BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Tuesday, September 7, 2010



Kila kukicha wasanii wamekuwa wakilalamika kuhusu kipato wanachovuna kutokana na kazi zao.Lakini mpaka leo kilio hiki hakijatafutiwa ufumbuzi wake, kila kukicha ni pirates wanaolalamikiwa na wasanii.Ebu fikiria kibanda kama hiki pichani kinaingiza watu wapatao 30-50 ambao lila mtu analipa 500 mpaka 300 kwa picha moja,kwa ujumla unapata kama 15,000 mpaka 20,000 kwa session moja na unakuta kwa siku kuna sesion mpaka 5,Je? msanii ni shs ngapi anapoteza kwa watu kama hawa.Je? watu wanaoingia humu wangeamua kununua kwa kila tape moja shs 5000 ni shs ngapi msanii angepata.Yote haya ni kwasababu hakuna sheria za kuwabana watu kama hawa hata ukiwakamta utamfungulia mshataka kwa sheria ipi? Hiki ndicho kilio chetu kila siku wasanii.Hawa ni wachache tu wako wengi sana huko mitaani wanaorudufu kazi zetu.Ni lini serikali itatilia mkazo kazi zetu ili tufaidike kutokana na kazi zetu?,
Baadhi ya bidanda vinavyoonesha filamu za kibongo.
Msanii Chopa akiangalia kwa masikitiko makubwa bango la matangazo.

No comments:

Post a Comment