BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Tuesday, September 7, 2010

KANUMBA THE GREAT FILM MZIGONI KUTOKA NA UNCLE JJ.

Kanumba the greatest na Jeniffer katika scene.

MSANII nyota wa filamu na maigizo hapa nchini Kanumba ama the Great ameanza kuandaa kazi yake mpya iitwayo UNCLE JJ akiwa na wasanii vijana wadogo wale waliokamua nae vizuri katika THIS IS IT. Safari atakuwa Bush na anasema itakuwa na full vituko.filamu hii ikiwa imeandaliwa chini ya kampuni yake ya KANUMBA THE GREAT FILM na akitumia vifaa vyake mwenyewe ambavyo kanumba anasema kwa sasa hatarudi tena katika suala la kukodi kutokana na kununua vifaa hivyo kuanzia kamera mpaka vifaa vya editing. 

Akizungumzia kuhusiana na ma-actors walioshiriki katika filamu hiyo ni watoto waliokuwepo katika filamu ya THIS IS ITambao ni Jenifa na Patriq na anasema kuwa toka awatambulishe katika ulimwengu wa filamu Jenifa na Patriq kupitia filamu hiyo wamekuwa gumzo mtaani hata kwa watoto wenzao kila wanapopita inawalazimu kupiga picha na wenzao jambo ambalo nao kwa sasa wanaanza kuzooea hawakatai maana ameshawafundisha nini maana ya kuwa Star,mbali na hayo anawasimamia shuleni kuhakikisha wanasoma vizuri na kupata elimu bora hii ni kutokana na uwezo wao katika sanaa.

 Patric na Jeniffer wakiwa na watoto.
Katika filamu hiyo amemtumia Farid Uwezo kama camera man ambae ndio mara ya kwanza kufanya nae kazi,na Farid alimweleza Kanumba kuwa kila mara kwa mda mrefu sana alitamani kufanya kazi na yeye na leo ndoto yake imetimia tena akitumia camera yake ya kiwango cha juu,
 Farid Uwezo akiwa na Kanumba na Camera yake mpya.
Jamani hiyo ndio camera yake Kanumba kutoka katika kampuni yake ninayomiliki kwa sasa ‘ni kifaa ninachojivunia kukinunua maana uwezo wake ni mkubwa mno katika picha pia ni producer wachache sana nchini wanaotumia na kumiliki camera kama hii,ni SONY DSR 390’ asema kanumba.

Hiz ni picha za baadhi ya scene zitakazo kuwepo katika filamu hiyo ya UNCLE JJ.
 Jeniffer akifanya mambo katika Scene.
Kanumba the greatest na Jeniffer katika scene.
 Patric na Jeniffer katika Scene.

No comments:

Post a Comment