungumzia kuhusiana na mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu na kusema “ Napenda kuongelea mmmomonyoko wa maadili katika ngazi tatu yaani kwa waandishi wa habari, vyombo vyo habari na wasanii uchwara. Zamani katika Radio na television nyimbo zisizo na maadili zilikuwa  hazichezwi lakini sa hivi wadau hawazingatii maadili hayo wanaonesha mambo yasiyofaa. Kwa waandishi wanaharibu jamii kwa kuandika habari chafu mfano uchangudoa na hata wanatoa picha chafu katika magazeti. Wasanii nao sa hivi wamepoteza maadili maadili wanaona furaha kupiga picha za uchi na kuzitoa katika baadhi ya magazeti ninaomba kushauri hawa wote wajirekebishe” alisema Fadhili.
Fadhili alipenda kuwashukuru baadhi ya wadau walimsaidia hata kimawazo hadi hapo alipofika kuweza kumiliki kampuni yake binafsi Focus media Company, watu hawa ni kama Mzee Kidai, fanuel Ndonde, Christian Kika, marehemu Mzee Hamir Rajab, Rose Mhando na meneja wake Nathani Wami kwa mchango wao anawashukuru. Aliwashauri wasanii watambue umaarufu utakuja tuu na si kwa kukaa uchi na aliwasili wanaopenda kuwasiliana nae hata kuomba ushauri na kikazi zaidi watumie 0712 515145 ili kukuza tasnia nzima ya sanaa na muziki kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment