BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Monday, April 16, 2012

NORA KURUDI KWA NGUVU NA I CAN’T FORGIVE.

Nuru Nassor
Nora msanii wa filamu Swahiliwood.

MWANADADA Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Nuru Nassor ‘Nora’ baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu katika mambo ya uigizaji wa filamu amerudi tena kwa nguvu zote kwa kuingia na filamu inayojulikana kwa jina la I Can’t Forgive, filamu hiyo ipo sokoni na inakimbiza filamu za wakongwe wanaofanya vizuri.
Akiongea na FC mmoja wa watayarishaji ambaye hakutaka jina lake litajwe katika habari amesema kuwa msanii huyo kuwa ni msanii mwenye uwezo wa hali ya juu sana na kwa upande mwingine ndiye kabeba sehemu kubwa ya filamu hiyo na kuifanya iwe ni ya kipekee zaidi.
“Msanii kama Nora ni wa kiwango cha juu sana iwapo anatumika vizuri katika filamu ya I Can’t Forgive kaitendea haki ameigiza kwa kiwango kikubwa sana ni vema tu wadau wasubiri kazi hiyo nakujionea wenyewe jinsi wasanii walioshiriki katika filamu hiyo walivyoonyesha uwezo wao katika kuigiza,”anasema mtayarishaji huyo

No comments:

Post a Comment