BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Friday, September 3, 2010

MATAYARISHO YA FILAMU YA PRETTY GIRL




Msanii nyota wa filamu hapa nchini Ray the greatest pamoja na mastaa wengine wamekamilisha utayarishaji wa filamu ya Pretty Girl chini ya kampuni ya RJ company na amesema kuwa itakuwa na mastaa  kibao na  pia  wasanii wakali wanao chipukia katika game ambao baadhi mastaa hao ni kama Irene Uwoya na Frank Mwikongi na msanii mpya Bisso. Kwa mujibu wa msaanii huyu amesema kuwa amekwisha maliza kufanya shooting kuandaa cover ya movie itakayokuwa mbele ya Cd na poster za matangazo.Na amesema kuwa Cover ya sasa hivi mbele itakuwa na vichwa vitatu akiwemo yeye mwenyewe,Irene Uwoya na Frank Mwikongi “Nina uhakika poster itakuwa nzuri na watu mtaipenda” alisema Ray




Ray the Greatest akiongelea kuhusiana na utengenezaji wa filamu hiyo pia aliendelea kueleza kuwa “Kuna scene katika movie huwa ni ngumu kwa mchezaji ikitokea umepangwa ucheze.Ndio ilivomtokea PRETTY GIRL Irene Uwoya katika baadhi ya scene ilimuwia vigumu kucheza,lakini kutokana na umahiri alionao aliweza kucheza na akamudu vizuri.Ndio maana mpaka sasa naamini kuwa Irene Uwoya ni the best kwa sasa kwa upande wa actress in Tanzania.” Na amewasihi mashabiki wa tasnia hii wakae mkao wa kula kwa kusubiri kazi hiyo kwa kuwa kama kawaida ya RJ company inavyofanya vitu bombaa


Haya ni baadhi ya matukio yaliyojili wakati wa utengenezaji wa filamu hiyo ya “Pretty Girl”
 Irene akiwa kazini


 Bosco na Irene wakiwa katika scene
Frank naye kajipanga
Moja ya Scene ngumu kwa Irene
Raqee(akipiga picha za Cover). 
Camera man Yusuph on the set.

No comments:

Post a Comment