BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Wednesday, April 11, 2012

AFRICA MAGIC SWAHILI KUMUOMBOLEZA KANUMBA MWEZI MZIMA.

KITUO cha televisheni cha Africa Magic Swahili kimetangaza kumuomboleza msanii maarufu wa filamu Tanzania Steven Charles Kanumba ambaye alifariki mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuanza kuonyesha filamu za msanii huyo kwa mwezi mzima kutokana na kifo chake ambacho kime washtua mashabiki filamu Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Kama sehemu ya kumbukumbu ya kifo chake kituo hicho kitakuwa kikionyesha sinema zake kuanzia mwishoni mwa wiki hii kama zawadi kwa mchango wake katika tasnia ya filamu Afrika.
Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano na mawasiliano kutoka Multichoice Tanzania Limited Bi Barbara Kambogi alisema kuwa mpango huo utaanza siku ya Jumamosi Aprili 14 saa 19:30 kwa saa za Afrika Mashariki (EAT) ambapo watazamaji wataanza kuangalia filamu ya Uncle JJ, na siku ya Jumapili Aprili 15 muda wa saa 20:00 EAT watangalia filamu ya This is it (sehemu ya 1 na 2).
Alisema kuwa siku ya Jumamosi Aprili 21 saa 19:30 EAT watazamaji wataangali sinema ya More than Pain na siku ya Jumapili Aprili 22 wataangalia filamu ya Young  Billionaire (sehemu ya 1 na 2) ambapo filamu zingine zitaendelea kuonyeshwa siku zinazofuatia.
Marehemu Kanumba akizungumza katika moja ya walsha zilizoandaliwa na Africa magic swahili.
Akimzungumzia Kanumba kutokana na kipaji chake alichokuwa nacho, Mkurugenzi mtendaji wa M-Net Africa Bi Biola Alabi alisema, "Ni lazima tutambue nguvu kijana ambaye amekuwa akifanya vizuri katika tasnia hii. Kifo chake ni hasara kubwa kwa sekta ya burudani Afrika na sisi tunatoa rambirambi zetu kwa familia yake, marafiki na wapendwa wake. "
MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba alifariki dunia siku ya Jumamosi usiku kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa.

No comments:

Post a Comment