Kanumba (Msanii wa filamu Tanzania).
Hivi sasa sanaa ya filamu inazidi kukua nchini Tanzania. Inatia moyo sana kuona watu wa mataifa mengine wanaangalia filamu ambazo zinaitwa “za kibongo”. Msanii wa filamu Irene Uwoya kutoka Bongo.
Pamoja na hayo kazi kubwa bado ipo mbeleni.kuna haja ya serikali kutoa support ya kutosha ili kuzidi kuinua sanaa hiyo. Marekani ipo hapo ilipo kwa sababu ilitangaza sanaa na sera zake za mambo ya nje kupitia kwenye filamu. Ikulu ya Marekani ina kitengo cha kushughulikia masuala ya filamu.Kama filamu itaonekana haijakaa “vizuri” kwa mujibu wa taratibu zao,basi haitoki.Frank (Msanii wa filamu Tanzania).
Mmoja wa wasanii wa filamu hapa nchini Frank alifanya mazungumzo na waandishi na akasema lazima wasanii na washika dau wote katika nyanja za filamu wakubali kukosolewa. Unapokubali kukosolewa unajipa nafasi ya ushindi kwani maana yake ni kwamba kesho utafanya kizuri zaidi.Lakini pia ipo haja ya wakosoaji kutokuwa “wabezaji”. Unapokosoa basi useme pia sababu zako na utoe ushauri wa kujenga kwamba nini kifanyike.Kwa mwendo huo filamu za kibongo zitazidi kupata jina na sio ajabu kabisa siku moja nasi tukaona wakina Denzel Washington wa kikwetu kutokana na sanaa hii hapa bongo. Msanii wa filamu Ray kutoka Bongo.
No comments:
Post a Comment