BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limewaasa waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi yao hususan wakati huu wa kuripoti kesi inayomhusu Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Jana na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya MCT Jaji Mstaafu Thomas Mohayo alisema wadau wa tasnia ya habari wamekuwa wakimhukumu moja kwa moja Lulu kuwa ndiye aliyemuua Steven Kanumba.
“Kwa mjibu wa sheria na maadili ya uandishi wa habari mtu yeyote anayekamatwa kwa tuhuma yoyote ile ni mtuhumiwa mpaka atiwe hatiani na mahakama” alisema Jaji Mohayo na kuongea:
MCT inasikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa ukiukwaji mkubwa wa maadili uliojitokeza hivi karibuni wakati vikiripoti kuhusu kifo cha Kanumba vimemuhukumu Lulu kuwa amemuua kinyume na maadili ya kazi yao.
Jaji Mihayo alisema MCT kwa nyakati tofauti imekuwa ikitoa matamko yanayowakumbusha wanahabari kujiepusha na uandishi wa habari au vichwa vya habari vinavyohukumu.
“MCT inatambua fika kesi zilizoko mahakamani ni kivutio kwa umma kutaka kujua kinachopendelea ili kuona haki ikitendeka na pia wanahabari wana haki ya kujua na kuripoti yanayojiri huko na katika vyombo vingine vya sheria” alisema Jaji Mihayo na kuongeza:
Wanahabari ni lazima watambue kunataratibu na makubalianao ya kijamii juu ya namna gani taarifa zinavyopaswa kuripotiwa ili kutowadhuru watu wengine.
Katibu Mkuu wa (MCT) Kajubi Mukajanga alisema mwandishi wa habari anauwezo wa kuifanya jamii ikaamini na kumfikilia Lulu moja kwa moja kuwa ndiye aliyemuua Kanumba kitu ambacho si kweli mpaka sasa.
“Kama sasa munaripoti kuwa Kanumba ameuwawa na Lulu lakini baada ya kesi yake kumalizika ikagundulika hakumuua hatuoni atakuwa katika mazingira ya hatari katika mazingira yanayomzunguka” alihoji Mukajanga.
Mukajanga akifafanua kuhusu taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa na mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha Kanumba kuwa zimesabishwa na Lulu alisema MCT hawahusiki na mitandao hiyo.
“Katiba ya MCT inahusisha vyombo vya habari vya Magazeti,radio na runinga pekee lakini mitandao ya kijamii inaendeshwa na watu tofauti kutokana na katika ya nchi ya kila mtu kuwa na uhuru wa kupata na kutoa habari bila kujalisha kama anataaluma ya uandishi wa habari” alisema Mukajanga.
Mukajanga alisema kutokana na polisi kutotoa taarifa ya wapi Lulu alitakiwa kufikishwa mahakamani ili waandishi wa habari wapate nafasi ya kufanya kazi yao alisema atafuatilia kujua nini kilisababiaha kuwepo kwa usiri huo.
“Nitafuatilia na kuchukua hatua sehemu husika ili kujua kwa nini Polisi walifanya siri kumfikisha Lulu katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kuwafanya waandishi kutokudhuria na kuwasababishia usumbufu wa kupata habari kuona ni hatua gani MCT itachukua” alisema Mukajanga.
No comments:
Post a Comment