BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Tuesday, September 21, 2010

KANUMBA AMTEMBELEA MZEE KIPARA KUTAZAMA HALI YAKE!.



 Mzee Kipara.
Bila shaka umesikia habari kupitia vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vinavyomilikiwa na Global Publishers kuhusu hali ya muigizaji mkongwe nchini,Fundi Saidi maarufu kama Mzee Kipara.
Habari hizo zilikwenda sambamba na habari kwamba msanii huyo mkongwe,amesikitishwa na hali ya “kutelekezwa” na baadhi ya wasanii aliowasaidia katika kuinua kama sio kuanza safari yao katika kazi za sanaa kama vile Steven Kanumba na Ray Kigosi.
 Kanumba na Mzee Kipara wakizungumza.
Katika kuthibitisha kwamba kimsingi hakuna uhasama au “kutojaliana” baina ya Mzee Kipara na wasanii hao,hivi karibuni Kanumba alimtembelea Mzee huyo nyumbani kwake maeneo ya Kigamboni jijini Dar-es-salaam.

Mzee KIPARA anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu ambapo kwa mujibu wake ameeleza hospitali kadhaa alizoenda hawaoni tatizo japo miguu inamuuma

 Kanumba akimpatia Mzee kipara kiasi cha pesa cha kumsaidia.

No comments:

Post a Comment