BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Wednesday, September 7, 2011

MASAWE MTATA APANIA KUFANYA KWELI..

MSANII wa maigizo ya vichekesho ( The Commedy) Rogers  Richard a.k.a. Masawe Mtata amesema atahakikisha anafanya vizuri katika kazi yake ili kipindi cha The commedy kinachorushwa na EATV kiwavutie zaidi watazamaji.
Mtata, ambaye anashika nafasi ya pili katika igizo la komedi linalorushwa na Televisheni ya East Afrika kama wasemavo wapenzi wa kipindi hicho.

“Naipenda sana kazi yangu, hii ni kutokana na harakati mbalimbali nilizopitia katika kuhakikisha kuwa namimi natoka kimaisha.Nitahakikisha nafanya kila mbinu ambayo itaweza kufanya mabadiliko ya hapa na pale lengo likiwa ni kukiboresha kipindi chetu,” anasema.
Mtata anasema, kazi ya kuigiza kwa vichekesho inahitaji ubunifu mkubwa na kwamba wasanii wengi hawatambui ubunifu huo.
“Hili ni tatizo kubwa kwa wasanii kwa kuwa sisi wasanii tunapenda umaarufu wa magari tu bila kutambua kuwa tunatakiwa kuwa wabunifu katika kazi zetu,” anasema.
Aidha Mtata anasema, wasanii wanatakiwa kujiamini katika kila fani ili waweze kufikisha ujumbe kwa jamii kwa njia mbalimbali.
Mtata anasema, mbali na kuwa msanii wa komedi pia ni mwanamuziki na tayari ameandaa albamu yake itakayotambulika kwa jina la ‘Swaga za Kichaga’.
Akitoa ushauri kwa wasanii wenzake, anasema wasanii waboreshe ushirikiano ili waweze kuimarisha Industry ya sanaa.

No comments:

Post a Comment